Tundu Lissu: Ninampinga Magufuli hadharani. Sio mnafiki na sijahongwa

Tundu Lissu: Ninampinga Magufuli hadharani. Sio mnafiki na sijahongwa

ukitaka kujua Tundu Lissu ni tahira hebu angalia anacho kiongea na sisi tunacho kiongea ni tofauti.
Yeye anafikiri watu wengi wana kataa kusafirishwa kwa mchnaga kumbe kikubwa kinachopingwa ni udanganyifu kwenye kilichomo kwenye mchanga... yeye alishawai kusema mikataba hii ni ya usiri sasa anaongelea nini kitu ambacho hajawai kukiona? hivi hiyo mikataba ndio inasema kuwa wawe wanadanganya kuna kiasi fulani cha dhahabu?
Hivi Tundu Lissu utahira atapona lini? Hata ACCACIA wanajua concern ya serikali ni kuhusu kiasi kilichomo kwenye mchanga au makanika na wao wanataka upimwe tena...
Lakini Tahira Lissu anapinga utafiti kwa tumbo na mdomo tuuu...
Mwenzie Zitto amenyamaza na kusema wazi kuwa utafiti hupingwa kwa utafiti..
Anacho zungumza lisu kinaeleweka sana labda wewe ndio huelewi.
 
Sijajua hiyo kamati ya pili iliyojaa wanasheria watamshauri vipi Rais lakini iwapo watataka kumfurahisha kwa kumdanganya Rais kama ile ripoti ya kamati ya awali basi nchi itaingia ktk mgogoro mkubwa wa kisheria na mwisho wa siku washindi ni BARRICK(ACACIA)
 
Aisee huu ushabiki ndo adui mkubwa sema huelewi siyo kosa lako, Kati ya hiyo tume iliyofanya uchunguzi wa kumfurahisha raisi na hao jamaa nani anadanganya ?? Unaambiwa kiasi cha madini kinacho semekana kimo kwenye mchanga huo kama ni kweli maana yake inamaanisha migodi ya buzwagi na hiyo ya musoma ndiyo inaongoza kwa utoaji wa dhahabu nyingi duniani. Sasa huoni hapo kuna udanganyifu umefanyika kumdanganya raisi!! Tumia hata muda wako kusoma usikurupuke kwa kuona vichwa vya habari.
 
Kwa nini wewe uiamini tume iliyopima yenyewe bila wawakilishi wa Acacia kushirikishwa.Just imagune,kama wangekuja na vipimo vile vile vya Acacia vya mwanzo,je mngewaamini?Si ngeanza kusema nao wamehongwa na Acacia?..Je hakuna uwezekano kwamba Tume imeleta yale majibu ili kuwa please wa TZ na rais?..
Ni kwa nini acacia hawakushirikishwa kama sababu ilikuwa ni kupata ukweli?,just think freely..
Ilishindikana nini kukaa na Acacia na kuunda indeprndent Committee ihusike na upimaji ili kuridhisha party zote..Yaani haiwezekani ukawaondoa Acacia kwenye hili zoezi sababu wao ni party of tha contract na chochote kitachotokea kitawaathiri moja kwa moja.
safi sana akili kama hizi ndo naziunga mkono,ni kama umesoma nnachowaza,uko on point asee
 
Hawa wazungu wamekuwa wanatuibia SANA, SANA. Lakini kiini cha wizi huo ni sheria mbovu zilizowezesha mikataba mibovu kusainiwa. Wabunge wa ccm ndio wamepitisha hizo sheria mbovu. Na wala marais waliopita sio wa kulaumiwa wao maana kwa kupitisha hizo sheria mbovu wabunge wa ccm wamewapa hao marais 'msingi' wa kuweka saini hiyo mikataba mibovu. Lazima tuelewe kwamba ACACIA HAWATOLIPA hicho kiasi tulichoambiwa wanadaiwa kwa sababu zifuatazo: a) Wameshakubaliana na Rais kwamba watalipa BAADA ya makubaliano kwenye mazungumzo kati yao na sisi. Sheria tulizopitisha zinasema hizo makinikia ni mali yao. Kwa hiyo hata kama makinikia ina thamani ya trilioni mia hiyo ni pesa yao sio yetu. b) Hata kama huo udongo una thamani ya trilioni mia kilicho CHETU HAPO NI ASILIMIA NNE TU yaani trilioni nne tu. c) ACACIA hawawezi kukubali majibu ya ile timu ya Mruma kwa sababu hawakushirikishwa. Watasema 'wamebambikiziwa' udongo uliopimwa na kwa vile hawakushirikishwa, watatushinda. d) Wakisema timu ingine yenye watu wao ianze kupima tena TUKUKUBALI TUMEKWISHA. Profesa Mruma na watu wake wamepima sawasawa makontena ambayo ndani yake hao wazungu walikuwa wameficha udongo wenye dhahabu nyingi. Makontena mengine yana dhahabu kidogo sana kwa kiwango ambacho ACACIA wanasema. Kwa hiyo, udongo wake ukipimwa tutaonekana upimaji wetu ulikuwa feki kuliko maelezo. Njia ya pekee ya kuwakamata ni kutumia makosa mengine waliyofanya. Miaka iliyopita kulikuwa na tetesi kwamba kuna watu waliofukiwa Bulyanhkulu. Kuna hizo sumu zilizozagaa kwenye maeneo ya migodi. Tunaweza kudai fidia kubwa sana kwa kuathiriwa afya za wananchi wetu. ACACIA wametuibia sana maana ndege zao zilikuwa zinaondoka na dhahabu nyingi sana na serikali haikifuatilia. Lazima tum-support Magufuli "kuwabamiza' kadiri iwezekanavyo lakini tutumie mbinu ingine tofauti na majibu ya upimaji wa makinikia
 
18622446_1126398777465538_2060351389369899505_n.jpg



Na mimi ni Mtanzania pia.

Tofauti kati yangu mimi na wewe na Magufuli ni hii: Mimi nimepigania nchi yangu katika masuala haya tangu mwaka '99.

Wakati huo tulikuwa na mgodi mmoja tu wa dhahabu, Resolute Golden Pride Nzega. Bulyanhulu ilikuwa haijajengwa. Geita ndio kwanza walikuwa wanafukuza wanakijiji wa Mtakuja.

Nadhani nilikuwa wa kwanza katika nchi hii kupiga yowe kwamba tutaibiwa sana kwenye sekta ya madini.

Wewe sijui ulikuwa wapi wakati huo. Najua Magufuli alikuwa wapi: upande wa MaCCM na wawekezaji hawa.

Nimepigana na wawekezaji hawa mahakamani, kwenye medani ya kisiasa ndani na nje ya nchi hii kwa zaidi ya miaka 15. Nimetetea wananchi completely free of charge Bulyanhulu, Tarime, Nzega, Geita, n.k.

Sijui wewe ulikuwa wapi lakini najua Magufuli alikuwa upande wa nani: wa MaCCM na wanyonyaji hawa.

Soma Rai ya tarehe 17 Julai, 2001, uone tulimwambia nini Mkapa siku anaenda kuzindua Mgodi wa Bulyanhulu.

Sijui ulikuwa wapi lakini najua Magufuli alikuwa wapi: alikuwa anatetea tumbo lake na matumbo ya wanyonyaji hawa.

Nilikamatwa na kushtakiwa kwa uchochezi kwa sababu ya Bulyanhulu. Hiyo ilikuwa December 2002. Nilikaa na kesi hiyo mahakamani Kisutu kwa miaka sita.

Sijui ulikuwa wapi ila najua Magufuli alikuwa wapi: upande wa watesi wa wananchi na wanyonyaji wa rasilmali zetu.

Leo Magufuli anajifanya mzalendo na anahoji uzalendo we yeyote anayepingana nae.

Ni muongo. Anatafuta umaarufu wa kisiasa kwa wasiojua na wasiokumbuka. Ataupata. Kwa siku chache tu. Mark my words: ataumbuka na mtaumbuka.

Mimi ninampinga hadharani. Sio mnafiki, na sijahongwa. Ninampinga kwa sababu atatusababishia matatizo makubwa zaidi kuliko tuliyonayo sasa.

Huo mchanga atauachia upelekwe ambako umepelekwa kwa miaka 16 iliyopita. Kama sheria ndiyo hiyo na mikataba ndiyo hiyo hana pakwenda.

Tatizo ninaloliona ni kwamba by the time anawarudishia mchanga wao, Tanzania itakuwa imekuwa a basket case kama Zimbabwe.

Na tutakuwa tumelipishwa mapesa mengi kama fidia na arbitral tribunals za kimataifa kwa kuvunja mikataba na wawekezaji hawa.

Kama kuna anayefikiri uzalendo ni kufumbia macho masuala haya basi huyo na amuunge mkono Magufuli kwenye upofu wake wa kujitakia.

Ripoti ya Prof. Mruma haitamaliza hata nusu saa under serious scrutiny. Zaidi ya majina ya maprofesa walioiandaa, ripoti hii haina credibility yoyote. Ni kazi ya kisiasa iliyopakwa rangi ya usomi.

Kama umefuatilia taarifa za kitaalamu za Bulyanhulu hata kabla ya Barrick Gold kuingia mwaka '99 utajua ninasema nini.

Sutton Resources, Outukumpu Oy na hata STAMICO walishafanya utafiti mkubwa juu ya utajiri wa Bulyanhulu. Taarifa zipo na zimekuwepo kwa hata mbumbumbu wa jiolojia ya madini kama mimi.

Hiki alichoambiwa Magufuli ni rubbish, hata kama ni ya kiprofesa. Rubbish. Hatuibiwi kwenye mchanga, that's the rubbish fed on the unlettered.

Tunaibiwa kwenye sheria. Kama hamuoni hilo then God have mercy on us.
Sijawahi kuona kipindi au wakati ambao wananchi wamegoma kuyumbishwa na wanasiasa km sasa watu wapo silious kula msimamo ili waone mstakabari wao wa maisha wewe naye unakuja na historia? Lkn pia Lisu anajua vyema ktk siasa za Tz zinafanana tu ila tatizo ni mapenzi ya kupitiliza mf.km anachoongea anamaanisha mbona hamtaji Lowasa &Sumaye? Kwanini anamtaja Magufuli peke yake? Huoni kuwa huu nao ni usanii tu km fisadi aliyeandikwa miaka nenda rudi na hawa2 tunaowaita wasomi na wazalendo? Leo wanamuona ndoo shujaa[emoji1] [emoji2] [emoji99] [emoji99] na mkombozi wa wanyonge.
 
P Rutashobolwa usikasirike utafiti kwa utafiti. Sisi tunamwelewa Lissu vizuri.
1. Muhimu zaidi ni mikataba
2. Hivo vipimo walivyotoa maprof siyo sahihi
3. Kuzuia wakati wamefuata kilichoandikwa kwenye mikataba inaweza kutuletea gharama kama taifa.
Sasa hapo huna sababu ya kumtukana njoo tu na hoja yako.
Shida ya miccm ni hiyo. Kutukana badala ya hoja na pia wana uwongo kutaka kutudanganya kuwa Lissu ndiye msaliti na siyo viongozi wetu wa zamani na wabunge wao!!!
 
Watanzania shule hazitusaidii maana tumezoea kila kitu kujiuliza kwa sangomas
 
Najiuliza sana swali dogo tu kila nikiona post ya Lisu kiufupi nasubiri apost kuwa amepima yeye au kashuhudia upimaji wa huo mchanga na kajiridhisha kuwa hatuibiwi,nitamuelewa sana,tofauti na hapo aendelee kusoma takwimu na historia kwenye makaratasi hadi pale atakapo ikomboa nchi kwa takwimu na sheria
Hujaelewa! Hasemi kuwa hatuibiwi! Bali anasema tulihalalisha huo wizi kwa kutunga sheria na kusaini mikataba inayowapa mwanya wa kutuibia! Kwa hiyo tuliibiwa kwenye sheria! Huo mchanga ni wao! Sana sana chetu hapo ni 4%!
 
Najiuliza sana swali dogo tu kila nikiona post ya Lisu kiufupi nasubiri apost kuwa amepima yeye au kashuhudia upimaji wa huo mchanga na kajiridhisha kuwa hatuibiwi,nitamuelewa sana,tofauti na hapo aendelee kusoma takwimu na historia kwenye makaratasi hadi pale atakapo ikomboa nchi kwa takwimu na sheria
Bora ungenyamaza Mkuu. Umejinyea..
 
Lissu is a classic example of a loose cannon. Watu kama Lissu ni wazuri sana kuongea lakini ukimkabidhi zizi mifugo yote itakufa kwa funza. He will do nothing apart from lecturing the planet earth. No wonder baada ya miaka 8 alikuwa matapishi, shamelessly.
Ni Bora yeye kuliko wewe.
 
Najiuliza sana swali dogo tu kila nikiona post ya Lisu kiufupi nasubiri apost kuwa amepima yeye au kashuhudia upimaji wa huo mchanga na kajiridhisha kuwa hatuibiwi,nitamuelewa sana,tofauti na hapo aendelee kusoma takwimu na historia kwenye makaratasi hadi pale atakapo ikomboa nchi kwa takwimu na sheria
Jiulize walienda kupima wapi mchanga ndio utaweza kupata jibu lako. Haiwezekani uchukue kilo moja kati ya kilo 1000 afu ufanye sampo ya makotena 270 huu ni utoto. Ila wangetaka kupata sampo ya uhakika wangechukua kontena moja ndio liwe sampo ya makontena 270.
 
Lissu tangu lini ulikuwa mzalendo! Uzalendo wa kutetea fisadi lowasa, au uchumia tumbo upi anausema zaidi ya huu wa kupewa kitu kidogo kumsafisha mtu aliye mchafua kwa miaka 10. Lissuu wadanganye vipofu wa vabichaa
Tundu Lissu ni mzalendo namba 2 Tanzania baada ya BABA WA TAIFA.

Yaani kama mpaka Leo fisadi unamuona ni Lowassa basi wewe akili zako zinatosha kukusaidia kufunga kamba za viatu pekee.

Tulishaambiwa maagizo yalikua yanatoka juu sasa cjui huelewi aliyekua juu ni nani au unaamua kujitoa ufahamu ?

Lowassa kajiuzuru 2007,sasa jiulize ni matukio mangapi ya kifisadi yameendelea kutokea baada ya 2007 mpaka sasa???
 
Tundu Lissu ni mzalendo namba 2 Tanzania baada ya BABA WA TAIFA.

Yaani kama mpaka Leo fisadi unamuona ni Lowassa basi wewe akili zako zinatosha kukusaidia kufunga kamba za viatu pekee.

Tulishaambiwa maagizo yalikua yanatoka juu sasa cjui huelewi aliyekua juu ni nani au unaamua kujitoa ufahamu ?

Lowassa kajiuzuru 2007,sasa jiulize ni matukio mangapi ya kifisadi yameendelea kutokea baada ya 2007 mpaka sasa???
thibitisha, uzalendo wa lissu
 
Back
Top Bottom