The Palm Beach
JF-Expert Member
- Dec 30, 2015
- 1,967
- 4,267
Mbona nimetoa sababu hapo kwanini Lissu anafanywa kuwa kama Mungu. Lissu kila analosema yeye ndio sahihi, mawazo yake yeye ndio sahihi kuliko mtu yeyote, hamkubali kuona mtu akimkosoa Lissu mtaanza kumshambulia hamuamini kwamba Lissu nae anakosea, mmeanza kutuambia kama taifa tuwe tunamsikiliza Lissu kila anachoshauri.
Kiujumla mnatuaminisha kuwa Lissu ni bora kuliko wengine, mtu msiyetaka akosolewe mtu msiye amini kama anakosea kama wengine mtu ambaye mmejisalimisha kwake mtasikiliza na kukubali kila anachosema huyo ni mungu.
Nimekuambia usilalamike tu, toa mifano ya uongo wa Lissu kama ambavyo sisi tunatoa mifano ya makosa na ushenzi wa viongozi wa CCM likiwemo hili la kuingia mikataba ya hovyo halafu hao hao wanakuja kuivunja na nchi kutakiwa kulipa fidia...
OFCOZ YES, sisi wengine tunawelewa na kumwamini sana tu TUNDU LISSU kwa sababu anatufumbua macho watanzania kupitia maarifa na ufahamu wake wa sheria za taifa na kimataifa...
Na kama wewe unaona shida sisi kumfanya TL kama "mungu mtu" wetu, basi wewe na wenzako huko mfanyeni Magufuli au hata Samia viwe vi-mungu mtu vyenu halafu tukutane ktk ulingo wa HOJA tuone nani atakuwa "the last man standing.."
NDIYO. Tufanye kama Nabii Eliya na Mungu wa kweli alivyochuana na miungu ya mke wa mfalme Ahabu wa Israel ya kale aitwaye Yezebeli na miungu yake iliyokuwa inaitwa Mabaali