Tundu Lissu: Niliwahi kufanya kazi katika kampuni iliyokamata ndege ya Tanzania Uholanzi. Kauli hii inakupa hisia gani?

Uo ukakas umeamua wewe ila ukiwa positive utagundua umuhimu wake
 
Kabisa
 
Usaliti mkubwa uko serikalini mwenu.

Kama hamna uwezo wa kulipa semeni aliyeshikilia ndege auze apate chake.

Sent from my SM-N9150 using JamiiForums mobile app
 
..makampuni yote ya uwekezaji toka nje lazima yatafute Wanasheria wa Kitanzania watakaowaongoza ktk masuala ya mikataba.

..kwa msingi huo kampuni yoyote ile ya kigeni unayoiona hapa Tanzania ujue kwamba masuala yake yakisheria yanasimamiwa na mawakili wa Kitanzania.

..Vilevile kama kampuni hiyo toka Sweden ingeamua kuishitaki serikali ktk mahakama za hapa nyumbani basi kesi hiyo ingefunguliwa na kusimamiwa na mawakili Watanzania, au wakili aliyesajiliwa kutetea kesi ktk mahakama za Tanzania.


..Ukiuelewa msingi huo utaona kwamba hakukuwa na tatizo kwa Tundu Lissu kutoa ushauri wa kisheria kwa kampuni ya Kiswidish.

..Tatizo liko kwa wanasheria wa serikali ambao hawakutumia taaluma zao vizuri ktk kuishauri serikali na kupelekea mkataba kuvunjwa kimakosa na serikali kushindwa kesi ktk mahakama ya usuluhishi ya kimataifa.
 
Labda hata alikuwa Lawyer wao. Information zote alikuwa anawapa yeye. Mkono Advocates aliwatetea wazungu kulikamua Taifa.

Mtu kama huyu awe Rais?
 
Labda hata alikuwa Lawyer wao. Information zote alikuwa anawapa yeye. Mkono Advocates aliwatetea wazungu kulikamua Taifa.

Mtu kama huyu awe Rais?

..nini maana ya kuandikishana MKATABA?

..Ukiandikishana mkataba na mtu / kampuni yoyote maana yake mmeaminiana na mnapeana information zote.

..Suala linapokwenda mahakamani maana yake ni kwamba mkataba umekiukwa, upande unaoshitaki unaona haujatendewa haki na upande mwingine.

..Dhana kwamba Mkono Advocates waliwatetea wazungu kuwakamua Watanzania ni potofu. Pia ni imani potofu kuamini ktk kukamuana. Mtanzania hatakiwi kukamuliwa, na Mzungu hapaswi kukamila.

..Kila anayetembea ktk ardhi ya Tanzania anatakiwa ajisikie salama, na mwenye HAKI sawa na wengine.
 
Hiyo kesi ukisoma vizuri inaelekea Mawakili wa Tanzania wala hawkuhudhuria na mahakama ya kimataifa iliwateulia mwakilishi aliesimamia maslahi ya Tanzania na waliposhindwa hukumu ikawa halali.Watanzania wajiulize je hiyo wizara ya sheria kwa nini hawakufuatialia hili swala??ni dharau au jeuri??hata sasa wamekata rufaa lakini hawana mwakilishi kwenye mahakama ya kimataifa je hiyo rufaa itasimamiwa na nani??!
 

..halafu serikali inashtakiwa na makampuni hata ya ndani ya Watanzania.

..tatizo ni kuwa hata kampuni ikishinda kesi dhidi ya serikali, sheria zetu zinakataza kukamata mali za serikali kutekeleza hukumu.

..Nina hakika makampuni ya wazawa Watanzania wanatamani wangekuwa na uwezo wa kisheria kutumia mahakama za nje badala ya mahakama za ndani.
 

..Hiyo ni hoja nzuri sana.


..Waziri wa Sheria, Mwanasheria Mkuu, na Wakili Mkuu wa serikali, wanapaswa kuhojiwa kuhusu suala hilo.


..Hao ndio wanaotakiwa kulaumiwa kwa kukosa uzalendo na kuuza mechi.
 
Huyu sasa ndiye aliyepaswa kuwa Mwanasheria mkuu wa Serikali mahali wanapozingatia weledi na umahiri.
 

..waliosoma taarifa kuhusu mwenendo wa hiyo kesi wanadai serikali ya Tanzania haikutuma mawakili wa kuitetea.


..sasa huoni kama Waziri wa Sheria,Mwanasheria Mkuu, na Wakili Mkuu wa serikali, wamefanya uzembe na kuiingiza nchi hasara?
 
Kwa nini nyie mliingia mikataba ya hovyo ??
Lissu ndio alikuwa anawachochea wafungue kesi, wao hawakuwa na haja na kesi, ni kama zile za migodi, jambo jema watu wa migodi walimpuuza, isipokuwa watatu ambao ni rafiki zake, na anahisa katika kampuni zao.
 
Kwa nini mliingia mikataba ya hovyo??
Mliongia mikataba ya hovyo ndio mlipaswa muanzwe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…