Hayo maneno, kwamba amekuwa hivyo kwa sababu ya risasi, unampamba tu. Kwa wale tunaomjua Lissu hajabadilika. Maisha yake yote haheshimu mamlaka. Kwake yeye ndiye mamlaka ya mwisho. Ushahidi ni maneno aliyoyatamka wakati wa kuomba kura kwenye Mkutano wa Baraza Kuu la CHADEMA. Hayo maneno yanawakilisha kwa 100% tabia yake.
Lissu, anajua fika kuwa kesi zinazomkabili zinamweka katika mazingira magumu. Kwenye huo mkutano, akijibu swali kuhusu hizo kesi alijigamba kuwa hatishiki. Kwa hivyo anatafuta njia ya kutokea, ambayo ni ya yeye kuchaguliwa na chama chake kuwa mgombea wa Urais. Kichwani mwake, kwa jeuri aliyo nayo, anamini kuwa, kama mgombea Urais, kutampa kinga dhidi ya hukumu na kitendo chake cha kufutiwa dhamana, baada ya wadhamini kujitoa.
Na isitoshe ana "kiporo" cha kueleza kuhusu tukio la kushambuliwa, wakati dereva, shahidi wake muhimu, kafichwa.