Tundu Lissu: Niliwahi kufanya kazi katika kampuni iliyokamata ndege ya Tanzania Uholanzi. Kauli hii inakupa hisia gani?


Nimekuambia usilalamike tu, toa mifano ya uongo wa Lissu kama ambavyo sisi tunatoa mifano ya makosa na ushenzi wa viongozi wa CCM likiwemo hili la kuingia mikataba ya hovyo halafu hao hao wanakuja kuivunja na nchi kutakiwa kulipa fidia...

OFCOZ YES, sisi wengine tunawelewa na kumwamini sana tu TUNDU LISSU kwa sababu anatufumbua macho watanzania kupitia maarifa na ufahamu wake wa sheria za taifa na kimataifa...

Na kama wewe unaona shida sisi kumfanya TL kama "mungu mtu" wetu, basi wewe na wenzako huko mfanyeni Magufuli au hata Samia viwe vi-mungu mtu vyenu halafu tukutane ktk ulingo wa HOJA tuone nani atakuwa "the last man standing.."

NDIYO. Tufanye kama Nabii Eliya na Mungu wa kweli alivyochuana na miungu ya mke wa mfalme Ahabu wa Israel ya kale aitwaye Yezebeli na miungu yake iliyokuwa inaitwa Mabaali
 
Kama umekubali kumfanya Lissu kuwa Mungu kwako basi sawa maana kila mtu ana uhuru wa kuchagua kuamini atakacho. Maana mie hoja yangu ni ilikuwa huko kumfanya Lissu kuwa kama Mungu ila kama umekiri hilo basi mie sina la kusema.
 
Kama umekubali kumfanya Lissu kuwa Mungu kwako basi sawa maana kila mtu ana uhuru wa kuchagua kuamini atakacho. Maana mie hoja yangu ni ilikuwa huko kumfanya Lissu kuwa kama Mungu ila kama umekiri hilo basi mie sina la kusema.

..Lissu ana mapungufu yake kama mwanadamu yeyote yule.

..Pia anayo baadhi ya mitizamo na misimamo ambayo sio sahihi, au ina makosa.

..Lakini kwa kiwango kikubwa Lissu ni mtetea HAKI.

..Lissu pia ni MKWELI kuliko wanasiasa wengi hapa nchini.

..Ni mtu mwenye UJASIRI wa kuwaambia watawala mambo ambayo hawapendi kuyasikia, au hawataki wananchi tuyafahamu.

..Tatizo ninaloliona mimi ni kikundi fulani kujaribu kufanya character assasination dhidi ya Lissu.

..Kuna kikundi ambacho hakijishughulishi na kujibu hoja za Lissu, bali kimejizatiti kumchafua, na kumjengea taswira mbaya machoni mwa Watanzania.

..Lissu ni Mtanzania, mzalendo, mkweli kwa nchi na watu wake.
 
Mlipa deni ndio mtanzania, sasa walichosaliti ni kipi eleza? Wamesaliti au wametia hasara?

..nadhani usaliti ni tuhuma mbaya na kubwa.

..lakini kuna kipindi tuhuma hiyo ilianza kutumiwa na watu fulani dhidi ya mtu fulani.

..matokeo yake usaliti imekuwa tuhuma inayotumika hovyo-hovyo bila kuzingatia uzito wake.

..swali ambalo tunatakiwa kujiuliza ni kama wahusika walichukua TAHADHARI za kutosha kabla ya kufanya maamuzi ya kuvunja mkataba.

..vilevile kama wahusika walifanya JITIHADA za kutosha kuitetea nchi ili tusiingie hasara ya kulipa faini kubwa kiasi hiki.

..Nchi hii ni MASIKINI. Billioni 300++ ni fedha nyingi sana. Kama sijakosea ni zaidi ya bajeti ya maendeleo ya wizara ya kilimo.

..Sasa kipi ni sahihi kufanyika?

..Je, tukae hapa tukimtukana Tundu Lissu na kumpa lawama za uongo kuhusu kadhia hii?

..Au tudai waliochukua maamuzi ya kuvunja mkataba na kushindwa kutetea kesi wawajibike?
 
Advocate and client relationship Iko protected na sheria, hapo mwenzio alikuwa anatoa ushauri WA kisheria i.e alikuwa kazini
 
Terminator lissu siyo mzalendo,ni bora ngamia kupenya katika tundu LA sindano
 
Ni dalili kwamba yuko tayari kuuza nchi.. Kwa maslahi yake binafsi na mabeberu
 
Ni dalili kwamba yuko tayari kuuza nchi.. Kwa maslahi yake binafsi na mabeberu
Kabisa, nadhani Kuna jinsi anapata mgao kutoka kwa hizo kampuni za kibeberu
 
Ni mitizamo na misimamo ipi ya Lissu hiyo ambayo ina makosa?
 
Kama kweli Lissu ni msaliti basi huyo ndio adui wetu wa kwanza kisha ndio wanafuata hao wengine, huwezi kufanya usaliti kwa taifa lako halafu bado ukawa unahesabika ni raia mwema.
 
Ni mitizamo na misimamo ipi ya Lissu hiyo ambayo ina makosa?

..msimamo wake kuhusu devolution of central govt nadhani ni mkali sana au wa kihafidhina.

..naamini tunatakiwa kuteremsha madaraka kwa wananchi lakini sio kwa kiwango anachopendekeza Lissu.
 
Kama kweli Lissu ni msaliti basi huyo ndio adui wetu wa kwanza kisha ndio wanafuata hao wengine, huwezi kufanya usaliti kwa taifa lako halafu bado ukawa unahesabika ni raia mwema.

..Lissu amefunguliwa makesi mengi sana hapa Tanzania.

..Wameanza kumfungulia makesi tangu miaka ya 90.

..Kama angekuwa msaliti, au ana fanana na tuhuma hizo, watawala [ mkapa, kikwete,magufuli ] wangemfungulia kesi hiyo, au inayokaribiana na hiyo.

..Hii habari ya kumuita msaliti bila ya kumfikisha mahakamani ni jitihada za kumchafua na kumbomoa Lissu ili asiaminike na wananchi. Hiyo ni mbinu ambayo imetumika dhidi ya wanasiasa wengi waliokuwa mwiba kwa serikali.
 
Huo sio usaliti, tafuta jina lengine usilazimishe kutumia neno la usaliti.
Tafuta wewe..

Kwangu mimi hili ndilo sahihi kwa watu wote waoneshao tabia ya usaliti.. Ndiyo viongozi wa CCM na serikali yao...

Hawa wamewasaliti wana wa nchi hii na sasa badala ya kula matunda ya UHURU wanakula machungu toka kwa wakoloni weusi...
Hao waliyoingia hiyo mikataba ndio wasaliti kwa sababu kwa niaba yetu wameingia mikataba ya hovyo isiyo na maslahi kwa taifa na huyo Lissu kama kweli anafanya haya yanayosemwa basi nae ni msaliti.
Alaa!, Bhageshi unalalama nini sasa iwapo umekwisha kutambua kuwa walioingia mikataba na kuivunja na nchi kupata hasara ndiyo wasaliti?

Otherwise kama TL na CHADEMA ndiyo waliingia mikataba hiyo na kisha kuanza kuivunja, basi hawa ni kweli kabisa ni wasaliti...!!
 
Mimi nimemaliza, wewe pambana na Karma ya maneno yako uliyoandika. Pole maana naona kichwa Sasa kimeponza mwili.
Tangu lini shetani akamlaani mwenye haki? Ni sawa na Farao wa Misri ya kale eti amlaani Israel...!!

It's impossible on earth & heaven...!

Hayo yameshachomoka kuja kwenu na hayatarudi hadi yatende kazi yake...

Kutotenda kazi kwa maneno haya ni mpaka mjisalimishe upande wa haki, upande wa wana wa nchi hii..!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…