Nimesoma habari ya gazeti la Mwananchi kuhusu swala la Lissu kujiandaa na Urais 2020 hivyo kufanya idadi ya wagombea waliokwisha kutangaza nia ya kugombea Urais kwa tiketi ya Chadema kinyume kabisa na miongozo ya chama hicho kwa watia nia wake kuwa wawili mpaka sasa yaani Lissu na Lowassa.
Miongozo ya CHADEMA inawataka watia nia wa Urais kutangaza nia hiyo mwaka mmoja kabla ya Uchaguzi mkuu ili kuepusha mpasuko ndani ya Chama. Aidha yuko Mbowe nae anataka kugombea Urais ila hatangazi ili apate nafasi ya kuwaengua wanaotangaza mapema wakati ukifika.
Kwa tunaomjua Lissu tunaamini kabisa kuwa hawezi kuwa kwenye nafasi kubwa kama Urais kwa sababu kubwa kuwa hayuko settled. Lissu anapaswa kuwa na chombo au mtu wa juu yake kumdhibiti. Lissu ni kama Lema, Wenje na sampuli hizo. Ni waongeaji, wakosoaji na wakitumwa kusemea jambo wana uwezo mkubwa wa kufanya.
Udhaifu wao mkubwa ni kwamba hawawezi kukaa kwenye kikao dakika 20 bila kutoka nje. Wako mbio mbio muda wote. Hawana ubunifu wao ni watekelezaji tu, ni watu wa visasi na makundi, wamekubuhu kwenye fitina hawa wote ndio walimpoteza Lytonga Mrema kwa kumgombanisha na wenzake akina Marando sasa wameshamgombanisha Mbowe na waliokuwa wapenzi wake akina Zitto, Dr. Slaa sasa wanataka Urais.
Dhambi kubwa ya Zitto na Dr Slaa CHADEMA ilikuwa ni kutangaza kugombea Urais. Waliosimamia mkakati wa kuvunja ndoto zao ni hawa vijana wa Lytonga Mrema waliotoka nae NCCR kwenda TLP halafu wakamtelekeza kule na kukimbilia CHADEMA. Kwasababu ni wabaguzi dhambi ile hawajawahi kuiacha ni sawa na kula nyama ya mtu.
Mimi binafsi namuunga mkono Lissu kuwa mwenyekiti wa CHADEMA kwa sababu ndio pekee ninayemuona ana ujasiri wa kupambana na Mbowe japo hana mkakati. Simuungi mkono kwa sababu yeye atakuwa mwenyekiti mzuri kuliko Mbowe la hasha ila atavunja mwiko na kufungua mlango uliofungwa miaka mingi wa kupokezana vijiti ndani ya CHADEMA.
Aidha Lissu atatoa changamoto kwa siasa za upinzani nchini na kuzinogesha. Nampa tahadhari Lissu kuwa kama amesharubuniwa na Mbowe kuwa ataachiwa Urais na yeye aachie uenyekiti ameshashindwa kabla ya kuanza.
Kwa sasa Lissu focus kwenye Uenyekiti wa CHADEMA kwanza Urais unakuja tu wenyewe.
Nakutakia uponaji wa haraka Kamanda