Pre GE2025 Tundu Lissu: Nimewasilisha kusudio la kugombea nafasi ya Mwenyekiti CHADEMA

Pre GE2025 Tundu Lissu: Nimewasilisha kusudio la kugombea nafasi ya Mwenyekiti CHADEMA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA - Bara, Tundu Lissu ametangaza rasmi nia ya kugombea nafasi ya Uenyekiti wa CHADEMA Taifa ambayo kwa sasa inashikiliwa na Freeman Mbowe.

Akitangaza nia yake hiyo Jijini Dar es salaam leo December 12,2024, Lissu amesema ""Kwa sasa Mimi ni Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara lakini pia nimewahi kuwa Rais wa TLS, Wakili, Mwanaharakati na Mtetezi wa Wananchi pamoja na nafasi nyingine, kwasababu zote hizi naamini Wanachama wenzangu mnaamini kuwa nina sifa ya kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Chama Taifa"

"Napenda kuwajulisha rasmi kwamba nimeshawasilisha taarifa rasmi kwa Katibu wa Chama chetu la kuondoa kusudio langu la kugombea nafasi ya Makamumi Mwenyekiti na badala yake mimewasilisha rasmi kusudia langu la kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Chama chetu" Lissu.
 
Watu wenye misimamo mikali huwa hawafai kushika nafasi za juu kabisa (mwisho) katika uongozi. Wanafaa kuwa na nafasi ambayo anaweza dhibitiwa na aliye juu yake.
Wakuu,

Siku ya leo Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu atakuwa ananguruma wakati anazungumza na vyombo vya habari

Fuatilia uzi huu kujua nini kinaendelea kwenye mkutano huo.

  • Katika mkutano huo uliofanyika Mlimani City, Tundu Lissu amedokeza kuwa anagombea nafasi ya Uenyekiti wa CHADEMA ambayo kwa sasa inashikiliwa na Freeman Mobwe

  • Lissu amesema kuwa tayari ameshawasilisha maombi yake ya kugombea nafasi ya Uenyekiti kwa viongozi wa juu wa CHADEMA

Akiongea na Waandishi wa Habari, Makamu wa Rais wa CHADEMA Bara, Tundu Lissu, amesema anaaamini na Wanachama wengine wanaamini kuwa ana sifa zote za Kugombea nafasi ya juu kabisa ya Uongozi wa Chama hicho kwa ngazi ya Taifa, kama zilivyoanishwa katika Katiba ya Chama.

Lissu amesema amewasilisha taarifa rasmi kwa Katibu Mkuu wa CHADEMA ya kuondoa kusudio lake la kugombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti (Tanganyika) na badala yake amewasilisha kusudio la Kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Chama taifa katika Uchaguzi Mkuu wa Chama ujao.

i
 
Mbowe akileta za sumu haionjwi tu!
Ameshapata sababu za kuhamia utopoloni.
 
Lissu ana vision tungekuwa na raia makini alitakiwa kuwa Rais
Hapana mkuu. Huyu labda awe waziri mkuu. Watu wenye hulka yake hawafai kuwa wa mwisho katika maamuzi. Watu kama hawa wanafaa kuwa kama sokoine, anakuwa waziri mkuu halafu raisi anasapoti afanyayo ila inapotokea jambo lisilohitaji hulka ya watu aina yake basi anakuwepo wa kummpunguza mwendo.
 
1000017181.jpg
 
Utawala ndio unaamua hata ww uamke saa ngapi au ununue bidhaa flan Kwa sh ngapi

So huo huo utawala hauwezi kuruhusu lisu awe mwenyekiti because Kwa tabia la lissu then vurugu zitakuwa kila siku, maandamano yatakuwa kila siku
Unaumwa wewe usidhani kila mtu ana akili za kimasikini kama zako. Eti utawala unaamua watu waamke saa ngapi kwa akili hizi Tanzania ina safari ndefu sana.

Nakuuliza swali, huo utawala ndio unapiga kura? Chadema haiko compromised hivo huo utawala unaoupamba unavyokudanganya.
 
Back
Top Bottom