Tundu Lissu: Ninampinga Magufuli hadharani. Sio mnafiki na sijahongwa

Tundu Lissu: Ninampinga Magufuli hadharani. Sio mnafiki na sijahongwa

Kila kamati inayo mapendekezo yake. Kamati ya pili itatoa muongozo na ushauri wa kisheria na ndio sababu ya kuundwa kwake.
Wewe na Lisu wako ni wapuuzi na ni wa kupuuzwa tu.
Kuyazuia makontena si ni adhabu hiyo?
Ikitokea kamati ikashauri ifuatwe njia ya kisheria huioni stepu tuliyobugi?
 
Tundu Lisu kaenda Shuleni kujifunza kiingereza na kuongezea muda aliokaa Uingereza kajua kiingereza basi, lkn Kichwani ni Zero, jamaa ni mtupu hadi huruma, eti kapigania hii nchi ana akili ndogo kama Nape, wewe Tundu lisu upiganie hii Nchi?? Hata kwenu Singida kwenyewe hawakutaki unapita kwa shida halafu unasema umeipigania hii nchi? Labda umempigania Fisadi Mwenzako lowasa!

Comment yako inanikumbusha kwamba ujinga ni mzigo
 
Kwa hiyo mikataba ya madini inaruhusu kudanganya kilichopo??
Tumbo hunyonya damu ya ubongo!!

Ndio hapo sasa

Hawa wanaumia wanataka Raisi aache anayofanya, ni walafi wakubwa.

Wanataka kuvuta wale wapenda kufata mikumbo, huku wao matumbo yao mbele kwanza.
 
Lissu tangu lini ulikuwa mzalendo! Uzalendo wa kutetea fisadi lowasa, au uchumia tumbo upi anausema zaidi ya huu wa kupewa kitu kidogo kumsafisha mtu aliye mchafua kwa miaka 10. Lissuu wadanganye vipofu wa vabichaa
Amepambana na mambo ya migodi kwa mrefu tu akisema maonevu yanayofanywa na wawekezaji mlimuelewa?zaidi ya kusema na wapigwe tu?yaani nyinyi sjui ni majitu gani msokuwa na haya leo polepole anaulizwa maswali anashindwa kujibu na kuanza kukwepa kama fisi maji.
 
Lissu is a classic example of a loose cannon. Watu kama Lissu ni wazuri sana kuongea lakini ukimkabidhi zizi mifugo yote itakufa kwa funza. He will do nothing apart from lecturing the planet earth. No wonder baada ya miaka 8 alikuwa matapishi, shamelessly.
We Una mchango gani? We mzuri kwenye kipi?
 
Mkuu nakuheshimu sana. Lakini kwa nini hatulielewi hili sakata la mchanga?

Tatizo sio mkataba.

Tatizo ni kuwa wanadanganya kuwa mchanga una dhahabu kilo X kumbe ukweli una kilo 10X. Hiki ndicho anachoshupalia Raisi Magufuli.

Kwa nini hatumuelewi?

Au ndio upinzani wenyewe huo?

Ninashindwa kuelewa kiini cha huu mjadala.

Maybe I am dumb.
Kama unadai kuibiwa mchanga unaweza kutueleza huo mchanga uliuchimba lini wapi na kwa namna ipi!!?
UKOME KUYAPAKAZIA UZEMBE MAJESHI YETU YA ULINZI NA USALAMA WA MIPAKA, MAISHA NA MALI ZETU WATANZANIA.
 
“The industry can be its own worst enemy when it sits down and agrees these terms, it’s gonna come back and bite us. And in this case it has,” Gordon says. Those early arrangements, while perfectly legal, “were not equitable”, he adds. To head off the bad feeling, Acacia began paying corporate tax last year. “In total we paid $162m in taxes and other payments to the Tanzanian government in 2016 so we are one of the largest taxpayers in the country.”
 
...You have our back up.
Your back up?

...get one's back up, to become annoyed; take offense.

We got your back:- An expression assuring someone that you are watching out for them. Comes from making sure you are safe by watching what's behind you when you're busy looking ahead. (Urban Dictionary)
 
Mkuu nakuheshimu sana. Lakini kwa nini hatulielewi hili sakata la mchanga?

Tatizo sio mkataba.

Tatizo ni kuwa wanadanganya kuwa mchanga una dhahabu kilo X kumbe ukweli una kilo 10X. Hiki ndicho anachoshupalia Raisi Magufuli.

Kwa nini hatumuelewi?

Au ndio upinzani wenyewe huo?

Ninashindwa kuelewa kiini cha huu mjadala.

Maybe I am dumb.
Na kama kuna kitu huwa tunapata kutokana na kilo x basi ni kidogo na sio haki yetu.

Kama kilo x tunapata sh 100 basi ilitupaswa tupate sh 1000 kutokana na kilo 10x.
 
18622446_1126398777465538_2060351389369899505_n.jpg



Na mimi ni Mtanzania pia.

Tofauti kati yangu mimi na wewe na Magufuli ni hii: Mimi nimepigania nchi yangu katika masuala haya tangu mwaka '99.

Wakati huo tulikuwa na mgodi mmoja tu wa dhahabu, Resolute Golden Pride Nzega. Bulyanhulu ilikuwa haijajengwa. Geita ndio kwanza walikuwa wanafukuza wanakijiji wa Mtakuja.

Nadhani nilikuwa wa kwanza katika nchi hii kupiga yowe kwamba tutaibiwa sana kwenye sekta ya madini.

Wewe sijui ulikuwa wapi wakati huo. Najua Magufuli alikuwa wapi: upande wa MaCCM na wawekezaji hawa.

Nimepigana na wawekezaji hawa mahakamani, kwenye medani ya kisiasa ndani na nje ya nchi hii kwa zaidi ya miaka 15. Nimetetea wananchi completely free of charge Bulyanhulu, Tarime, Nzega, Geita, n.k.

Sijui wewe ulikuwa wapi lakini najua Magufuli alikuwa upande wa nani: wa MaCCM na wanyonyaji hawa.

Soma Rai ya tarehe 17 Julai, 2001, uone tulimwambia nini Mkapa siku anaenda kuzindua Mgodi wa Bulyanhulu.

Sijui ulikuwa wapi lakini najua Magufuli alikuwa wapi: alikuwa anatetea tumbo lake na matumbo ya wanyonyaji hawa.

Nilikamatwa na kushtakiwa kwa uchochezi kwa sababu ya Bulyanhulu. Hiyo ilikuwa December 2002. Nilikaa na kesi hiyo mahakamani Kisutu kwa miaka sita.

Sijui ulikuwa wapi ila najua Magufuli alikuwa wapi: upande wa watesi wa wananchi na wanyonyaji wa rasilmali zetu.

Leo Magufuli anajifanya mzalendo na anahoji uzalendo we yeyote anayepingana nae.

Ni muongo. Anatafuta umaarufu wa kisiasa kwa wasiojua na wasiokumbuka. Ataupata. Kwa siku chache tu. Mark my words: ataumbuka na mtaumbuka.

Mimi ninampinga hadharani. Sio mnafiki, na sijahongwa. Ninampinga kwa sababu atatusababishia matatizo makubwa zaidi kuliko tuliyonayo sasa.

Huo mchanga atauachia upelekwe ambako umepelekwa kwa miaka 16 iliyopita. Kama sheria ndiyo hiyo na mikataba ndiyo hiyo hana pakwenda.

Tatizo ninaloliona ni kwamba by the time anawarudishia mchanga wao, Tanzania itakuwa imekuwa a basket case kama Zimbabwe.

Na tutakuwa tumelipishwa mapesa mengi kama fidia na arbitral tribunals za kimataifa kwa kuvunja mikataba na wawekezaji hawa.

Kama kuna anayefikiri uzalendo ni kufumbia macho masuala haya basi huyo na amuunge mkono Magufuli kwenye upofu wake wa kujitakia.

Ripoti ya Prof. Mruma haitamaliza hata nusu saa under serious scrutiny. Zaidi ya majina ya maprofesa walioiandaa, ripoti hii haina credibility yoyote. Ni kazi ya kisiasa iliyopakwa rangi ya usomi.

Kama umefuatilia taarifa za kitaalamu za Bulyanhulu hata kabla ya Barrick Gold kuingia mwaka '99 utajua ninasema nini.

Sutton Resources, Outukumpu Oy na hata STAMICO walishafanya utafiti mkubwa juu ya utajiri wa Bulyanhulu. Taarifa zipo na zimekuwepo kwa hata mbumbumbu wa jiolojia ya madini kama mimi.

Hiki alichoambiwa Magufuli ni rubbish, hata kama ni ya kiprofesa. Rubbish. Hatuibiwi kwenye mchanga, that's the rubbish fed on the unlettered.

Tunaibiwa kwenye sheria. Kama hamuoni hilo then God have mercy on us.
Taarifa iliyopekelewa na mh Rais ilikuwa ni ya kamati ya uchunguzi ambayo ilikuwa na hadidu rejea.. ambazo zilihitaji majibu. Na bila shaka majibu yaliypatikana ni hayo.
sasa mlitaka wasiyachunguze hayo makontena? Na wasingeyachunguza hizo taarifa za kilichomo na uwezo wa scanner zetu pale bandarini je yangejulikanaje?
Kwa mujibu wa ripoti baada ya uchinguzi...
je ndani ya mchanga kuna madini?
Kama yapo ni ya aina gani?
Kwa kiwango gani?
je taratibu zinazohusika na madini kwa nchi yetu zinafuatwa? Ni kwa kiwango gani?
uwezo wetu kupima kilichopo katika makontaina hayo ni wa uhakika?
Kama ndio je ni kwa kiwango gani?

Waliohusika na upimaji huo wana elimu katika masuala hayo? Kama ndio elimu na uelewa wao ni wa kiwango gani?
je taarifa ilikuwa inamhusu nani ? Kama ni yetu Watanzania enyi wanasiasa "wabwatukaji" mlitaka tuipokee kwa mtindo upi?
enyi mbweha mlio wanafaki mabwingwa wa kuhadaaa na kurubuni akili za watu kwa maswali hayo sioni shaka kwa kiwango kidogo cha elimu nilicho jaaliwa kukipata.
 
Kila kamati inayo mapendekezo yake. Kamati ya pili itatoa muongozo na ushauri wa kisheria na ndio sababu ya kuundwa kwake.
Wewe na Lisu wako ni wapuuzi na ni wa kupuuzwa tu.

Ooh, kumbe ile ya 2, 3 ,4 hadi ya 100 itakuja na pendekezo la kumrudisha ktk nafasi yake Prof. Muhongo, siyo ?

Itakuja na lipi jipya hasa ambalo ni tofauti na hii ya kisiasa ya Prof. Mruma iliyopakwa rangi ya "uprofesa " kumfurahisha Farao Uchwara ?

Aisee, nyie maCCM ni wendawazimu wa kiwango cha kuzimu hakya nani vile....!!
 
Tundu Lisu kaenda Shuleni kujifunza kiingereza na kuongezea muda aliokaa Uingereza kajua kiingereza basi, lkn Kichwani ni Zero, jamaa ni mtupu hadi huruma, eti kapigania hii nchi ana akili ndogo kama Nape, wewe Tundu lisu upiganie hii Nchi?? Hata kwenu Singida kwenyewe hawakutaki unapita kwa shida halafu unasema umeipigania hii nchi? Labda umempigania Fisadi Mwenzako lowasa!
Kwahiyo huu ndio mchango wako kuhusu makanikia.
 
Maskini siasa uchwara za watanzania hazitatusaidia kusonga mbele.Ingekuwa Marekani mtu kama Tundu Lissu kwa uzoefu wake katika sheria za kitaifa na kimataifa hususani uzoefu alionao kuhusu sakata la mikataba ya wawekezaji wa madini ushauri wake ungezigatiwa na angejumuishwa ktk jopo la wataalam wa kututoa katika janga hili la wizi na utapeli.

Lakini kinyume chake kwa ushabiki wa kijinga tunamuona kuwa anawatetea wawekezaji wa madini.Huyu Lissu ni kichwa adimu sana na ana akili nyingi sana ktk mambo ya sheria na pia uzalendo wake unaonekana wazi wala si wa kutilia shaka

Pia Lissu ana maono ndio maana kils anachotabiri hutokea,mfano katika makala hayo inaonekana kinachotokea sasa kuhusu sakata la mchanga alishakieleza na kukitabiri miaks mingi. Pia kuhusu utawala huu alitabiri mambo mengi ambayo yametokea mfano,uvamizi wa clouz media,kutishiwa bastora kwa Nape na kutekwa na kuuawa kwa raia nk
Hivyo serikali ikubali ushauri wake wa kisheria tusiupuuze kisa uchadema wake ili hali uwezo wake kisheria unaeleweka kitaifa na kimataifa.Kwa wasiokumbuka huyu Lissu ndie aliyemtetea rais Zuma kwenye sakata lake kama raisi wa Afrika kusini na akamwokoa kisheria za Afrika kusini akaonekana hana hatia na mpaka leo ni raisi.
 
Unajuwa ukishakuwa ccm hata akili uwazinapetea unafanana chizi hili liccm lillilochangia hapa halinahoja naistoshe hayamajamaa kaziyao huayanasubilia viongoziwao wakijampa menyewe yanapiga makofi navigelegele siatabungeni tunawaona sasa kamawabungewao kaziuao nikupiga makofi jeleo humfwasi wao atafanya nn ndiyomaana anapingana na ukweli wa lisu
 
Naona Lisu ana ushawishi mkubwa sana ila nasikitika sana kwa nini hakujumuishwa kwenye kamati mojawapo bnafsi ningeelewa zaidi ya nijuavyo manake nakosa wa kumuamini,Lisu aunganishwe tu kubishana wenyewe kwa wenyewe kunazidi kuwapa nguvu ACACIA in case kama ni lweli wanaiba,tujiridhishe tu kwa namna yoyote hamna namna

Kuibiwa, tunaibiwa sana.... hakuna anayebisha !!

Kinacholeta shida na kutuudhi sisi wengine ni kuwa, hata hawa CCM ambao ndiyo waliosaini kuibiwa kwetu, wanajifanya kulia pamoja na sisi wakati wanapaswa wote kuwa wako jela akiwemo Magufuli mwenyewe !!!

Wangekuwa waungwana hawa, kuanzia Magufuli mwenyewe, hadi huku chini wangepaswa kuachia ngazi ktk kuongoza jahazi la taifa hili......!!
 
huyu ni chizi tuu aseme kama mikataba iliyo sainiwa ina halalisha kudanganya kiasi cha madini kilichomo ndani ya mchanga....
Tahira huyu

Aliyesaini hiyo mikataba ni nani? Kwa maelekezo ya nani? Chini ya serikali ya chama gani? Iliyopitishwa na wabunge wengi wa chama gani?
 
Back
Top Bottom