Tundu Lissu: Ninampinga Magufuli hadharani. Sio mnafiki na sijahongwa


Mkuu Big up
 
Rais piga kazi achana na wanao bwabwaja kwenye mitandao.
 
Mbona povu jingi linamtoka, asubiri wanasheria wenzake waje na hii tathmini. Kuwatukana wenzako kwenye hili ni kutafuta kiki tu. Ni sawa tumejikwaa hata kama wakati huo mheshimiwa Rais alikuwa upande huo asingeweza kukurupuka tu lazima Lisu ajue hilo, sasa hivi yeye ndio dereva hivyo keshaanza tumsupport.
 
Ukiangalia hata yeye Tundu Lisu anataka sifa na hulka kujiona yeye anajua kila kitu itamgharmu muda si mrefu.
 
Sisi wana singida kwa ujumla tunampongeza kijana wetu huyu ambaye anaipigania nchi yetu kila uchao,ewe mtanzania mwenzetu mzalendo popote ulipo jitahidi kumuombea huyu kijana TUNDU LISSU kwa mwenyezi mungu amuongezee ulinzi ili aendelee kutupigania na kutufumbua macho.
 
Ngoja nisogeze kigoda na popukoni nione hili li series linaendaje.
 
Kwani umeisoma vizuri andiko lililotolewa humu au unakurupuka tu,,maana kina sizonje mpo wengi. Labda nikueleweshe tu kauli na maana ya anachokiongea Tundu Lissu,, yy hajasema wala kukataa kuibiwa mchanga wenye madini,maana kwa miaka mingi wamekuwa wakiongea kuhusu uwizi huo na mkuu wa kaya na maficm wenzake wamekuwa wakitetea kwa kuipitisha tena kwa vifijo na nderemo na huyuhuyu mkuu akiwa mmoja wao hatujawahi kumsikia hata mara moja akihoji zaidi ya kusuport kila miswada ya madini ambayo ni mibovu ikiletwa bungeni wakati huo,na ni hawahawa wakina Tundu walikuwa wakiwaasa kuwa kuna uwizi mkubwa unafanyika,,. Sasa alichokiongea Tundu Lissu ni kuwa hapo tunachoibiwa sisi ni mikataba mibovu tuliyoingia na ndio maana akasema siku ya mwisho tutawarudishia aidha mchanga wao huo tunaojibatiza kuwa ni wetu na tunaibiwa au tukitumia mabavu kuuchukua na kuvunja nao mikataba tuliyoingia chaka wenyewe na kuipitisha kwa kuibariki kwa zimwi la kiitikadi na kuacha uzalendo eti sababu upo chini ya himaya yetu basi itabidi tuwalipe hela nyingi ambayo tutajuta kwa kutafuta sifa ya kisiasa ya mda mfupi,. Yaani maana yake badala ya kuangalia tulipojikwaa tunaangalia tulipoangukia,,au hamkumbuki ngano mbovu ya bakressa,,?? Kilichotokea kwa kumpa utajiri wa bure kama fidia iliyopelekea hadi leo ni mmoja kati ya matajiri wakubwa Afrika na yote ni nn,,!!? Sifa za kijinga
 


Labda Mungu wa chadema, Mange Kimambi!
 
AMINA na kila mtanzania atamuombea ili huyo kiongozi wetu azidi kutupigania
 
Kama ni kweli Lisu mkweli, angepingana na chama chake ujio wa Lowasa CHADEMA kwa sababu ni yeye aliyekuja na list of shame. Sasa swali kwake ni kitu gani kilichomfanya amkubali Lowasa wakati kwa miaka nane anamwimba kuwa fisadi. Hii inadhihirisha kuwa watanzania ni vigeugeu, Lisu anajua kwa nini alimkubali Lowasa kwa sababu pesa yake tu na si vinginevyo na nina imani hata leo Rais akimteua kwa mwanasheria Mkuu wa serikali hatakataa kabisa na atawageuka wenzake.
 
Watanzania tunamuombea tena bila ya kulazimishwa kwani yeye ndiyo mzalendo wa kweli kuliko maccm wanao lazimisha kuaminiwa


Watanzania wepi hao? Mbona anapita kwa tabu Jimboni kwake huyo kilaza wako?
 

GREAT POINT!

Tuliofuatilia harakati za Lissu akipambana na manyanyaso na mikataba mibovu ya uwekezaji katika sekta ya madini tangu enzi za Mkapa, tunaheshimu sana mchango wake. Kikwete aliposema "heri Slaa kuwa rais kuliko Lissu kuwa mbunge", alikuwa akikumbuka jinsi Lissu alivyowapa taabu katika harakati zao hasa za kusuka dili kwenye mikataba ya madini.

Kama kweli Magufuli ana nia ya dhati ya kuinyosha sekta hiyo, basi amwalike Lissu kwa mashauriano makini ya ana kwa ana ya kuachana na malumbano ya kishabiki yasiyo na tija kabisa kwa taifa. Wapeane mikakati thabiti ya kung'oa na kufagilia mbali mizizi ya ufisadi iliyosimikwa ndani ya sekta ya madini na chama chake kwa miaka mingi. He needs to swallow his false pride and woo resourceful persons like Lissu to his side.

Magufuli ajue kuwa si kila anayemchekea huko CCM ni rafiki yake. Na si kila aliye upinzani anayeikosoa serikali yake ni adui yake. Tanzania ina watu wa ajabu sana. Wamejaa CCM wanampigia mahesabu tu kila hatua anayochukua. Asijekuta akiishia kushangaa sana huko siku za mbeleni. Mwalimu Nyerere mwenyewe siku zake za mwisho aliishia kuwa mpweke na aliyekata tamaa kuhusu mwelekeo wa CCM na nchi kwa ujumla (sikilliza hotuba zake za mwisho).
 
Mi sisomagi makala za huyu taahira. Kwanza ndeeefu.
 
Mi sisomagi makala za huyu taahira. Kwanza ndeeefu.
Ni hicho chama kimekufanya mjinga, na ni rahisi kumficha mjinga kwa maandishi. Hata viongozi wako, wako hivyo wanashindwa kusoma kilichoandikwa wanaishia kutia sahihi kwenye mikataba ya kishetani leo eti tunaibiwa.
 
Kila kinachochimbwa ni mali ya mwekezaji sawa, ila na sisi inabidi tukijue. Ila hawa wanatudanganya, hapo ndo wao wanapovunja mkataba kwasababu huo mkataba hauruhusu uongo.
 
Ni hicho chama kimekufanya mjinga, na ni rahisi kumficha mjinga kwa maandishi. Hata viongozi wako, wako hivyo wanashindwa kusoma kilichoandikwa wanaishia kutia sahihi kwenye mikataba ya kishetani leo eti tunaibiwa.
Swadakta kama ile mikataba 17 ya wachina iliyosainiwa kwa nusu saa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…