Tundu Lissu: Ninampinga Magufuli hadharani. Sio mnafiki na sijahongwa

Unasubiri mafisadi kuisha CCM mkuu? Unapoteza muda wako. Jiulize tangu magufuli aingie madarakani amewafukuza wangapi na bado anaendelea kila siku.lakini hawaishi. Jaribu kushangaa
 

Ukiachia kwamba Tindu Lissu anajibu kwa jazba na lugha ya kuuzi lakini hana tofauti sana na lugha za mkulu, ila ana hoja ya msingi. Ni ukweli kwenye hiyo mikataba tunaibiwa na yeye Lissu alipiga kelele tena ya dhahiri juu ya wizi huu. Lakini hakuna mahali popote ambapo Magufuli aliwahi kupinga kuhusu hii mikataba licha ya kuwa mwanaccm, mbunge na waziri katika serekali zote mbili zilizopita ambazo ndio zimeingiza nchi hii kwenye huo wizi. Tumpongeze Magufuli kwa kuthubutu kuchukua hatua sasa japo anapaswa kuchukua hatua zaidi ya kupitia upya mikataba hii, na ikibidi mikataba hiyo ipelekwe bungeni ikapitiwe upya kwani ccm ndio iliyoshabikia mikataba hii kuwa ya siri hatimaye kujikuta tunapigwa.

Unapounga mkono hicho kiasi tunachopata bado nakuuona ni mpuuzi fulani, haiwezekani nchi yetu ikawa inapata mrahaba wa 3% eti useme ni sawa kisa wabunge na viongozi waandamizi wa ccm walipitisha mikataba hiyo. Kuliko kupata 3% kama mrabaha ni bora hayo madini yasichimbwe mpaka wenye uwezo wa kuyachimba kwa faida watakapozaliwa. Mbona Nyerere amekaa kwenye urais wa nchi hii kuliko mtanzania yeyote na wala hakuwa na pupa ya kuyachimba hayo madini?
 
Ni ukweli ulio wazi kuwa tunaibiwa lakini tunaibiwa kihalali na kisheria, maana mikataba yetu tuliyoingia na hawa wazungu ni kwamba wabebe kila kitu waende nacho. Zitto Kabwe alifukuzwa mpaka bungeni kwa sababu ya kutetea rasilimali ya madini, Tundu Lissu amefungwa mara kadhaa kwa sababu ya kutetea madini yetu yasiibiwe. Mikataba hii ya madini yote ilisainiwa kipindi Magufuli akiwa serikalini hajawahi kuonesha makali yoyote eti leo ndiyo mzalendo?
 
Lissu tangu lini ulikuwa mzalendo! Uzalendo wa kutetea fisadi lowasa, au uchumia tumbo upi anausema zaidi ya huu wa kupewa kitu kidogo kumsafisha mtu aliye mchafua kwa miaka 10. Lissuu wadanganye vipofu wa vabichaa
Hata shetani anakuogopa.
 
Mtalipishwa sana tena sana mpaka mtaona aibu haiwezekani hii nchi ikawa inaendeshwa kwa mikurupuko. Sheria inasema nini kuhusu hiyo mikataba? Unafikiri hayo madini ni yetu? Hata ukiambiwa yapo gram ngapi unafikiri yatabaki hapa bongo?
 
Hivi mnapomtukana Lisu mnaona hiyo mikataba ya madini ni sawa? Kama leo wewe una shamba lako halafu akaja mtu akakwambia amegundua shambani kwako kuna dhahabu na atakusaidia kuichimba lakini katika dhahabu atakayouza atakupa wewe mwenye shamba lenye dhahabu shilingi ELFU NNE TU katika kila shilingi LAKI MOJA utakubali? Mnaona ni sawa hawa wawekezaji wa madini watulipe kiasi kidogo hivyo?
 
unaambiwa kwa viwango vya tume acacia ni ya tatu duniani kwa uzalishaji wa dhahabu bado unaamini hiyo ripoti?
mi najipa muda kuamini
 

Soma alichokiandika Lissu na ujue jinsi tunavyoibiwa. Usikimbilie kuandika
 
kwa kweli naona ile mbegu tayari inamea, ukisema kitu tofauti na mawazo ya mkulu, bhasi inaonekana unampinga juhudi zake, hakuna MTU anayochukia, Ila watu wanatoa ushauri no nini tufanye ili kuepuka hasara mbeleni kisheria, yaani siku hizi ukishauri kitu unakua kama msaliti flan hivi, hii sio nzuri ndio maana kuna lugha humu zinatumia maneno ya kuudhi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…