Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Nitalipa malimbikizo ya wafanyakazi yote kuanzia 2015 - 2020

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Nitalipa malimbikizo ya wafanyakazi yote kuanzia 2015 - 2020

Wewe hujui serikali inaendeshwaje ndiyo maana unafikiri ni kirahisi hivyo eti atawalipa malimbikizo ya wafanyakazi kwa miaka mitano!! Naona hayo maturubai aliyovaa yanampunguzia akili kichwani. Akawadanganye wanafunzi wa chekechea!!
Tz wafanyakaz hawazid 10000 ajira rasmi
 
Hauwezi kuongelea serikali ya Magufuli bila kuongelea ukatili, udikteta, kukosekana uhuru wa vyombo vya habari... Nchi hii si ya wakulima tu. Kuna watu wa haki za binadamu, wafanyabiasha, wafanyakazi... Na wengine basi tu hawapendi uonevu. Magufuli ni katili. Ukatili wake hauwezi fumbiwa macho na watu wote milioni 60 wa nchi hii.
Sasa aya ndio tulitaka kisikia...sasa me mkulima wa kijijini unaanza niambia mambo ya risasi kiunoni.
 
Kuongea ni rahisi ili apate ulaji, kutenda najua itakuwa ziro. Akagombee Ubeligiji huko
 
Huyu anataka turudi kwenye uchumi tegemezi.

Atatoa wapi hela endapo anaivunja TRA?

Haelezei atainuaje uchumi wa nchi bali anaelezea atakavyoharibu mifumo mizuri iliyojengwa
Kwani TRA ndio hela? Badala ya kuwajali walipa kodi wewe unamthamini mkusanya kodi? CCM ni janga katika taifa hili kama mnayo mawazo ya namna hii. Walaaniwe wote wenye mawazo kama yako.
 
Tundu Lissu anasema atalipa malimbikizo yote ya mishahara na kupandisha vyeo vyote vilivyosimama toka mwaka 2015 mpaka leo 2020.

Anasema lazima wafanyakazi walipwe fidia na Serikali yake.

Anasema atawalipa pia fidia wote waliofukuzwa kazi na Serikali ya CCM ndani ya hii miaka 5.

Anasema atarudisha makato ya loan board kutoka 15% na kuwa 3%

Na yatakuwa kwa wale tu watakao kuwa na kazi za kueleweka ndani ya serikali yake.

Anasema atafumua mfumo wa elimu ili utoke kwenye kujibu mithihani na kuwa elimu ya maarifa na kujitegemea na kuajirika kirahisi.

Anasema ataifumua TRA na kuanzisha mfumo wa Kodi moja ili nchi zote zilizo tuzunguka zije kununua bidhaa bandarini na kwenye maduka yetu ya ndani.

View attachment 1552154View attachment 1552155
Kwa ilani hizi tumelamba Dume tupambane tuliondoe JIKONO JANDAMA ikulu.
 
Back
Top Bottom