Uchaguzi 2020 Tundu Lissu ni mwarobaini wa Upinzani kumng'oa Magufuli

JPM anang'oka 2020.
Yaani hata mkiungana vyama vyote vya upinzani hamuezi kufikisha hata nusu ya kura za JPM .

Chondechonde baada ya uchaguzi hatutaki kusikia mtu ameibiwa kura hapa maana safari tunaenda kuwatembezea kipigo kitakatifu Kuanzia ngazi ya ya udiwani hadi urais.

Yaani mikakati yetu ni kuhakikisha hakuna hata Halmashauri moja inaongozwa na upinzani pili kule bungeni kinakuwa hakuna hata Mbunge mmoja wa upinzani .
 
Huyu magufuli anapaswa kuondoshwa hata kwa nguvu,anatuharibia nchi yetu.
Sisi hatuna na shaka na ushindi wa Magufuli ,tayari ameishashinda tunasubiria kuapishwa kwake tunakiwaza sasa hivi ni kumuongezea muda wa kuongoza.
 
Chadema kama cha Kikuu cha Upinzania Tanzania kimeiva na kiko tayari kuongoza nchi, Umma kwa asasa unakiamini, na hata wafanyamaamuzi kwa sasa wanakiamini chama hiki.

Kisiasa Chama cha siasa katika Uchsguzi hutembea katika madaraja makuu MATANO hadi kufikia kushika madaraka ya nchi (Kushika Dola), Chadema imevuka Daraja la NNE na sasa iko tayari kuingia Daraja la TANO ifikapo October 2020.

1. Daraja la kwanza huwa ni kuunda chama, Chadema imelivuka hili.

2. Daraja la pili huwa ni kupata wabunge angalau 10 hadi 50 hivi kwenye bunge la viti 264. Chdema imevuka hatua hii,

3. Daraja la Tatu huwa kuongeza idadi ya Wabunge ulionao, Chadema imevuka lengo hili tangu chama kianzishwe idadi ya wabunge huongezeka kila uchaguzi.

4. Daraja la nne huwa ni kulinda wabunge ulionao. Chadema imefaulu hili na Uchaguzi huu italinda status hii. Ni wajibu wa chama iki kiendelee kuwepo.

5. Na daraja KUU la TANO huwa ni Kushika Dola. Hapa ndipo tulipo sasa na tunawajibu wa kuchanga karata vizuri chama Kikabebe dola ama kukirejesha nyuma.

Siasa za Tanzania zimebadilika ghafla tangu Jumatatu na sasa nguvu na mvumo kamili wa kumuondoa Magufuli kwa njia halali za kikatiba na kisheria ifikapo October unajidhihirisha tangu Binadamu pekee mwenye miujiza kamili kurejea katika Ardhi ya kitovu chake imara, Si Mwingine nae ni Tundu Antipas Lissu.

Unaweza kujiuliza kwanini ni Tundu Lissu? Jibu linaweza kuwa moja na fupi, kwamba rekodi za Tundu Lissu tangu Magufuli awe Rais zimekuwa ni za kutukuka daima na hazina mfano. Ukianzia kumtazama kuanzia September 7, 2017 kurejea nyuma kabla hajashambuliwa kwa risasi, utajiridhisha kwamba Tanzania imebarikiwa kupata mtu sahihi wa kuwa Rais wa Nchi ambae ni Tundu Lissu.

Huyu ndie pekee mwenye uthubutu wa kumkabili Magufuli kwa maneno, na kwavitendo, angani, majini na aridhini. Huyu ndie anaweza kuwaambia chochote Watanzania na wakamsikiliza na kutenda. Huyu si yule aliyesema urais wa ghasia na maneno mengine meeengi kisha akatuacha Kisutu hadi leo.

Tunajitaji kuiondoa kwanza ccm madarakani, ndipo tujenge misingi yote imara ya Taifa iliyovunjwa na kuharibiwa, Tunahitaji mgombea mwenye kufanya counter-attack kali ukilinganisha na mshindani wetu. Hulka ya ccm na mgombea wao ni chama ambacho kinaamini Tanzania inaongozwa na Katiba na Sheria, huku wakiamini Ccm na mgombea wao ndio Katiba na Sheria zenyewe.

Sasa katika hali hiyo hamhitaji mgombea diplomatic, mtaumia huku mnaoana, Mnahitaji mgombea mwenye counter-attack mara mbili ya mshindani wenu. Dawa ya Moto ni Moto, sio Maji. Na kwa maoni yangu nikiwaangalia Wagongea Saba waliorejesha fomu, Tundu Lissu ni mwiba mkali kwa mpinzani wetu.

Ziko propaganda za ndani na nje kwamba Tume ya Uchaguzi haitamteu kuwa mgombea, kisa ana kesi ama kisa alivuliwa Ubunge na Ndugai kwa hila, Hizi ni propaganda zinazoenezwa na maadui zetu kisiasa ambazo Chadema tukizipokea kijinga tumeliwa.

Ukisoma Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara 39 (d) na (e) vifungu hivyo vinasema wazi sifa za Mgombea Urais, Nanuku,

(d) anazo sifa za kumwezesha kuwa Mbunge au Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi,

(e) katika kipindi cha miaka mitano kabla ya tarehe ya Uchaguzi Mkuu hajawahi kutiwa hatiani katikaMahakama yoyote kwa kosa lolote la kukwepa kulipa kodi yoyote ya Serikali.

Kifungu (d) Katika Katiba ndicho kinachotumiwa na wanapropaganda sana, Swali ni Je, Mh Lissu anazo sifa za kuwa Mbunge? Jibu ni Ndio anazo sifa za kuwa Mbunge kwa kuwa mchakato uliotumika kumvua ubunge ni batili, uliamuliwa na Job Ndugai tu bila kushirikisha vyombo vya maamuzi vya kibunge na Tume ya Maadili ya Utumishi wa Umma. Hivyo kufuta uhalali wa maamuzi ya Ndugai.

Kifungu cha (e), Kwamba Lissu atazuiwa kugombea kisa anakesi Mahakamani, hii ni propaganda hii ni nyepesi, Lissu ana kesi 6 mahakama ya Kisutu na kesi zote hazijafikia mwisho, hazijatolewa hukumu, na hazihusiani na Ukwepaji kodi, bali ni za jinai yaani za uchochezi ambazo haziko kwenye vifungu vya katiba vinavyomzuia mtu kugombea urais.

Akitangaza uamuzi wa Kugombea Urais Mh Lissu alizungumza mengi juu ya Uchumi, Utawala wa Sheria, Bunge, Haki ya Kuishi, Uhuru wa Kutoa maoni na mengine mengi.

Na vile vile alizungumza na kufafanua juu ya proaganda kwamba atakatwa jina lake.

Nanukuu:

"Ninafahamu kwamba baadhi yenu mna hofu kubwa na ya halali kabisa juu ya mimi kuwa na sifa za kikatiba na kisheria za kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano. Hii ni kufuatia uamuzi wa Spika Ndugai wa kunifutia Ubunge mwezi Juni ya mwaka jana. Nitalitolea suala hili ufafanuzi wa kina wa kikatiba na kisheria endapo utahitajika. Itoshe tu kusema kwamba mtu anayekosa sifa za kugombea Urais (au Ubunge) kwa kukiuka masharti ya Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma ni yule tu ambaye amepatikana na hatia ya kukiuka Sheria hiyo na chombo pekee kilichoanzishwa kwa mujibu wa Sheria hiyo, yaani Baraza la Maadili.

Katika utumishi wangu wote kama kiongozi wa umma, mimi sijawahi kutuhumiwa, kushtakiwa, kuitwa kwenye shauri, kutolewa ushahidi wowote dhidi au kwa niaba yangu, na kuhukumiwa na Baraza hilo la Maadili kwa kosa lolote lile chini ya Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma. Aidha, sijawahi kutuhumiwa, kushtakiwa, kuitwa kwenye kesi, kutolewa ushahidi dhidi ya au kwa niaba yangu, kuhukumiwa na kuadhibiwa kwa kosa lolote linaloweza kunifutia sifa za kugombea nafasi yoyote ile ya uchaguzi wa umma kwa mujibu wa Katiba na sheria zetu za Uchaguzi.

Spika Ndugai ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano. Hata hivyo, licha ya dhamana hiyo kubwa ya uongozi aliyonayo kitaifa, yeye sio Baraza la Maadili, na wala sio Mwenyekiti au mjumbe wake. Kwa sababu hiyo, uamuzi wa Spika Ndugai wa kunifutia ubunge haujaniondolea sifa za kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania au nafasi nyingine yoyote ya uongozi.

Kwa hiyo, wananchi wenzangu, nawaombeni wote mniunge mkono katika safari hii ngumu iliyopo mbele yetu" Mwisho wa Kunukuu.

Nje ya hayo, tunahitaji usalama wa Tundu Lissu, Usalama huu unatakiwa kutazamwa kuanzia Geneva Uswis hadi Ikungi Singida Mashariki. Kwamjibu wa sheria za Tanzania mgombea Urais hulindwa na vyombo vya dola, Usalama wa Lissu utakuwa na nguvu kama atatazamwa kama mgombea urais na si Lissu tu. Tangu alipotangaza kwamba atagombea urais, Dunia inamtazama Lissu kama mgombea Urais sio Lissu yule aliyeshambuliwa kwa risasi, hivyo thamani ya Ulinzi wake kidunia inatazamwa kama Mgombea Urais. Na hata Rais Magufuli kama mkuu wa Nchi kiitifaki hata mtazama kama Lissu, bali mgombea Urais, na hata CCM hawatamtazama kama Lissu bali mgombea urais. Ulinzi wake utakuwa na jicho la dunia zaidi kuliko kama Lissu.

Tundu Lissu ni mwarobaini wa Upinzani kumg'o Magufuli.

Na Yericko Nyerere

View attachment 1523072
View attachment 1523066
Ndugu mabandiko yakobm yanaku marefu mnoo, na hatuna time ya kuyasima yote. Anyways nilitaka kukujuza kuwa siku mbili zijazo, Chadema inamchagua mnyiramba mwenzake Nyalandu kupeperusha bendera ya Chadema
 
Ccm wanatakiwa kutolewa madarakani kwa nguvu,huu uchaguzi tufanye tu ili kutafuta kasababu ka kuwaondoa madarakani kwa nguvu Kama walivyofanya wamalawi
Jaribuni muone kitakachotokea, na mkifanya hivyo mtakachokipata hamtarudia tena siyo tu kufanya hata kuwaza kufanya maana mtafyatuliwa vibaya.
 
Wewe ni utopolo,kwa taarifa yako watu wakiamua kuingoa ccm kwa nguvu na Magufuli wao,siku tano ni nyingi sana
 
Shangazi picha ya huyu mwamba inanichekesha sana!
Mwamba sikuhizi anavaa up to date hizi picha hataki hata kuziona. Na kama unazimiliki unapata kesi ya uhujumu uchumi ambayo haina dhamana.
 
Ha ha ha Haha...... Lissu atapata urais wa Twitter au Facebook.. Hata Bob Junior ni Rais ha ha ha.. lkn rais wa masharobaro sio JMT
 
Safari ni mwendo wa kuandika lakini ukweli ni kwamba Magufuli atashinda kwa zaidi ya 80% .
Chama kuondolewa madarakani na upinzani tena upinzani wenyewe wa akina Lissu ni ndoto za alinacha na pia ni kosa ambalo halitakiwi kusameheka Duniani na Mbinguni.

Lissu haamui lolote....

Kinachoamua jambo fulani kutokea ni MAJIRA na NYAKATI...

Hata kama CCM na Magufuli wataamua kutumia uhuni wote walioupata toka kuzimu ili kung'ang'ania madaraka isivyo halali hata baada yq sanduku la kura kuwakataa, lakini kama MAJIRA na NYAKATI za kuondoka kwao zitakuwa zimefika/wadia hakuna wa kuzuia, WATAONDOKA TU na kuiacha nchi inapeta...

Hiyo imani na huo uoga ulionao ni wa kibinadamu. Wakati mwingine, yatazame mambo kwa kutumia jicho la tofauti kidogo....

Acha mazoea...
 
Yetu macho na ngoja niandae kitambulisho changu hatutaki story za kusema oooh tumeibiwa kura hahaha
 
Ccm wanatakiwa kutolewa madarakani kwa nguvu,huu uchaguzi tufanye tu ili kutafuta kasababu ka kuwaondoa madarakani kwa nguvu Kama walivyofanya wamalawi
Aya... kumbuka Upinzani haina watu serikali za mtaa tunavyo post thread hapa. Kila la heri.
 
Yaani hata mkiungana vyama vyote vya upinzani hamuezi kufikisha hata nusu ya kura za JPM .

Chondechonde baada ya uchaguzi hatutaki kusikia mtu ameibiwa kura hapa maana safari tunaenda kuwatembezea kipigo kitakatifu Kuanzia ngazi ya ya udiwani hadi urais.

Yaani mikakati yetu ni kuhakikisha hakuna hata Halmashauri moja inaongozwa na upinzani pili kule bungeni kinakuwa hakuna hata Mbunge mmoja wa upinzani .
Day Dreaming.

Chadema kama cha Kikuu cha Upinzania Tanzania kimeiva na kiko tayari kuongoza nchi, Umma kwa asasa unakiamini, na hata wafanyamaamuzi kwa sasa wanakiamini chama hiki.

Kisiasa Chama cha siasa katika Uchsguzi hutembea katika madaraja makuu MATANO hadi kufikia kushika madaraka ya nchi (Kushika Dola), Chadema imevuka Daraja la NNE na sasa iko tayari kuingia Daraja la TANO ifikapo October 2020.

1. Daraja la kwanza huwa ni kuunda chama, Chadema imelivuka hili.

2. Daraja la pili huwa ni kupata wabunge angalau 10 hadi 50 hivi kwenye bunge la viti 264. Chdema imevuka hatua hii,

3. Daraja la Tatu huwa kuongeza idadi ya Wabunge ulionao, Chadema imevuka lengo hili tangu chama kianzishwe idadi ya wabunge huongezeka kila uchaguzi.

4. Daraja la nne huwa ni kulinda wabunge ulionao. Chadema imefaulu hili na Uchaguzi huu italinda status hii. Ni wajibu wa chama iki kiendelee kuwepo.

5. Na daraja KUU la TANO huwa ni Kushika Dola. Hapa ndipo tulipo sasa na tunawajibu wa kuchanga karata vizuri chama Kikabebe dola ama kukirejesha nyuma.

Siasa za Tanzania zimebadilika ghafla tangu Jumatatu na sasa nguvu na mvumo kamili wa kumuondoa Magufuli kwa njia halali za kikatiba na kisheria ifikapo October unajidhihirisha tangu Binadamu pekee mwenye miujiza kamili kurejea katika Ardhi ya kitovu chake imara, Si Mwingine nae ni Tundu Antipas Lissu.

Unaweza kujiuliza kwanini ni Tundu Lissu? Jibu linaweza kuwa moja na fupi, kwamba rekodi za Tundu Lissu tangu Magufuli awe Rais zimekuwa ni za kutukuka daima na hazina mfano. Ukianzia kumtazama kuanzia September 7, 2017 kurejea nyuma kabla hajashambuliwa kwa risasi, utajiridhisha kwamba Tanzania imebarikiwa kupata mtu sahihi wa kuwa Rais wa Nchi ambae ni Tundu Lissu.

Huyu ndie pekee mwenye uthubutu wa kumkabili Magufuli kwa maneno, na kwavitendo, angani, majini na aridhini. Huyu ndie anaweza kuwaambia chochote Watanzania na wakamsikiliza na kutenda. Huyu si yule aliyesema urais wa ghasia na maneno mengine meeengi kisha akatuacha Kisutu hadi leo.

Tunajitaji kuiondoa kwanza ccm madarakani, ndipo tujenge misingi yote imara ya Taifa iliyovunjwa na kuharibiwa, Tunahitaji mgombea mwenye kufanya counter-attack kali ukilinganisha na mshindani wetu. Hulka ya ccm na mgombea wao ni chama ambacho kinaamini Tanzania inaongozwa na Katiba na Sheria, huku wakiamini Ccm na mgombea wao ndio Katiba na Sheria zenyewe.

Sasa katika hali hiyo hamhitaji mgombea diplomatic, mtaumia huku mnaoana, Mnahitaji mgombea mwenye counter-attack mara mbili ya mshindani wenu. Dawa ya Moto ni Moto, sio Maji. Na kwa maoni yangu nikiwaangalia Wagongea Saba waliorejesha fomu, Tundu Lissu ni mwiba mkali kwa mpinzani wetu.

Ziko propaganda za ndani na nje kwamba Tume ya Uchaguzi haitamteu kuwa mgombea, kisa ana kesi ama kisa alivuliwa Ubunge na Ndugai kwa hila, Hizi ni propaganda zinazoenezwa na maadui zetu kisiasa ambazo Chadema tukizipokea kijinga tumeliwa.

Ukisoma Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara 39 (d) na (e) vifungu hivyo vinasema wazi sifa za Mgombea Urais, Nanuku,

(d) anazo sifa za kumwezesha kuwa Mbunge au Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi,

(e) katika kipindi cha miaka mitano kabla ya tarehe ya Uchaguzi Mkuu hajawahi kutiwa hatiani katikaMahakama yoyote kwa kosa lolote la kukwepa kulipa kodi yoyote ya Serikali.

Kifungu (d) Katika Katiba ndicho kinachotumiwa na wanapropaganda sana, Swali ni Je, Mh Lissu anazo sifa za kuwa Mbunge? Jibu ni Ndio anazo sifa za kuwa Mbunge kwa kuwa mchakato uliotumika kumvua ubunge ni batili, uliamuliwa na Job Ndugai tu bila kushirikisha vyombo vya maamuzi vya kibunge na Tume ya Maadili ya Utumishi wa Umma. Hivyo kufuta uhalali wa maamuzi ya Ndugai.

Kifungu cha (e), Kwamba Lissu atazuiwa kugombea kisa anakesi Mahakamani, hii ni propaganda hii ni nyepesi, Lissu ana kesi 6 mahakama ya Kisutu na kesi zote hazijafikia mwisho, hazijatolewa hukumu, na hazihusiani na Ukwepaji kodi, bali ni za jinai yaani za uchochezi ambazo haziko kwenye vifungu vya katiba vinavyomzuia mtu kugombea urais.

Akitangaza uamuzi wa Kugombea Urais Mh Lissu alizungumza mengi juu ya Uchumi, Utawala wa Sheria, Bunge, Haki ya Kuishi, Uhuru wa Kutoa maoni na mengine mengi.

Na vile vile alizungumza na kufafanua juu ya proaganda kwamba atakatwa jina lake.

Nanukuu:

"Ninafahamu kwamba baadhi yenu mna hofu kubwa na ya halali kabisa juu ya mimi kuwa na sifa za kikatiba na kisheria za kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano. Hii ni kufuatia uamuzi wa Spika Ndugai wa kunifutia Ubunge mwezi Juni ya mwaka jana. Nitalitolea suala hili ufafanuzi wa kina wa kikatiba na kisheria endapo utahitajika. Itoshe tu kusema kwamba mtu anayekosa sifa za kugombea Urais (au Ubunge) kwa kukiuka masharti ya Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma ni yule tu ambaye amepatikana na hatia ya kukiuka Sheria hiyo na chombo pekee kilichoanzishwa kwa mujibu wa Sheria hiyo, yaani Baraza la Maadili.

Katika utumishi wangu wote kama kiongozi wa umma, mimi sijawahi kutuhumiwa, kushtakiwa, kuitwa kwenye shauri, kutolewa ushahidi wowote dhidi au kwa niaba yangu, na kuhukumiwa na Baraza hilo la Maadili kwa kosa lolote lile chini ya Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma. Aidha, sijawahi kutuhumiwa, kushtakiwa, kuitwa kwenye kesi, kutolewa ushahidi dhidi ya au kwa niaba yangu, kuhukumiwa na kuadhibiwa kwa kosa lolote linaloweza kunifutia sifa za kugombea nafasi yoyote ile ya uchaguzi wa umma kwa mujibu wa Katiba na sheria zetu za Uchaguzi.

Spika Ndugai ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano. Hata hivyo, licha ya dhamana hiyo kubwa ya uongozi aliyonayo kitaifa, yeye sio Baraza la Maadili, na wala sio Mwenyekiti au mjumbe wake. Kwa sababu hiyo, uamuzi wa Spika Ndugai wa kunifutia ubunge haujaniondolea sifa za kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania au nafasi nyingine yoyote ya uongozi.

Kwa hiyo, wananchi wenzangu, nawaombeni wote mniunge mkono katika safari hii ngumu iliyopo mbele yetu" Mwisho wa Kunukuu.

Nje ya hayo, tunahitaji usalama wa Tundu Lissu, Usalama huu unatakiwa kutazamwa kuanzia Geneva Uswis hadi Ikungi Singida Mashariki. Kwamjibu wa sheria za Tanzania mgombea Urais hulindwa na vyombo vya dola, Usalama wa Lissu utakuwa na nguvu kama atatazamwa kama mgombea urais na si Lissu tu. Tangu alipotangaza kwamba atagombea urais, Dunia inamtazama Lissu kama mgombea Urais sio Lissu yule aliyeshambuliwa kwa risasi, hivyo thamani ya Ulinzi wake kidunia inatazamwa kama Mgombea Urais. Na hata Rais Magufuli kama mkuu wa Nchi kiitifaki hata mtazama kama Lissu, bali mgombea Urais, na hata CCM hawatamtazama kama Lissu bali mgombea urais. Ulinzi wake utakuwa na jicho la dunia zaidi kuliko kama Lissu.

Tundu Lissu ni mwarobaini wa Upinzani kumg'o Magufuli.

Na Yericko Nyerere

View attachment 1523072
View attachment 1523066

Waziri wa Zamani wa Vitalu anaenda kumng’oa Jamaa yako,Pesa pesa,Wajumbe wa Mikoani wana njaa,Inawezekana jamaa kashamaliza Mchezo zamani mnooo,Ndo maana juzi ka tweet kuwa wajumbe wasiingiliwe na Miongozo kutoka juu!Anajua analolifanya!Nyalanguu!
humpendi hana uwezo sawa ila ana fedhaaaa!Subiria Uone kitakachotokea!
 
Chadema wana kazi moja tu sasa nayo ni kupanga mikakati yao ya mambo ya kuyafanya baada ya kuchukua nchi hapo October 2020.
Njia ni nyeupe sana kwa Lissu. Amini nakwambia njia ni nyeupe sana kwa Lissu. Ajipange tu

wewe Unaota Au Na Nyalanguu waziri wa Vitalu vya Maliasili wa zamani unamuacha wapi?unajua nguvu ya fedha weye kwa wajumbe?
Subiria Uje kuona Maajabu! nani atawakilisha Chadema!
 
Chadema wana kazi moja tu sasa nayo ni kupanga mikakati yao ya mambo ya kuyafanya baada ya kuchukua nchi hapo October 2020.
Njia ni nyeupe sana kwa Lissu. Amini nakwambia njia ni nyeupe sana kwa Lissu. Ajipange tu
Ama kwa hakika tume yetu ni huru na matokeo yatakuwa mazuri sana na huyo mheshimiwa atatangawa
 
Back
Top Bottom