Tundu Lissu: Ninampinga Magufuli hadharani. Sio mnafiki na sijahongwa

Tundu Lissu: Ninampinga Magufuli hadharani. Sio mnafiki na sijahongwa

Ni kweli Lisu ameanza miongo miwili iliyopita akiwa na LEAT. Lakini ccm enzi hizo ndio waliotufikisha hapa.
 
18622446_1126398777465538_2060351389369899505_n.jpg

Na mimi ni Mtanzania pia.

Tofauti kati yangu mimi na wewe na Magufuli ni hii: Mimi nimepigania nchi yangu katika masuala haya tangu mwaka '99.

Wakati huo tulikuwa na mgodi mmoja tu wa dhahabu, Resolute Golden Pride Nzega. Bulyanhulu ilikuwa haijajengwa. Geita ndio kwanza walikuwa wanafukuza wanakijiji wa Mtakuja.

Nadhani nilikuwa wa kwanza katika nchi hii kupiga yowe kwamba tutaibiwa sana kwenye sekta ya madini.

Wewe sijui ulikuwa wapi wakati huo. Najua Magufuli alikuwa wapi: upande wa MaCCM na wawekezaji hawa.

Nimepigana na wawekezaji hawa mahakamani, kwenye medani ya kisiasa ndani na nje ya nchi hii kwa zaidi ya miaka 15. Nimetetea wananchi completely free of charge Bulyanhulu, Tarime, Nzega, Geita, n.k.

Sijui wewe ulikuwa wapi lakini najua Magufuli alikuwa upande wa nani: wa MaCCM na wanyonyaji hawa.

Soma Rai ya tarehe 17 Julai, 2001, uone tulimwambia nini Mkapa siku anaenda kuzindua Mgodi wa Bulyanhulu.

Sijui ulikuwa wapi lakini najua Magufuli alikuwa wapi: alikuwa anatetea tumbo lake na matumbo ya wanyonyaji hawa.

Nilikamatwa na kushtakiwa kwa uchochezi kwa sababu ya Bulyanhulu. Hiyo ilikuwa December 2002. Nilikaa na kesi hiyo mahakamani Kisutu kwa miaka sita.

Sijui ulikuwa wapi ila najua Magufuli alikuwa wapi: upande wa watesi wa wananchi na wanyonyaji wa rasilmali zetu.

Leo Magufuli anajifanya mzalendo na anahoji uzalendo we yeyote anayepingana nae.

Ni muongo. Anatafuta umaarufu wa kisiasa kwa wasiojua na wasiokumbuka. Ataupata. Kwa siku chache tu. Mark my words: ataumbuka na mtaumbuka.

Mimi ninampinga hadharani. Sio mnafiki, na sijahongwa. Ninampinga kwa sababu atatusababishia matatizo makubwa zaidi kuliko tuliyonayo sasa.

Huo mchanga atauachia upelekwe ambako umepelekwa kwa miaka 16 iliyopita. Kama sheria ndiyo hiyo na mikataba ndiyo hiyo hana pakwenda.

Tatizo ninaloliona ni kwamba by the time anawarudishia mchanga wao, Tanzania itakuwa imekuwa a basket case kama Zimbabwe.

Na tutakuwa tumelipishwa mapesa mengi kama fidia na arbitral tribunals za kimataifa kwa kuvunja mikataba na wawekezaji hawa.

Kama kuna anayefikiri uzalendo ni kufumbia macho masuala haya basi huyo na amuunge mkono Magufuli kwenye upofu wake wa kujitakia.

Ripoti ya Prof. Mruma haitamaliza hata nusu saa under serious scrutiny. Zaidi ya majina ya maprofesa walioiandaa, ripoti hii haina credibility yoyote. Ni kazi ya kisiasa iliyopakwa rangi ya usomi.

Kama umefuatilia taarifa za kitaalamu za Bulyanhulu hata kabla ya Barrick Gold kuingia mwaka '99 utajua ninasema nini.

Sutton Resources, Outukumpu Oy na hata STAMICO walishafanya utafiti mkubwa juu ya utajiri wa Bulyanhulu. Taarifa zipo na zimekuwepo kwa hata mbumbumbu wa jiolojia ya madini kama mimi.

Hiki alichoambiwa Magufuli ni rubbish, hata kama ni ya kiprofesa. Rubbish. Hatuibiwi kwenye mchanga, that's the rubbish fed on the unlettered.

Tunaibiwa kwenye sheria. Kama hamuoni hilo then God have mercy on us.
Hapo amesema vyema
 
Ametufukuzia muhongo wetu na umeme umeanza kukatwa toka Jana. Kigamboni Jana umekatwa asubuhi umerudishwa saa tano usiku. Sasa hivi hapa Kariakoo tayari umeshakatwa. Haya matatizo tulishaanza kuyasahau.
 
KWA NINI TUSIELEWE?
MFANYABIASHARA ANAPAKIA BANGI KUPELEKA INCHI JIRANI KWA KUCHANGANYA NA PUMBA YA MAHINDI.
BANGI INASAFIRISWA KWA JINA LA PUMBA.
TUJIRIDHISHE KWANZA, JE DHAHABU ILYOKO KWENYE MCHANGA NI NYINGI KULIKO TULIVYOKUBALIANA KWENYE MKATABA?
HAKUNA WIZI MDOGO, WIZI NI WIZI TU.
TUANZE NA WIZI MDOGO THEN TWENDE KWENYE ULE MKUBWA.
LISSU SHIRIKIANA NA RAIS KATIKA HILI KWA SABABU UMULIPIGANIA MUDA MREFU NA SASA AMEKUJA MTU AMBAYE ANATAKA KUFANYA ULIYOKUWA UNATAKA.
UKIMTUHUMU HATAKUBALI KUSHIRIKIANA NA WEWE HATA KAMA UNA UWEZO KIASI GANI.
ACHA RAIS ASHUNG'ULIKIE HILI SWALA KISIASA, KIUCHUMI, KISHERIA, KISAYANSI, KIDINI NA HATA KWA KUTUMIA NGUVU INGINE YEYOTE INAOKUBALIKA NA MUNGU AU ISIYOKUBALIKA ILI MRADI SISI TUSHINDE.
TUSIGOMBANIE SILAHA WAKATI TUNAPIGANA VITA MOJA.
CHADEMA WAJUE KAMA SI WAO KUMCHAFUA LOWASSA, LOWASA ANGEKUA RAIS WA INCHI HII KUPITIA CCM.
KWA MAANA HIYO NA KWA WATU WACHAMBUZI WA MAMBO, RAIS WA SASA YUKO MADARAKANI KWA MSAADA MKUBWA TOKA CHADEMA.
LEO LOWASA ANGEKUWA RAIS WA INCHI HII KUPITIA CCM MNGEMPIGIA KELELE ZAIDI NA ANGEWATANDIKA NAKUWAWEKA NDANI BILA HURUMA.
Kwani rais angependa kushirikiana na Lisu?
 
Ajue asijue kwahiyo aache tu madhara yaendelee?
Utadhuiaje madhara wakati ulikuwa na utashi na akili kipindi unaridhia miswaada mibovu na kandamizi ya madini ipite,afadhari angeonekana wa maana kama kipindi hicho alikuwa anapinga tungemsifia kwa hilo leo hi unasimamisha bodi nzima wakati baba yao Mkapa unamuacha kisa tu anakinga ya rais
 
18622446_1126398777465538_2060351389369899505_n.jpg

Na mimi ni Mtanzania pia.

Tofauti kati yangu mimi na wewe na Magufuli ni hii: Mimi nimepigania nchi yangu katika masuala haya tangu mwaka '99.

Wakati huo tulikuwa na mgodi mmoja tu wa dhahabu, Resolute Golden Pride Nzega. Bulyanhulu ilikuwa haijajengwa. Geita ndio kwanza walikuwa wanafukuza wanakijiji wa Mtakuja.

Nadhani nilikuwa wa kwanza katika nchi hii kupiga yowe kwamba tutaibiwa sana kwenye sekta ya madini.

Wewe sijui ulikuwa wapi wakati huo. Najua Magufuli alikuwa wapi: upande wa MaCCM na wawekezaji hawa.

Nimepigana na wawekezaji hawa mahakamani, kwenye medani ya kisiasa ndani na nje ya nchi hii kwa zaidi ya miaka 15. Nimetetea wananchi completely free of charge Bulyanhulu, Tarime, Nzega, Geita, n.k.

Sijui wewe ulikuwa wapi lakini najua Magufuli alikuwa upande wa nani: wa MaCCM na wanyonyaji hawa.

Soma Rai ya tarehe 17 Julai, 2001, uone tulimwambia nini Mkapa siku anaenda kuzindua Mgodi wa Bulyanhulu.

Sijui ulikuwa wapi lakini najua Magufuli alikuwa wapi: alikuwa anatetea tumbo lake na matumbo ya wanyonyaji hawa.

Nilikamatwa na kushtakiwa kwa uchochezi kwa sababu ya Bulyanhulu. Hiyo ilikuwa December 2002. Nilikaa na kesi hiyo mahakamani Kisutu kwa miaka sita.

Sijui ulikuwa wapi ila najua Magufuli alikuwa wapi: upande wa watesi wa wananchi na wanyonyaji wa rasilmali zetu.

Leo Magufuli anajifanya mzalendo na anahoji uzalendo we yeyote anayepingana nae.

Ni muongo. Anatafuta umaarufu wa kisiasa kwa wasiojua na wasiokumbuka. Ataupata. Kwa siku chache tu. Mark my words: ataumbuka na mtaumbuka.

Mimi ninampinga hadharani. Sio mnafiki, na sijahongwa. Ninampinga kwa sababu atatusababishia matatizo makubwa zaidi kuliko tuliyonayo sasa.

Huo mchanga atauachia upelekwe ambako umepelekwa kwa miaka 16 iliyopita. Kama sheria ndiyo hiyo na mikataba ndiyo hiyo hana pakwenda.

Tatizo ninaloliona ni kwamba by the time anawarudishia mchanga wao, Tanzania itakuwa imekuwa a basket case kama Zimbabwe.

Na tutakuwa tumelipishwa mapesa mengi kama fidia na arbitral tribunals za kimataifa kwa kuvunja mikataba na wawekezaji hawa.

Kama kuna anayefikiri uzalendo ni kufumbia macho masuala haya basi huyo na amuunge mkono Magufuli kwenye upofu wake wa kujitakia.

Ripoti ya Prof. Mruma haitamaliza hata nusu saa under serious scrutiny. Zaidi ya majina ya maprofesa walioiandaa, ripoti hii haina credibility yoyote. Ni kazi ya kisiasa iliyopakwa rangi ya usomi.

Kama umefuatilia taarifa za kitaalamu za Bulyanhulu hata kabla ya Barrick Gold kuingia mwaka '99 utajua ninasema nini.

Sutton Resources, Outukumpu Oy na hata STAMICO walishafanya utafiti mkubwa juu ya utajiri wa Bulyanhulu. Taarifa zipo na zimekuwepo kwa hata mbumbumbu wa jiolojia ya madini kama mimi.

Hiki alichoambiwa Magufuli ni rubbish, hata kama ni ya kiprofesa. Rubbish. Hatuibiwi kwenye mchanga, that's the rubbish fed on the unlettered.

Tunaibiwa kwenye sheria. Kama hamuoni hilo then God have mercy on us.

Hatuibiwiw kwenye mchanga tunaibiwa kwenye sheria duhhh hapo tu dah so sad
 
kama kweli watanzania wana uchungu na nchi hii waseme ukweli haya yote yanayotendeka yanafanyika katika utawala wa chama gani? na je?hakunawatu walikuwa wanalalamikia haya?tukibaki kujipendekeza kwa watu walioko madarakani tutazidi kuibiwa. ukwaeli ni kwamba yote haya yamefanyika chini ya utawala wa ccm hivyo bila kuwa wakweli wa kuwaondoa ccm madarakani tukubali kila mtu aishi kwa ujaja wake
Uko vizuri sana ndugu . . [emoji106] [emoji106]

Tukiendelea kutaja taja vimajina vya JPM, Mkapa, Chenge , Polepole . . , tujue kuwa wote hawa ni walewale toka mwaka 1961 . .
Wanapeana deals za wizi tuu, hawataki KATIBA MPYA, hawataki UHURU WA HABARI, UKISEMA UNANG'OLEWA KUCHA, UKIIMBA UNATEKWA . . , mbona hawa ccm hawafai kabisa jamani hamwoniiiii . .

Subiri uchaguzi ufike uone watakavyokuja na ngonjera . . , kuleta sheria mpya ya TUME HURU YA UCHAGUZI hawataki . . , kazi kuwanunua wasanii njaa wasiojitambua kuwafanyia campaign . .
Na hela za kuhonga wakati wa uchaguzi ndio zinatoka huko huko kwenye mi mikataba mibovu ya madini, utalii, Loliondo, Mchuchuma . . Hao ndio CCM bwana . .
 
Swadakta kama ile mikataba 17 ya wachina iliyosainiwa kwa nusu saa
Nshozi . . ,

Bado kuna madudu mengi saaana ya ccm hayajafumuka . .

1. Kuna CHUMA cha Mchuchuma na LIGANGA, yale madini pale ni yetu au tulishawapa wachina . . ?!

2. LOLIONDO ni jipu jingine la ccm linalosubiri kulipuka . .

3. IPTL . . , imeishaje ile skandali . . ?! JPM yupo au hayupo . . ?

Ongezeeni majipu mengine mnayoyajua . .
 
Kama ni kweli Lisu mkweli, angepingana na chama chake ujio wa Lowasa CHADEMA kwa sababu ni yeye aliyekuja na list of shame. Sasa swali kwake ni kitu gani kilichomfanya amkubali Lowasa wakati kwa miaka nane anamwimba kuwa fisadi. Hii inadhihirisha kuwa watanzania ni vigeugeu, Lisu anajua kwa nini alimkubali Lowasa kwa sababu pesa yake tu na si vinginevyo na nina imani hata leo Rais akimteua kwa mwanasheria Mkuu wa serikali hatakataa kabisa na atawageuka wenzake.
Nani kakwambia siasa ni uadui?kila kiongozi anaweza kubadili tabia kama amekusudia
 
Huyu ndiye mpiganaji wa ukweli sio yule mwingine anayetafuta kick kwa kufukuza mawaziri huku akijua tatizo lipo kwenye mikataba
Binafs nilimjua Lissu kutokana na hizi mambo za madini.Alikua akialikwa sana na Masako kwenye kipindi cha Kipima Joto na alikua akienda pale anaenda kama mtetez wa mazingira hasa huko migodini.Miaka hiyoooo
 
Lissu tangu lini ulikuwa mzalendo! Uzalendo wa kutetea fisadi lowasa, au uchumia tumbo upi anausema zaidi ya huu wa kupewa kitu kidogo kumsafisha mtu aliye mchafua kwa miaka 10. Lissuu wadanganye vipofu wa vabichaa
_20170527_141404.JPG

Umemjua Lissu mwaka 2010 wewe.
Ila Chenge ndo mzalendo
 
Tatizo la Lissu anaongea sana bila kurecommend au kuingia kusaidia nini kifanyike ili kushinda Vita hii.

Maneno makali na kebehi hayatasaidia kuiokoa nchi yetu dhidi ya unyonyaji wa nje.

Rais ameanzisha Vita ambayo huko nyuma anakokulalamikia Lissu hakuwa na misuli hiyo.

Lissu aungane na timu ya Magufuli, tusonge mbele.

Ushindi wa JPM ni wetu sote, kushindwa kwake ni hasara yetu sote mpk ya Lissu mwenyewe
 
Kweli kabisa ulichoongea. Hata mi uzalendo wake siuoni maana Lowassa ndo mwenye Acacia na ndo anayewaibia dhahabu na kusafirisha mchanga.

Kwa akili hii usipochukua nafasi ya Muhongo, utakuwa umeonewa na udai haki yako.
Hahahaaa eti adai chake
 
Back
Top Bottom