Tundu Lissu: Ninampinga Magufuli hadharani. Sio mnafiki na sijahongwa

Tundu Lissu: Ninampinga Magufuli hadharani. Sio mnafiki na sijahongwa

Huyu naye siasa tu, Hivi alitaka Mh. Rais afanyeje katika Swala kama hili si aseme, kazi kulalamika. Kwa maelezo yake nafikiri ulikuwa ni wakati sasa kumuunga Raisi mkono......
 
Huyu naye siasa tu, Hivi alitaka Mh. Rais afanyeje katika Swala kama hili si aseme, kazi kulalamika. Kwa maelezo yake nafikiri ulikuwa ni wakati sasa kumuunga Raisi mkono......
Raisi aungweje mkono na Lissu . . Hebu eleza na sie tuelewe . .
 
Na kweli wewe ni Dumb wala hujakosea..Magufuli wakati kipindi hicho anasema Ndiyo mswaada wa madini upite alikuwa hajui faida na madhara yake? Au alikuwa anaunga mkono ilimradi tu bora liende?
Katika mkataba kati ya ACACIA na serikali ni wapi panaposema kuwa ACACIA wanaweza kutudanganya kiasi cha dhahabu kilichopo ndani ya mchanga wanaosafirisha?

Mikataba haina uhusiano wowote na WIZI uliobainishwa katika huu mchanga uliokamatwa.

Focus on the issue at hand. Ni kweli mikataba ni mibovu. Hata CEO wa ACACIA amekiri hilo. Lakini hili sakata la mchanga halikusababishwa na mkataba mbovu. Ni WIZI, period.
 
Kama unadai kuibiwa mchanga unaweza kutueleza huo mchanga uliuchimba lini wapi na kwa namna ipi!!?
UKOME KUYAPAKAZIA UZEMBE MAJESHI YETU YA ULINZI NA USALAMA WA MIPAKA, MAISHA NA MALI ZETU WATANZANIA.
Jamani shule inasaidia sana. Ningekujibu kama swali lako lingeeleweka.

Naona jazba tu lakini sielewi unauliza nini.
 
Jamani shule inasaidia sana. Ningekujibu kama swali lako lingeeleweka.

Naona jazba tu lakini sielewi unauliza nini.
Unaonyesha dhahiri kuwa bila kimondo hufaulu mtihani hata wa chekechea.
 
Tundu Lissu hajui hata namna ipi bora ya kushauri nchi inapokuwa vitani ....anaropoka kama vile ni ile michezo ya Chadema vs CCM ....anakuja na ngojera za kuanza kupigania issues za madini toka 99 na anatumia kigezo hicho kuponda kuwa hatuibiwi kwenye mchanga!!! ....hivi hiyo mikataba hata kama ingekuwa na ubora kiwango anachotaka yeye ....itaweza kuzuia udanganyifu kama huu ukihusisha maafisa wa serikali? Mbona anamshambulia JPM kuwa anajua alikuwa upande upi kipindi mikataba inasainiwa lakini hawataji mawaziri wakuu walioshiriki kama wakuu wa serikali ambao wapo nao huko Chadema? ....Tundu Lissu asitake kutafuta sifa kwenye issues za kitaifa ....maoni yake ni kama anatamani kuwasaidia ACACIA kuishtaki serikali .....atafute namna ya kutoa maoni yake kwa faida ya taifa na si kuropoka ovyo kama vile hii ni siasa .....Tundu Lissu amevimba kichwa inabidi aambiwe ukweli ....

..jaribu kuwa balanced.ukishindwa
hilo jaribu ktk mijadala hii kuchambua "mchele" na "pumba" uachane nazo.

..hayo mambo hayatokei tu. Kuna mahali tumejikwaa. Ni lazima tupajue, na siyo kuwa fixated na tulipoangukia.

..kwa maoni yangu, mazingira mabovu ya kisiasa yamesababishwa au yanachochewa na Mzee mwenyewe.

..kwa maoni yangu Mzee haamini ktk dhana ya demokrasia ya vyama vingi. Hili nililisema tangu hajawa "mtu mkubwa."

..Lingine nadhani haamini ktk rule of
law. Anataka yeye asimike sheria na taratibu.

..Zaidi Mzee hana uvumilivu kwa yeyote mwenye mawazo tofauti na ya kwake. Jaribu kumsikiliza jinsi anavyowaadhiri wale aliotofautiana nao kimtizamo.

..Kwa maoni Mzee ndiyo chanzo cha kuchafuka kwa hali ya kisiasa na kijamii nchini. Vilevile ndiyo kikwazo cha hali hiyo kutengemaa.

SAKATA LA MIKATABA YA MADINI.

..CCM walipaswa kuonyesha UUNGWANA kwa kukiri makosa ya kuruhusu dhuluma hii iendelee kwa miaka 15++.

..RAISI na Mwenyekiti wa CCM alipaswa kuliomba RADHI taifa kutokana na maamuzi ya serikali za CCM yaliyolitia taifa hasara.

..Raisi alipaswa kutambua mchango wa wanaharakati kuwa walikuwa sahihi na waliweka maslahi ya taifa mbele.

..Katika hili WANAHARAKATI walitakiwa kutambuliwa kama MASHUJAA wa taifa letu.

..Kama kiongozi alipaswa kuliunganisha taifa na kusititiza umuhimu wa mchango wa kila Mtanzania.


..Baada ya hapo sasa ndipo Raisi angetangaza vita dhidi ya wawekezaji wanaotuibia.

Cc Nguruvi3
 
Kwani umeisoma vizuri andiko lililotolewa humu au unakurupuka tu,,maana kina sizonje mpo wengi. Labda nikueleweshe tu kauli na maana ya anachokiongea Tundu Lissu,, yy hajasema wala kukataa kuibiwa mchanga wenye madini,maana kwa miaka mingi wamekuwa wakiongea kuhusu uwizi huo na mkuu wa kaya na maficm wenzake wamekuwa wakitetea kwa kuipitisha tena kwa vifijo na nderemo na huyuhuyu mkuu akiwa mmoja wao hatujawahi kumsikia hata mara moja akihoji zaidi ya kusuport kila miswada ya madini ambayo ni mibovu ikiletwa bungeni wakati huo,na ni hawahawa wakina Tundu walikuwa wakiwaasa kuwa kuna uwizi mkubwa unafanyika,,. Sasa alichokiongea Tundu Lissu ni kuwa hapo tunachoibiwa sisi ni mikataba mibovu tuliyoingia na ndio maana akasema siku ya mwisho tutawarudishia aidha mchanga wao huo tunaojibatiza kuwa ni wetu na tunaibiwa au tukitumia mabavu kuuchukua na kuvunja nao mikataba tuliyoingia chaka wenyewe na kuipitisha kwa kuibariki kwa zimwi la kiitikadi na kuacha uzalendo eti sababu upo chini ya himaya yetu basi itabidi tuwalipe hela nyingi ambayo tutajuta kwa kutafuta sifa ya kisiasa ya mda mfupi,. Yaani maana yake badala ya kuangalia tulipojikwaa tunaangalia tulipoangukia,,au hamkumbuki ngano mbovu ya bakressa,,?? Kilichotokea kwa kumpa utajiri wa bure kama fidia iliyopelekea hadi leo ni mmoja kati ya matajiri wakubwa Afrika na yote ni nn,,!!? Sifa za kijinga
Nimesoma mistari miwili tu ya reply yako nikagundua huwezi kujenga bure,ila ukilipwa unabomoa,una nini cha kunielewesha wewe,unavyodai sijamuelewa Lisu so unahisi wewe nikuelewe na mitusi yako,endelea kubomoa
 
Kwenye siasa na hasa siasa za kipumbavu za ccm ni kutengeneza matatizo na kuja kujifanya wanayatatua baadae.....yaani hiki ni chama cha sanaa na wizi mtupu. Matukio mengine yapo hawayatatui mpaka watz wateseke ndipo wao wanakuja na kujifanya wanatatua.....
Magufuli was is and will never be a hero coz he is a member of corrupt system of ccm which consistently destroys watz.....
I will the very last person to agree on any move initiated by ccm

veri truuuuu!
 
Ni muongo. Anatafuta umaarufu wa kisiasa kwa wasiojua na wasiokumbuka. Ataupata. Kwa siku chache tu. Mark my words: ataumbuka na mtaumbuka.

Mh. Lissu na wewe ulikuwa unalipwa na wazungu hao hao kwa maslahi yao huku ukitafuta sifa zilizo kupa ubunge
 
Tundu, yawezekane ulifanya hivo lakin no prove of success, kama mlizunguka taifa zima mkinenea uma kuwa flani ni fisadi, na umma ukaamini na kwa kulinda heshima mh. Ka resign. Baada tu hatujasahau mkageuza shingo wewe ukiwepo na kusema huyu jamaa msafi sana basi tu mpeni usukan.
Hata sasa watu wamekosa kukuamini kama hujajua asi me nakuibia siri wanaona unaongeaga tu wakati wa tukio baada ya hapo hulikana tukio kwa nguvu zote
So matatizo this one
 
Jamani eee!!! aliyeianzisha hii vita ni Mh Magufuli na kajipangia namna ya kuipigana. Kaunda kamati mbili za kumshauri. Kamti ya kwanza imetoa majibu na maoni bado ya pili.
Kutletea maoni ya huyu mwehu humu ni kutuchosha sana. Maprofesa na madokta washeria na uchumi wamo kwenye kamati ya pili watamshauri kisheria limekaaje. Chochote watakacho shauri ndicho kitakachofanyika. Lisu na wapuuzi wengine wasimsafishe mtoto bado anajisaidia waache kihelehele.
Hata Lipumba ni Profesa!
 
Back
Top Bottom