Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Nikiibiwa kura nitawaingiza Wananchi barabarani

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Nikiibiwa kura nitawaingiza Wananchi barabarani

Hayo maneno, kwamba amekuwa hivyo kwa sababu ya risasi, unampamba tu. Kwa wale tunaomjua Lissu hajabadilika. Maisha yake yote haheshimu mamlaka. Kwake yeye ndiye mamlaka ya mwisho. Ushahidi ni maneno aliyoyatamka wakati wa kuomba kura kwenye Mkutano wa Baraza Kuu la CHADEMA. Hayo maneno yanawakilisha kwa 100% tabia yake.

Lissu, anajua fika kuwa kesi zinazomkabili zinamweka katika mazingira magumu. Kwenye huo mkutano, akijibu swali kuhusu hizo kesi alijigamba kuwa hatishiki. Kwa hivyo anatafuta njia ya kutokea, ambayo ni ya yeye kuchaguliwa na chama chake kuwa mgombea wa Urais. Kichwani mwake, kwa jeuri aliyo nayo, anamini kuwa, kama mgombea Urais, kutampa kinga dhidi ya hukumu na kitendo chake cha kufutiwa dhamana, baada ya wadhamini kujitoa.

Na isitoshe ana "kiporo" cha kueleza kuhusu tukio la kushambuliwa, wakati dereva, shahidi wake muhimu, kafichwa.
Unajua sana kubumba na kuokoteza vijihadithi na kuaminisha wenye umakini haba, sijui ni mganga wa kienyeji au msaidizi wake ?
 
Akusanye ukoo wake aingie barabarani atuache kwanza watu hatujitaji vita hata covid tumeiondoa [emoji23][emoji23][emoji23]tustarehe
 
Sidhani kama wananchi watakuwa tayari kuingia barabarani kwa faida za wanasiasa.
Kauli hizi si tu ni hatari kwa usalama wa nchi bali ni hatari hata kwa yeye mwenyewe.
Hekima ya Mwenyezi Mungu inahitajika kumuongoza Mh. Lissu katika mbio za Urais, mtu mmoja hawezi kuwaingiza watu barabarani labda kama kuna mpango waliokwisha kuuandaa muda mrefu.
Usiwasemee wananchi. Uoga wa kukubali na kujivunia kuonewa na kunyanyaswa, ni wako mwenyewe
 
Wakiingia barabarani ni kipigo tu akuna maelezo mengine.

Unadhani ni sisimizi watakuwa barabarani eti uwapige tu?

Kama mnadhani nchi hii ni ya mama na baba zenu tutawaona.....

Mtapigwa upofu mpaka mtaombapoo...
 
Usiwasemee wananchi. Uoga wa kukubali na kujivunia kuonewa na kunyanyaswa, ni wako mwenyewe
Sijaona mantiki ya sentensi zako.
Ingawa mwishoni umeishia kueleza nilichoeleza "mtu mmoja asiwafanye wengine kuumia kwa maslai yake /kikundi chake ",hivyo basi hoja za kuonewa, kunyanyaswa na nk ziko ndani ya mtu mmoja/kikundi fulani cha watu.
Huo ujasiri wa kuwasemea watu wao wameutoa wapi?
 
Hivi UKUTA iliishia wapi enzi zile.
Huu uchaguzi utakuwa mwepesi sana kuwahi kutokea ktk historia ya nchi hii.
 
Hiyo ndio Kauli ya Tundu Lissu iwapo ikitokea ameshindwa kwenye Uchaguzi Mkuu mwezi October 2020.

Tundu Lissu amepitishwa na CHADEMA kuwania Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama hicho. Lissu amenukuliwa akisema ataingiza Watanzania barabarani ikiwa ataibiwa kura zake.


My Take: Ni mapema sana kwa Mgombea wa Urais kutoa kauli kama hii si kiashiria kizuri. Anataka kutuaminisha kuwa hata ikitokea ameshindwa kihalali tuamini kuwa kaibiwa kura ili atimize azima yake.

Uongozi wa CHADEMA umshauri huyu mgombea kauli hizi hazifai kwa usalama wa nchi yetu.
Wekeni tume inayotokana na vyama vyote vya siasa ili tumsute kesho yake akikulazimisha uingie barabaran
 
Karibu barabarani. Tena this time, watafanya makusudi ili ionekane umeibiwa ili uingie na wewe barabarani. Wanakutamani kinoma, usijishaue ukidhani wanakuogopa sabb ya mdomo wako. Njoooo tu baba, uchukue kura zako barabarani.

Mnataka usalama, dawa ni moja tu...

MSIIBE KURA. TUSHINDE KWA HAKI. ASHINDE KWA HAKI...

There's no way out....

Hii siyo nchi ya BABA na MAMA zenu. This time mtathibitishiwa hili...!!!
 
Hapo mbona bado sana ngoja muda wa campaign aanze kuongelea mambo ya kuvunja muungano, kumwita Nyerere mtu wa ovyo na hadithi yake isiyoisha ya risasi kumi 16.

Jamaa ni narcissist he rates himself so highly wenzake wanaenda kwenye campaign kwa porojo za watawafanyia nini wananchi, yeye anakwenda na agenda ambayo anaifahamu mwenyewe.

Yaani kichwani kwake keshaanza kuchagua rangi ya pazia atazoweka Ikulu; ni swala la muda kabla ya watu kukubali huyu mtu anahitaji psychological intervention ajatulia bado kutokana na mkasa uliompata na wala hana sifa za high office.
Hahaaaa eti rangi za Pazia,
Mpaka ile October ni bandika bandua hili season la uchaguzi.
 
Huyu bwana huwa namkubali sana kwa misimamo nahisi atakuwa ameumbwa tofauti kabisa na akina Fulani ambao wakitikiswa kidogo tu kesho utawasikia wanasema "nimeamua kujiunga na ccm ili kuunga mkono juhudi za magufuli"

Naamini kwa ujasiri wake lazima October hii tutakuwa tumemfurusha mtu kutoka magogoni ukizingatia CCM yenyewe wakiwamo mawakala wa wagombea wao hawaelewani kabisa kwa sababu ya zile mambo za wajumbe

Tegemeo pekee la maccm ilikiwa ni watu wasiojulikana lakini kwa sasa na wao hata hawajui hatima yao maana hawajapata tenda toka sijui mwezi wa ngapi
 
Mnaota ndoto, muulize mbowe alivyokimbia siku ya akwilina, utafikiri mwanariadha wa kenya.
WEWE ndio bado una ndoto za watoto wa chekechea. Na hayo ya Acquilina, Mwangosi, Mawazo lazima tuje kuyafukua upya.
 
Nawazungumzia watanzania hawahawa ambao walilazimisha Mwalimu Nyerere ang'atuke mwaka 1985. Au unadhani alikuwa anataka kuachia madaraka ??? Soma historia ufahamu matukio ambayo yule Mzee alifanyiwa na watanzania kuanzia mwaka 1980-1985: Halafu ukiwa na ufahamu utatambua kwamba kama busara haitatumika basi tunaweza kuona ule ukurasa mwekundu unajirudi hapa nchini. Be vigilant my friend, Raisi Magufuli analivuruga Taifa.

Ubaya wa Afrika ni huu, tofauti kabisa na Ulaya ambako mapinduzi yalifanywa na wananchi huku kwetu huwa yanaanzishwa na maafisa wa vyombo vya usalama wakishirikiana na wanasiasa. Nimesoma vizuri siasa za mapinduzi duniani kama sehemu yangu ya masomo ya Chuo Kikuu,na nikafanya Case Study yangu Afrika.

Hivyo navyokwambia kwamba Tanzania iko pabaya sana namaanisha ninachokwambia maana dalili zote zinaonekana, na sifahamu kwanini wenzangu ambao ni wasomi na mko Serikalini au kwenye chama hamyaoni haya na hamna hata chembe ya woga. Tunaweza tukakaa hapa JF tukiandika Propaganda kuwatishia wananchi vifo lakini ukweli ni kwamba watu ambao wanaweza kulivuruga hili taifa na serikali wako huko huko serikalini (TISS, JWTZ na CCM).

Soma vizuri historia na uchambue mambo kwa hekima utafahamu kwamba Lissu is not a threat entirely but an agent of chaos or in other words A man who opens Pandora's box.

You are really a GREAT THINKER...

Nakubaliana na wewe kwa 100%...

"....Lissu is not a threat entirely, but an AGENT of chaos or in other words, A MAN WHO OPENS THE PANDORA BOX....."

Hii statement imefunga na kumaliza kila kitu. Only GT can understand the logic in it....

Haya ni MAJIRA na NYAKATI ya kubadili mwelekeo wa Tanzania hii...

Sijui ni kwa nini watu hawaoni na kuelewa haya mambo???
 
Pimbi 2 Yani anataka kufanya yeye ndo rais 🐵🐵🐵🐵
 
You are really a GREAT THINKER...

Nakubaliana na wewe kwa 100%...

"....Lissu is not a threat entirely, but an AGENT of chaos or in other words, A MAN WHO OPENS THE PANDORA BOX....."

Hii statement imefunga na kumaliza kila kitu. Only GT can understand the logic in it....

Haya ni MAJIRA na NYAKATI ya kubadili mwelekeo wa Tanzania hii...

Sijui ni kwa nini watu hawaoni na kuelewa haya mambo???

Tatizo ni matendo ya kinyama na kidikteta yanayofanywa na mtu mmoja mfupi kutoka chattle tena mbele ya macamera na mamic plus mayoutube
 
Mnataka usalama, dawa ni moja tu...

MSIIBE KURA. TUSHINDE KWA HAKI. ASHINDE KWA HAKI...

There's no way out....

Hii siyo nchi ya BABA na MAMA zenu. This time mtathibitishiwa hili...!!!
Unabweka nyuma ya mlango uje barabarani uone robot wanavyokunywa damu.
Kuna watu wamefundishwa kupiga na wengine kuua kabisa lakini leo mwaka wa tano amekaa tu analamba pesa ya bure!!
 
Back
Top Bottom