Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 21,470
- 40,593
Ndiyo ukoje huo uroho wa madaraka?Uroho wa madaraka tu
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ndiyo ukoje huo uroho wa madaraka?Uroho wa madaraka tu
Unaumwa wewe usidhani kila mtu ana akili za kimasikini kama zako. Eti utawala unaamua watu waamke saa ngapi kwa akili hizi Tanzania ina safari ndefu sana.
Nakuuliza swali, huo utawala ndio unapiga kura? Chadema haiko compromised hivo huo utawala unaoupamba unavyokudanganya.
Huwezi kuongelea Chadema bila kumtaja mbowe yuko madarakani miaka 20 sasaMbowe msimuingize kwenye majadiliano yenu.
Hamuwezi kujenga hoja bila ya kumtaja Mbowe?
Misukule ya mzee mbowe kwisha habariMakamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) bara Tundu Lissu ametangaza nia ya kugombea uenyekiti wa CHADEMA Taifa, nafasi ambayo kwa sasa inashikiliwa na Freeman Mbowe.View attachment 3175126
Lissu ametoa rasmi tamko hilo, wakati akizungumza na wanahabari siku ya Alhamisi Desemba 12, 2024 Mlimani City mkoani Dar es Salaam.
"Ninaamini na ninapenda kuamini ninyi wanachama wenzangu nina sifa za kutosha za kugombea nafasi ya juu kabisa ya chama chetu (Chadema) yaani nafasi ya mwenyekiti wa chama Taifa."
“Kwa sasa Mimi ni Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara lakini pia nimewahi kuwa Rais wa TLS, Wakili, Mwanaharakati na Mtetezi wa Wananchi pamoja na nafasi nyingine, kwasababu zote hizi naamini Wanachama wenzangu mnaamini kuwa nina sifa ya kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Chama Taifa”
“Napenda kuwajulisha rasmi kwamba nimeshawasilisha taarifa rasmi kwa Katibu wa Chama chetu la kuondoa kusudio langu la kugombea nafasi ya Makamumi Mwenyekiti na badala yake mimewasilisha rasmi kusudia langu la kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Chama chetu” Tundu Lissu, Makamu Mwenyekiti wa Chadema-Bara
Mkuu, wewe utakuwa unaishi malawi na haujui siasa za TanzaniaKwani CCM ndio inapiga kura? Wapiga kura si ndio wataamua?
Bila Lissu chadema isingekuwepoLissu ni mropokaji tu anatakiwa kuongozwa na si kuongoza.sioni nafasi yake ya ushindi pale CHADEMA.
Lakini anayo haki ya kidemokrasia kugombea nafasi yoyote anayodhani anastahili.Lakini akumbuke kuna wapiga kura watakao amua asije na matokeo yake kichwani hapo atakuwa amefeli saana.
Bila DJ Kamanda Mbowe saa hizi Lissu angekuwa shimo la Tewa !
Safi sana, hii ndio kila kitukutafuta fedha na rasilimali kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli za chama
Mkuu mimi naongelea uchaguzi wa ndani ya CHADEMA siongelei uchaguzi wa viongozi wa serikali na mitaa. Unachanganya mambo.Pata muda wa kupitia malalamiko ya watu ambao wameshiriki uchaguzi
Pia pata muda wa kupitia hotuba ya mkuu wa wilaya ambae alitumbuliwa Kwa kusema mambo ambayo watawala walifanya kwenye uchaguzi
So yes Kura yako itakuwa na maana kama utawala watataka kura yako iwe na maana otherwise hata kama utashiriki kupiga kura itakuwa no tofaut na mtu ambae aliamua kulala nyumbani
Chama cha majizi watamfanyia figisu ili kisisajiliwe.Bora awe mwenyekiti wa chadema ili kuifufua upya.Mbowe kwa aina ya siasa yake ni ngumu chama kutoboa.Namshauri Lissu aanzishe chama chake...
Yes, huo Ndio ukweliKama ipo hivi basi imekaa vyema sana
Siyo kwenye kila hoja. Kwani pale Holland House mlikuwa mnajadili.Huwezi kuongelea Chadema bila kumtaja mbowe yuko madarakani miaka 20 sasa
Ok, kikubwa ana baraka za VIONGOZICha ajabu ni kuwa Mbowe hajatangaza kuwa ana nia ya kugombea nafasi ya Uenyekiti. Lakini kitendo cha Lissu kufanyia mkutano Mlimani kinanikumbusha Slaa na Serena. Mtihani uliopo mbele yake ni kuhakikisha kuwa anatimiza ndoto yake bila kukivuruga chama anachosema bado anakipenda. Wasiwasi wangu ni kuwa inaelekea kuwa ameanza kuamini kuwa yeye ndie Mkombozi wa CDM na hivyo itatumika kumtumia kukivuruga chama chake hata kama hilo sio kusudio lake. Inabidi atumie busara sana. Huu mwanzo wake haunipi matumaini makubwa.
Amandla...
Mkuu mimi naongelea uchaguzi wa ndani ya CHADEMA siongelei uchaguzi wa viongozi wa serikali na mitaa. Unachanganya mambo.
Upo sawa kama unaongelea uchaguzi mkuu na serikali za mitaa.
Kufanyia kwake mkutano Mlimani kunatia wasiwasi kwenye hilo.Ok, kikubwa ana baraka za VIONGOZI
Kila kituUnaweza kushindana nae kwenye sekta gani ya elimu yako?