Tundu Lissu: Ninampinga Magufuli hadharani. Sio mnafiki na sijahongwa

Tundu Lissu: Ninampinga Magufuli hadharani. Sio mnafiki na sijahongwa

ccm ndo walivyo, hata wanaloshangilia leo hawalijui. Magufuli kwa sasa ndo kipaumbele chao hivyo hata akiamuru lunch iliwe uani wao watashangilia tu. Na wengine watasema kuna harufu nzuri.
HAHAHAAAAAAA! noma sana
 
Raisi wetu naomba ututajie majna yale ulisema unayo, tujue nani ni nani.

Pia tunasubiri ripoti zingine kwa hamu kubwa.

Hongera Raisi wetu, nazidi kufurahia kuwa upande wako.
Hv ww bado upo tu, hujateuliwa kiwa mkuu wa wilaya bado??? Kama ndugu yako chabruma.......
 
Unasubiri mafisadi kuisha CCM mkuu? Unapoteza muda wako. Jiulize tangu magufuli aingie madarakani amewafukuza wangapi na bado anaendelea kila siku.lakini hawaishi. Jaribu kushangaa
Wataishaje wakati wengine wanakimbilia kambi ya pili
 
Leo mmekosa point kabisaaaa ndugu zangu......
Ebu tafuta historia ya lissu harakati zake za mwanzoni alizifanya wapi kama siyo migodini
Samahani sana kama nitakua nakuudhi,nna stress sana mkuu ki ukweli ila kuniambia nifatilie harakati za Lisu huko zamani sio poa man,ebu fatilia wewe tu,kuwa mgodini unaweza ukawa mlinzi getini so sio issue saaana cha msingi rahisisha kazi,sema alikua nani akasikia au akapima hivyo ndo vitu nataka kusikia,sina nnapo egemea kwa hiyo naomba ukijibu unijibu kama mtanzania asiye na chama kirahisi tu kwa sababu tunatofautiana IQ so tusisumbuane na homework, sorry
 
Huyu mmmmmmmmmh

In short anazidi kuboaaaaaaaaaaa kutafuta kiki tu na wivu.com umemjaa

Alipoona hayo yote kwanini hakwenda Ikulu kupigania anayodai, akakaa getini akaweka na kambi hadi aone mabadiliko kuwa amesikilizwa.

Maneno yake yamejaa uchungu anajua wengi wamependa alichofanya Raisi, na anajua mengi yanakuja.

Mdaku kweli huyu na hana heshima kwa jitihada za Mh. Magufuli akwende hukoooooooooo

Wanaojielewa hatudanganyiki

Hasira za kukosa mkato wa kutopokea vibahasha

Lolote na liwe, JPM anajua analofanya.

Hapa kazi tu

Magufuli 2020

Magufulie oyeeeeeeeeee
Lolote na liwe, JPM anajua analofanya.

we hujui?
 
Jamani eee!!! aliyeianzisha hii vita ni Mh Magufuli na kajipangia namna ya kuipigana. Kaunda kamati mbili za kumshauri. Kamti ya kwanza imetoa majibu na maoni bado ya pili.
Kutletea maoni ya huyu mwehu humu ni kutuchosha sana. Maprofesa na madokta washeria na uchumi wamo kwenye kamati ya pili watamshauri kisheria limekaaje. Chochote watakacho shauri ndicho kitakachofanyika. Lisu na wapuuzi wengine wasimsafishe mtoto bado anajisaidia waache kihelehele.
Kamati za kumshauri anachotaka!!!!!
Utachekea chooni uchekwe
 
TAARIFA ILIYOTHIBITISHWA INAONYESHA KWAMBA , MH TUNDU LISSU NDIYE MWANASHERIA BORA KABISA KUWAHI KUWEPO KWENYE ENEO LA MAZIWA MAKUU , TANGU KUUMBWA KWA MBINGU NA ARDHI .
 
Sasa kwa taarifa yako wewe mpuuzi kuna kipengele kwenye mkataba kinachosema kuwa kinachochimbwa chote ni mali ya mwekezaji na sisi tutaambulia mrabaha ambao kila mwisho wa mwaka mnapeleka wakaguzi. Pia kumbuka kuwa kule ndani ya migodi mna maagent kibao mlioweka huko.

Ule mkataba aliosaini mkuu wako wa miaka 100 ndiyo chanzo cha tatizo.
Mkuu nakuheshimu sana. Lakini kwa nini hatulielewi hili sakata la mchanga?

Tatizo sio mkataba.

Tatizo ni kuwa wanadanganya kuwa mchanga una dhahabu kilo X kumbe ukweli una kilo 10X. Hiki ndicho anachoshupalia Raisi Magufuli.

Kwa nini hatumuelewi?

Au ndio upinzani wenyewe huo?

Ninashindwa kuelewa kiini cha huu mjadala.

Maybe I am dumb.
 
18622446_1126398777465538_2060351389369899505_n.jpg



Na mimi ni Mtanzania pia.

Tofauti kati yangu mimi na wewe na Magufuli ni hii: Mimi nimepigania nchi yangu katika masuala haya tangu mwaka '99.

Wakati huo tulikuwa na mgodi mmoja tu wa dhahabu, Resolute Golden Pride Nzega. Bulyanhulu ilikuwa haijajengwa. Geita ndio kwanza walikuwa wanafukuza wanakijiji wa Mtakuja.

Nadhani nilikuwa wa kwanza katika nchi hii kupiga yowe kwamba tutaibiwa sana kwenye sekta ya madini.

Wewe sijui ulikuwa wapi wakati huo. Najua Magufuli alikuwa wapi: upande wa MaCCM na wawekezaji hawa.

Nimepigana na wawekezaji hawa mahakamani, kwenye medani ya kisiasa ndani na nje ya nchi hii kwa zaidi ya miaka 15. Nimetetea wananchi completely free of charge Bulyanhulu, Tarime, Nzega, Geita, n.k.

Sijui wewe ulikuwa wapi lakini najua Magufuli alikuwa upande wa nani: wa MaCCM na wanyonyaji hawa.

Soma Rai ya tarehe 17 Julai, 2001, uone tulimwambia nini Mkapa siku anaenda kuzindua Mgodi wa Bulyanhulu.

Sijui ulikuwa wapi lakini najua Magufuli alikuwa wapi: alikuwa anatetea tumbo lake na matumbo ya wanyonyaji hawa.

Nilikamatwa na kushtakiwa kwa uchochezi kwa sababu ya Bulyanhulu. Hiyo ilikuwa December 2002. Nilikaa na kesi hiyo mahakamani Kisutu kwa miaka sita.

Sijui ulikuwa wapi ila najua Magufuli alikuwa wapi: upande wa watesi wa wananchi na wanyonyaji wa rasilmali zetu.

Leo Magufuli anajifanya mzalendo na anahoji uzalendo we yeyote anayepingana nae.

Ni muongo. Anatafuta umaarufu wa kisiasa kwa wasiojua na wasiokumbuka. Ataupata. Kwa siku chache tu. Mark my words: ataumbuka na mtaumbuka.

Mimi ninampinga hadharani. Sio mnafiki, na sijahongwa. Ninampinga kwa sababu atatusababishia matatizo makubwa zaidi kuliko tuliyonayo sasa.

Huo mchanga atauachia upelekwe ambako umepelekwa kwa miaka 16 iliyopita. Kama sheria ndiyo hiyo na mikataba ndiyo hiyo hana pakwenda.

Tatizo ninaloliona ni kwamba by the time anawarudishia mchanga wao, Tanzania itakuwa imekuwa a basket case kama Zimbabwe.

Na tutakuwa tumelipishwa mapesa mengi kama fidia na arbitral tribunals za kimataifa kwa kuvunja mikataba na wawekezaji hawa.

Kama kuna anayefikiri uzalendo ni kufumbia macho masuala haya basi huyo na amuunge mkono Magufuli kwenye upofu wake wa kujitakia.

Ripoti ya Prof. Mruma haitamaliza hata nusu saa under serious scrutiny. Zaidi ya majina ya maprofesa walioiandaa, ripoti hii haina credibility yoyote. Ni kazi ya kisiasa iliyopakwa rangi ya usomi.

Kama umefuatilia taarifa za kitaalamu za Bulyanhulu hata kabla ya Barrick Gold kuingia mwaka '99 utajua ninasema nini.

Sutton Resources, Outukumpu Oy na hata STAMICO walishafanya utafiti mkubwa juu ya utajiri wa Bulyanhulu. Taarifa zipo na zimekuwepo kwa hata mbumbumbu wa jiolojia ya madini kama mimi.

Hiki alichoambiwa Magufuli ni rubbish, hata kama ni ya kiprofesa. Rubbish. Hatuibiwi kwenye mchanga, that's the rubbish fed on the unlettered.

Tunaibiwa kwenye sheria. Kama hamuoni hilo then God have mercy on us.
Watu kama tundulissu wako wengi; huu kwao ni mradi. On one hand anawskstisha tamaa wenye kuonewa kwa kutumia Kiingereza kigumu na legal subterfuge. Hapa anawinda kwamba just in the remote Acacia washinde ajipatie sifa kisiasa kwamba I told you so. Kama wakishindwa - na watashindwa, mkataba si mkataba kama ukiweza kuonyesha fraud - atakaa kimya, hakuna atakayemkumbuka, atabaki anadharauliwa kama zamani. He has thetefore nothing to lose. Lakini kibaya zaidi ni kuwa anawasaidia maadui wetu kujenga hoja ya utetezi akitegemea watamlipa. Si lazima aende mahakamani kuwatetea, kitakachotokea watamlipa kimya kimya awapatie Legal Opinion; hatuna namna ya kujua kama katoa kegal opinion na kulipwa au la, lakini tayari ananyemelea apewe kazi ya legal opinion, au Lawyer wao atamfuata privately atoe legal opinion. Hiyo argument ya kusema mikataba minovu ni ya kitoto. Shida si ubovu wa mkataba (kwa sababu mkataba umesema mawe yakaguliwe na kupimwa na watu wetu wa TRA na wa madini na mapolisi. Hawa wasipokuwa na uzalendo wakaachia tani 5 zipite bila kuhesabiwa, ina maana ni sawa na watu wanazini ingawa Amri ya 6 ya Mungu mwenyewe imekataa kuzini. Lissu anapalilia tumbo lake.
 
Hv ww bado upo tu, hujateuliwa kiwa mkuu wa wilaya bado??? Kama ndugu yako chabruma.......

Oooh

Hanifahamu na mimi ni mwananchi tu kama wewe, na mdau wa JF.

Kwa hiyo tulia mimi na nyie humu humu.
 
Kamati za kumshauri anachotaka!!!!!
Utachekea chooni uchekwe
Kama ndio utakuwa ushauri atafanya hivyo. Hata kama watamshauri kuomba radhi atafanya. Wakimshauri awapunguzie bei atafanya.
 
Mkuu nakuheshimu sana. Lakini kwa nini hatulielewi hili sakata la mchanga?

Tatizo sio mkataba.

Tatizo ni kuwa wanadanganya kuwa mchanga una dhahabu kilo X kumbe ukweli una kilo 10X. Hiki ndicho anachoshupalia Raisi Magufuli.

Kwa nini hatumuelewi?

Au ndio upinzani wenyewe huo?

Ninashindwa kuelewa kiini cha huu mjadala.

Maybe I am dumb.
Na kweli wewe ni Dumb wala hujakosea..Magufuli wakati kipindi hicho anasema Ndiyo mswaada wa madini upite alikuwa hajui faida na madhara yake? Au alikuwa anaunga mkono ilimradi tu bora liende?
 
Hilo lipo wazi kwa wafuatiliaji......nakumbuka jamaa alivyokuwa anapewa ulinzi na wananchi badala ya polisi wakati anapambana na hawa wazungu..........Zitto Kabwe alitimuliwa Bungeni kisa ishu ya madini......wakati haya yanatendeka ni kweli wanaofoka Leo walikuwa bungeni wakishabikia kumsulubu Zitto.
Yaani we acha tu ndugu yangu
 
Nchi hii inavituko sana Magufuri amekua mbuge zaidi za miaka kumi amekua waziri miaka kumi Chama chake ndo kilichoingia mikataba ya kuihujumu Nchi tena swahiba wake Mkapa sasa heti leo nishujaa kuseamea mchanga CCM wanatengeza matatizo tena wanajifanya kuyatatua wajinga wanashangalia
 
Back
Top Bottom