Pre GE2025 Tundu Lissu: Nimewasilisha kusudio la kugombea nafasi ya Mwenyekiti CHADEMA

Pre GE2025 Tundu Lissu: Nimewasilisha kusudio la kugombea nafasi ya Mwenyekiti CHADEMA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Tunahitaji serious internal reforms kwenye upinzani kabla hujafikiri kupambana na CCM. Kwasasa upinzani umegeuka mchongo wa siasa za kitapeli. Mimi nitasimama na wale walio serious kuindoa CCM madarakani.
 
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) bara Tundu Lissu ametangaza nia ya kugombea uenyekiti wa CHADEMA Taifa, nafasi ambayo kwa sasa inashikiliwa na Freeman Mbowe.

Lissu ametoa rasmi tamko hilo, wakati akizungumza na wanahabari siku ya Alhamisi Desemba 12, 2024 Mlimani City mkoani Dar es Salaam.

"Ninaamini na ninapenda kuamini ninyi wanachama wenzangu nina sifa za kutosha za kugombea nafasi ya juu kabisa ya chama chetu (Chadema) yaani nafasi ya mwenyekiti wa chama Taifa."

“Kwa sasa Mimi ni Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara lakini pia nimewahi kuwa Rais wa TLS, Wakili, Mwanaharakati na Mtetezi wa Wananchi pamoja na nafasi nyingine, kwasababu zote hizi naamini Wanachama wenzangu mnaamini kuwa nina sifa ya kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Chama Taifa”

“Napenda kuwajulisha rasmi kwamba nimeshawasilisha taarifa rasmi kwa Katibu wa Chama chetu la kuondoa kusudio langu la kugombea nafasi ya Makamumi Mwenyekiti na badala yake mimewasilisha rasmi kusudia langu la kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Chama chetu”
Tundu Lissu, Makamu Mwenyekiti wa Chadema-Bara​
Gelm_0SXkAA-iSg.jpeg
 
Tunahitaji serious internal reforms kwenye upinzani kabla hujafikiri kupambana na CCM. Kwasasa upinzani umegeuka mchongo wa siasa za kitapeli. Mimi nitasimama na wale walio serious kuindoa CCM madarakani.
Natangaza rasmi kumuunga mkono Tundu Lissu maana hakuna anachoogopa kwa sasa! Siasa za CCM ya leo siyo za kuchekeana tena
 
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
@ChademaTz
Bara Tundu Lissu
@TunduALissu
ametangaza nia ya kugombea uenyekiti wa CHADEMA Taifa, nafasi ambayo kwa sasa inashikiliwa na Freeman Mbowe
@freemanmbowetz
.Lissu ametoa rasmi tamko hilo, wakati akizungumza na wanahabari siku ya Alhamisi Desemba 12, 2024 Mlimani City mkoani Dar es Salaam.

Sasa ndio kifo cha chadema kinakuja

Because, utawala hauwezi kukubali lissu awe mwenyekiti

Na lisu akikosa hiyo nafasi lazima ataondoka chadema kwenda kuanzisha Chama kingine au ataenda Kwa Zitto
 
Back
Top Bottom