Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Nimepokea vitisho vya kuuawa. Wanachama wawasindikize wagombea Ubunge na Udiwani kuchukua fomu NEC

Sijasikia akisema atawafanyia nini watanzania. Lissu sio mtu sahihi kupambana na Magufuli. Magufuli alihitaji mtu kama lowassa wa 2015.
Kwani kampeni zimeanza? Shule za kata ni tatizo nchi hii
 
Ni sawa na ile hadithi ya:-
"Hapa hapa(uzwi)!!
Hapa hapa(uza)!!"
 
Hata uchaguzi wa S/M wakurugenzi walileta porojo hizo hizo , safari hii hatumwi mtoto dukani
 
Kumbe huwa mnamkiri kuwa JPM ni Amiri Jeshi Mkuu?
Vizuri sana kijana. Sasa subiri aendelee kuwa Amiri Jeshi Mkuu wako hadi 2025!

TUKUTANE OKTOBA 28!

Kwani kuwa amiri jeshi mkuu ni mpaka nikiri, au ukishakuwa rais cheo cha amiri jeshi mkuu ni automatically. Ni wapi nimebisha kuwa yeye ni amiri jeshi mkuu? Kuwa tena amiri jeshi mkuu sina tatizo iwapo ni kwa ridhaa ya walio wengi, sio ile ya mabox ya kura kujazwa kura za ccm kwa uratibu wa jeshi la polisi.
 
..ook.

..kwa hiyo sasa Jpm na CCM wameungana na mabeberu.

..Je, nchi itakuwa salama kweli?

Wameungana kivipi labda? Sijakuelewa ujue!!! Ulitegemea JPM amfukuze yule balozi wa USA, zaidi ya kumchora?
 
Mi nasibir mwezi wa kumi na jamaa unavojua kutoa povu sijui kama patatosha mwaka huu ...
 
Bi Binafsi sijaona kama Kuna Jambo ameliongea linalotaka kuichafua nchi, aliyoyazungumza ndiyo yanayofanywa na waliopewa dhamana. Kwa hiyo anatoa tahadhari, atakayemuona Tundu Lissu anakosea ni yule ambaye ujumbe unaousikia unamgusa kwa namna moja au nyingine.
 
Hata uchaguzi wa S/M wakurugenzi walileta porojo hizo hizo , safari hii hatumwi mtoto dukani
Ni vigumu sana wafuasi wa CDM kukubali makosa.

Ikitokea siku Lissu kavamia bank na kupora, watakwambia tatizo ni bank wenyewe kwanini wakae na mihela, walinzi nao walikuwa wapi, kwanza hawana mafunzo ndio maana Lissu kaamua awape somo la bure.

Ndio hapa deep down mnajua anachofanya Lissu sio sahihi.
 
Sijasikia akisema atawafanyia nini watanzania. Lissu sio mtu sahihi kupambana na Magufuli. Magufuli alihitaji mtu kama lowassa wa 2015.

Hizi akili ndizo kikwazo cha Tanzania kutopiga hatua za maendeleo ya haraka....

Tanzania hii, itazidi kuogelea ktk dimbwi la UJINGA, MARADHI na UMASIKINI kama watu wote watakuwa na mawazo kama yako...

Usiwe na mawazo ya;

"..Tundu Lissu akufanyie nini wewe ama mama yako ama baba yako ama ndugu zako..."

Badala yake kuwa na mawazo/kuwaza hivi;

"...Mimi na wewe tutaifanyia nini nchi yetu nzuri kabisa aliyotupa Mungu wetu Baba Yehova....!!"

Na jambo jema kabisa na zuri unaloweza kulifanya kwa ajili ya Tanzania, nchi yako, ni hili...

Shiriki uchaguzi wa mwaka huu 2020 kwa kupiga kura kuuondoa utawala huu DHALIMU na MWOVU wa zaidi ya miaka 63 wa CCM....

Piga kura ya kumwondoa Magufuli na CCM yake madarakani. Piga kura yako kwa TUNDU A.M. LISSU...

Ukipiga kura yako kwa TUNDU A. M. LISSU maana yake unaruhusu mfumo mpya wa UTAWALA Tanzania wenye kujali UTU wa MTU, SHERIA na KATIBA. Utakuwa umepiga kura kwa ajili ya UHURU WAKO...

Hiki ndicho ambacho TUNDU A. M. LISSU anataka kuifanyia Tanzania na Watanzania...

Imeandikwa; "....utafuteni kwanza UFALME wa Mungu na HAKI yake, na hayo mengine yote mtapewa na kuzidishiwa...."

"Hayo mengine" yote ni haya;

å Maisha bora na ya heshima kwa kila Mtanzania...

å Kilimo bora....

å Elimu bora...

å Barabara bora

å Nishati ya umeme ya uhakika na rahisi...

å Utu na kuheshimiana kama binadamu...

å Maji safi na salama ya kutosha kwa kila mwananchi nk nk

## Haya hutayapata chini ya mfumo wa Utawala huu tulio nao. Na kama mnayapata, ni ktk viwango vya chini sana visivyoendana na umri wa Tanzania wa karibu miaka 70 sasa...!!
 
.
Ainisha kosa la Tundu Lissu hapo....

å Je, ni kutoa taarifa kwa umma kuwa anatishiwa kuuawa na "wasiojulikana" ndilo kosa lake?

å Je, ni kuripoti "tendo la kutishiwa kwake kuuawa" polisi ambacho ndicho chombo cha kisheria na kikatiba cha kupokea na kushughulika na maswala kama hili la usalama wa watu kama Tundu Lissu?

Au hujui kuwa polisi ndiyo wenye jukumu la kulinda usalama wa raia na Mali zao? Sasa wewe hoja yako iko wapi?

å Au kosa lake ni kuwakunbusha IGP - Simon Sirro na Mkurugenzi wa idara ya usalama wa taifa Diwani Athumani wajibu wao?

å Je, kosa lake ni kuwatahadharisha wagombea wa udiwani na ubunge wa chama chake kuwa makini na waangalifu wanapokwenda kuchukua fomu za uteuzi NEC na ikibidi wasindikizwe na wapenzi, wafuasi na wanachama wao kwa wingi?

MAKOSA ya Tundu Lissu yako wapi hapo at least kwa ulichokisikia katika hizi video mbili?

Basically, hakuna kosa. Tatizo linaweza kuwa ni wewe ktk ufahamu na uelewa wako...!!
 
Huyu mpumbavu ametumwa kuja kutuharibia nchi yetu
 
Atajayekuwa amesababisha ni yule aliyempiga risasi
 
Wakisha jaza watoe copy wabaki nazo ili ikitokea wakaambiwa wamejaza vibaya kuwepo na evidence
 
Ana amasisha uvunjifu wa sheria
 
Ndio sera zenu mwaka huu, nina risasi mguuni, mkono wa kushoto, nina risasi pajani. Hayo ndio anayohubiri tokea amefika, maana lisu bado mgonjwa anafanya nini jukwaani. Mnatafuta huruma ya wananchi, anataka tumuhurimie tumpe nchi.
Wapi niliposema kuwa hizo ndo sera?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…