Tundu Lissu: Ninampinga Magufuli hadharani. Sio mnafiki na sijahongwa

Mtu mwenyewe anaitwa tundu, sasa unategemea nini toka kwa tundu?
 
Kwahiyo mmeridhika bila maelezo yoyote!Tuambiwe tuna wadai Usd bil 190,halafu tupewe usd ml 300 yaani chini ya 0.2% ya kile tunachodai halafu mchekelee na kuona ni sawa bila hata maelezo ya aliyekuja kwa mbwembwe kutambia tunadai $bil 190!!!!!Mtakuwa na matatizo ya akili!
Hakafu ni nani aliyeingia mikataba mibovu?Wakati akina Lissu na Zitto wakipiga kelele kulinda rasilimali zetu,CCM akiwemo JPM walikuwa busy kupitisha mikataba kwa hati ya dharura!
Zitto ilifika kipindi alifukuzwa bungeni kwa miezi minne kwa sakata la mrabaha kwenye madini wakati huo ameibua suala la Buzwagi!Lissu alipigwa na kukamatwa na polisi akiwatetea wananchi waliokuwa wamedhulumiwa haki zao na waawekezaji mgodi wa North mara!
Nchi hii wakubeba lawama ni CCM na si mwingine kwa hapa tulipo!
Acha kupuyanga sasa mkuu, nimekuuliza hapo juu aliye ziibua hizo usd bil 190 ambazo wewe leo unazidai alikuwa nani na hadi negotiation kufanyika hadi kupewa hizo unazoita mil 300 ni nani alisababisha?

Kwahiyo kwasababu Lissu alipinga mikataba mwanzo hadi kupigwa na polisi ndio sasa inatoa kibali kwake kupinga mabadiliko yoyote ya hiyo mikataba?
Mwanzo alitetea wananchi kwasababu mikataba mibuvu kwanini sasa inapofanyika juhudi ya kutaka kuirekebisha ageuke na kuwatete wazungu au kwamba ndio analipa kisasi kwa serikali kwa sababu ya kupigwa?

Kama Magufuli alikuwemo wakati mikataba inapitishwa hicho ndio kinamuondolea haki ya yeye kujaribu kurekebisha kwa kipindi chake na nafasi yake?
 
Kati ya Lissu na JPM,ni nani anawalinda Barrick?Inakuwaje kati ya usd bil 190 tuambulie dola mil 300 na JPM akubali?
Else Lissu alikuwa sahihi!
Huna ujualo wewee
Sera za lisu za corona ipo TZ naona zimeisha sasa,hata yeye anafurahia mikusanyiko ya watu na mafuriko ya watu Tena Bila Tahadhari.
Mkiambiwa Rais JPM anachosema Ana maanisha mnapinga ili tu muonekane mmeenda against.
 
Acha kupuyanga sasa mkuu, nimekuuliza hapo juu aliye ziibua hizo usd bil 190 ambazo wewe leo unazidai alikuwa nani na hadi negotiation kufanyika hadi kupewa hizo unazoita mil 300 ni nani alisababisha?

Kwahiyo kwasababu Lissu alipinga mikataba mwanzo hadi kupigwa na polisi ndio sasa inatoa kibali kwake kupinga mabadiliko yoyote ya hiyo mikataba?
Mwanzo alitetea wananchi kwasababu mikataba mibuvu kwanini sasa inapofanyika juhudi ya kutaka kuirekebisha ageuke na kuwatete wazungu au kwamba ndio analipa kisasi kwa serikali kwa sababu ya kupigwa?

Kama Magufuli alikuwemo wakati mikataba inapitishwa hicho ndio kinamuondolea haki ya yeye kujaribu kurekebisha kwa kipindi chake na nafasi yake?
Lissu bado yuko upande wa wananchi na hajawahi kuyumba katika hilo!Zaidi ya yote ni mwanasheria ambaye anajua mikataba mliyojifunga nayo ni vigumu kuruka!Uwazi wake ndio mnauchukulia kama usaliti wakati ndicho kilichotokea!Hayo mabilioni ya dola yako wapi au zilikuwa kiki za kisiasa?
Magufuli anafanya makosa yaleyale waliyofanya watangulizi wake,usiri kwenye mikataba bado ni mkubwa!Tena kwa sasa hakuna uwazi kwenye uendeshaji wa serikali!
 
Naomba majibu ya hili swali Hadi leo sijapata.

Kwa nini Lissu alikiwa anawetetea Sana Barick na kutishia kwamba tutashitakiwa? Alikuwa na nia ya dhati kweli ama alikiwa anatetea ulaji wake tu? Ama ilikuwa sehemu ya Siasa kwamba ukiwa upinzani lazima upinge kila Jambo?

Nikijibiwa nikaelewa basi kura yangu kwake.
Hili swali ni gumu mno kwa cdm. Utaambulia matusi na kejeli lakini wa kukujibu hakuna.
Lissu alikua anatumiwa na mabeberu na pale alikua kazini kuwatetea mabeberu harafu leo anautaka urais. Nitapiga kampeni chumba kwa chumba kumtetea Magufuli.
 
Huna ujualo wewee
Sera za lisu za corona ipo TZ naona zimeisha sasa,hata yeye anafurahia mikusanyiko ya watu na mafuriko ya watu Tena Bila Tahadhari.
Mkiambiwa Rais JPM anachosema Ana maanisha mnapinga ili tu muonekane mmeenda against.
Lissu akienda kenya anasema tz ina corona. Huyu jamaa ni tapeli sana.
 
Kwa sababu yeye ni Wakili,

Hata mawakili wa serikali huwa wanawatetea wauaji.
Kama ni mahakamani sawa. Unamtetea mtu unayemuwakilisha. Lakini Tundu Lissu alikuwa akizungumzia Bungeni ambamo alitakiwa atetee maslahi ya Taifa. Siku za nyuma nilizungumzia Lissu akilalama Bungeni kwamba kufuatana na mkataba ulioingiwa na Uingereza kabla ya uhuru wa Tanganyika, ziwa Nyasa lote ni la Malawi. Alikuwa akikomaa kabisa kwamba mikataba lazima iheshimiwe, sawa na vile alikuwa akikomalia mchanga wa makinikia kwamba kwa kuwa kuna mkataba lazima tuendelee hivyo hivyo. Magufuli akapinga hilo na mazungumzo yakafanyika kwa manufaa yetu. Mfano wa tatu ni ule wa maji ya ziwa Victoria ambao nao alikuwa akikomalia mkataba ulioingiwa kati ya Misri na Muingereza wakati anatutawala. Mkataba ulikuwa ukitukataza sisi tusiyachukue maji Ziwa Victoria kuyapeleka Dodoma. Yaani sasa tuumie ili Misri isidhurike. Magufuli akapinga upumbavu huo na sasa maji ya ziwa Victoria yamefika Shinyanga na Tabora. Kesho na keshokutwa yatakuwa yamefika Dodoma. Ni dhahiri kwamba tukikosea tumpe mtu huyu kutuongoza, nchi itauzwa kwa misingi kwamba kuna mikataba, badala ya kusema tuipitie upya mikataba mibovu iliyoingiwa kama afanyavyo Magufuli. Hakuna mantiki jinsi anavyoutumia ujuzi wake wa sheria kuliumiza Taifa.
 
We ni miongoni wa wale walomuamini lisu eeeh.

Punguza unyumbu brother,next time utatumbukizwa shimoni ujue Kama hujui lolote ndani ya nchi hii.

Utakua Katika kundi linaloamini Lissu ndo Rais wako baada ya 28/10.
Bila Shaka atakua Rais wa nyumbu
Yote uliyoandika hapa ni ujinga!
 
The super man....
1599681106311~2.jpeg
 
Lissu bado yuko upande wa wananchi na hajawahi kuyumba katika hilo!Zaidi ya yote ni mwanasheria ambaye anajua mikataba mliyojifunga nayo ni vigumu kuruka!Uwazi wake ndio mnauchukulia kama usaliti wakati ndicho kilichotokea!Hayo mabilioni ya dola yako wapi au zilikuwa kiki za kisiasa?
Magufuli anafanya makosa yaleyale waliyofanya watangulizi wake,usiri kwenye mikataba bado ni mkubwa!Tena kwa sasa hakuna uwazi kwenye uendeshaji wa serikali!
Sasa mkuu mh Tundu Lissu kwenye hilo sakata la madini alikuwa upande wa wananchi wepi wakati alimkataza Magufuli asifanye mabadiliko yoyote kwenye mikataba kwamba atashitakiwa MIGA na tutawalipa mabilioni? Au unadhani kwamba tumesahau mkuu, hebu nambia hapa alikuwa upande wa mwananchi yupi?

Narudia tena kukuliza hayo mabilioni ya dola unayo yazungumzia leo hii na hizo unazoita mil 300, ambazo kwa maoni yako ni kiki za kisiasa nani kaziibua?

Kufanya makosa yale yale ni jambo moja na kufanya marekebisho ya mikataba ni jambo la pili, nikakuuliza swali uwepo wa Magufuli bungeni wakati hiyo mikata inapitishwa unamuondolea haki yeye kufanya mabadiliko kwenye kipindi chake?

Uwazi upi wa mikataba ya madini unao uzungumzia Kaka, mbona hata humu JF hiyo mikataba ipo na tumeijadili Sana humu na kina mhe Zitto Kabwe na kina Pascall waliileta humu labda wewe ndio ambaye hukutaka kujua mkuu.
 
Kwa sababu yeye ni Wakili,

Hata mawakili wa serikali huwa wanawatetea wauaji.
Hapo ndipo huwa mnakosea. Mawakili kazi yao ni kuisaidia mahakama kutoa maamuzi yaliyo ya haki. Mawakili kazi yao siyo kutetea wahalifu. Kazi yao ni kuichambua sheria inayodaiwa kuvunjwa ili mahakama ione kama uvunjaji huo umethibitishwa beyond reasonable doubts. Wakili wa upande wa mhalifu (utetezi) kazi yake ni kuibua hizo reasonable doubts. Wakili wa upande wa mashitaka ni kutetea hizo reasonable doubts zilizoibuliwa na upande wa utetezi kuwa haziko reasonable. Baada ya hapo hakimu ndiye mwenye kuamua kama ziko reasonable au la.

Tunduli Lissu hakufanya hivyo kwa Barrick kwani Barrick wala haikuwa na kesi yo yote mahakamani kwetu. Yeye alikuwa anapayuka tu mitaani na kwenye mitandao, kitu ambacho si kazi ya wakili na ni ukiukaji wa maadili ya mawakili wa mahakama, kinyume na kiapo cha mawakili. Alipaswa kuwa ameshafutwa kwenye daftari la mawakili wa mahakama za Tanzania kama alivyofutwa huyo Fatuma Karuma kwa uropokaji wa aina hiyo. Uchaguzi mkuu utakapoisha lazima atafutwa kwenye daftari la mawakili. Hata akishinda urais (something impossible) atafutwa kwani huwezi ukawa rais wa nchi na ukaendelea kuwa wakili wa mahakama. Akishindwa urais (100% posibility) bado atafutwa uwakili kwani yote aliyoyasema katika kampeni zake yanamuondolea sifa ya kuendelea na kazi ya uwakili wa mahakama. Lazima tutamfuta. Haiwezekani mtu ambaye alikuwa mgombea wa urais akawa wakili wa mahakama.

Kwa hiyo baada ya 28 Oktoba 2020 Tundu Lissu ajiandae kwenda kwao Ikungwi kuwa mkulima wa nyanya au kurudi uhamiaji kwake Ubeligiji. Akirudi Ubelgiji mwaka 2025 hatutakubali tena awe mgombea urais wetu.
 
Sasa mkuu mh Tundu Lissu kwenye hilo sakata la madini alikuwa upande wa wananchi wepi wakati alimkataza Magufuli asifanye mabadiliko yoyote kwenye mikataba kwamba atashitakiwa MIGA na tutawalipa mabilioni? Au unadhani kwamba tumesahau mkuu, hebu nambia hapa alikuwa upande wa mwananchi yupi?

Narudia tena kukuliza hayo mabilioni ya dola unayo yazungumzia leo hii na hizo unazoita mil 300, ambazo kwa maoni yako ni kiki za kisiasa nani kaziibua?

Kufanya makosa yale yale ni jambo moja na kufanya marekebisho ya mikataba ni jambo la pili, nikakuuliza swali uwepo wa Magufuli bungeni wakati hiyo mikata inapitishwa unamuondolea haki yeye kufanya mabadiliko kwenye kipindi chake?

Uwazi upi wa mikataba ya madini unao uzungumzia Kaka, mbona hata humu JF hiyo mikataba ipo na tumeijadili Sana humu na kina mhe Zitto Kabwe na kina Pascall waliileta humu labda wewe ndio ambaye hukutaka kujua mkuu.
1.Niwekee link hapa nione mikataba ya mafuta na gas!
2.Lissu alikuwa anatoa tahadhari za kisheria kwenye hatua tunazotaka kuchukua!JPM sio mjinga kukaa kimya,aliona akiendelea kushika msimamo wake matokeo yake ni kile Lissu alichosema na tungeweza kukamatiwa mali zetu kama alivyofanya yule mkulima kukamata ndege mpaka wameamua kumlipa kisirisiri!
Walikaa na Mzungu na kukubaliana wawalipe Usd mil 300 toka usd bil 190!Kama tuna haki na usd bil 190 na tunao uhalali kisheria,kwanini tukubali usd mil 300?Mwenye akili ataelewa,JPM aliamua kulegeza kamba baada ya kujua Lissu alikuwa sahihi!Akatoka hapo anawaita wazungu ni wanaume na si mabeberu!Wenye akili tukajua mbuzi kafia kwa muuza supu!
3.JPM ni sehemu ya tatizo maana alikuwa kwenye baraza la mawaziri,kujaribu kurekebisha ni sahihi ila asitake kujifanya yeye ni mzalendo hasa kuliko wengine!
 
Ok mpaka hapa tulipo fikia naona kujibu maswali umeshindwa mkuu (unakwepa hoja).

1: Tumehama kutoka mikataba ya madini na sasa umeenda kwenye mafuta na gas ? Huo ni mjadala mwingine hausiki hapa.

2: Ametoa tahadhari za kisheria kwa kuita uchunguzi ni Rubbish huo ndio ushauri wa kisheria? ( Kumbuka kilichokuwa kinaendelea wote tulishuhudia mkuu).
Njia zilizo tumika ni kubadilisha mikataba na kwa Sheria zetu za ndani ndio mana Sheria zilienda bungeni kubadilisha na si vingivyo.

Magufuli hakukaa kimya Ila kilicho fanyika ni negotiation na nadhani team ya wawakilishi wao iliyo kuja uliiona na wote tulishuhudia ( labda unambie kwamba hujui maana ya negotiation kwenye biashara).
We unadhani wale wangekuwa na haki moja kwa moja wangekuja huku kubembeleza win win solution wapoteze mali na muda wao wote huo kizembe namna hiyo? Si wangeenda kushitaki huko MIGA tuwalipe hayo mabilioni?

Sasa hizo propaganda za mkulima kulipwa kimya kimya kama unavyo dai bila ushahidi mimi siwezi kuzijadili mkuu. Ninachojua mimi huyo mkulima alishindwa kesi S.A akaenda Canada akashindwa tena kesi labda wewe ulete ushahidi wa huko kulipwa kwake.
Na siku akikata rufaa kesi ikiendelea sijui utakuja tena kusemaje hapa?

3: Kama kurekebisha ni sahihi basi hakuna haja ya kumshambulia.
Na Kama alichokifanya kinaleta faida kwa asilimia fulani basi ni haki akijisifu mzalendo kuliko wengine walio tia sahihi za hio mikataba pamoja na hawa wanao mtishia kushitakiwa MIGA.
 
1.Report ile ilikuwa Rubbish na ndio maana hata matokeo yake ni Rubbish!Unaitaje win win situation watu unawadai $bil 190 unaambulia chini ya 0.2% yaani $mil 300?
Ni moja kati ya haya mawili,Report ilikuwa rubbish au viongozi wetu ni rubbish kwa kuona 0.2% ni win win situation!
2.Hiyo ya mkulima alichoshindwa ni namna ya kukamata mali ila siyo kesi ya msingi inayompa haki!Taarifa kutoka jikoni kabisa ni kuwa mkulima kashaliowa sehemu kubwa ya anachodai na malipo yaliyobaki ni kidogo!
 
Hivi unataka majibu au una lako jambo? Lissu hakuwa Wakili wa Barrick. Kwanza alikuwa akitaka kumwakilisha yule Mwanyika wa Acacia aliyewekwa ndani kwa uhujumu uchumi na madai ya acacia kukwepa kodi na kwamba ni kampuni ambayo haikusajiliwa.
Acha uongo. Lissu hajawahi kumtaja Mwanyika. Alikuwa nataja Barick. sio kwamba alikuwa anatafuta uteja ili apige pesa?
 
Back
Top Bottom