PostGE2025 Tundu Lissu: No Reforms, No Election ni kauli ya Freeman Mbowe

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Ni wapi na lini Mbowe amekana NRNE?

Amandla...

Timu ya kampeni ya re-election ya Mbowe kwa nafasi ya uenyekiti 99.9 walihama chama baada ya kushindwa walihamia CHAUMMA na wengine ACT na walianza kuishambulia CHADEMA na kuidogosha NRNE wakiongozwa na Yericko Nyerere , pia Mbowe hajawahi kutoka hadharani kuitaja na kuiunga mkono NRNE wakati ni mjumbe wa kudumu wa kamati kuu.

Mikutano ya kuhamasisha NRNE ilipoanza hata Lissu alipokamatwa April 9 iliendelea , Mbowe hajaawahi kuhudhuria mikutano hiyo wala kusema chochote iwe kwa NRNE wala kesi ya kubumba ya mwenyekiti wake ghafla tu tukamuona kaibuka Dodoma kwenye dira ya Samia na kupiga nae picha juu!

Huhitaji hadi hapo kujua msimamo wa Mbowe juu ya NRNE.
 
Timu ya kampeni ya re-election ya Mbowe kwa nafasi ya uenyekiti 99.9 walihama chama baada ya kushindwa walihamia CHAUMMA na wengine ACT
Hawakuhama baada ya Mbowe kushindwa uchaguzi. Baadhi yao kama Catherine Ruge, Sigrada walikubali nafasi ndani ya Chadema ya Lissu. Wanadai walihama baada ya kuona kuwa wanatengwa na hawasikilizwi na uongozi mpya.
na walianza kuishambulia CHADEMA na kuidogosha NRNE wakiongozwa na Yericko Nyerere
Zaidi ya Yericko, niambie kuna kiongozi gani wa Chaumma anayeishambulia Chadema? Ulitegemea waunge mkono NRNE wakati msimamo wao dhidi yake ulichangia sana wao kuondoka Chadema?!!!
, pia Mbowe hajawahi kutoka hadharani kuitaja na kuiunga mkono NRNE wakati ni mjumbe wa kudumu wa kamati kuu.
Kwa nini aitaje na kuiunga mkono hadharani? Angalau yeye hakuzunguka kupinga na kuusemea ovyo msimamo wa chama chake kama alivyofanya Lissu kuhusu Maridhiano.! Inawezekana kuwa hakubaliani na hali ilivyo sasa ndio maana amenyamaza. Hiyo ni haki yake.
Mikutano ya kuhamasisha NRNE ilipoanza hata Lissu alipokamatwa April 9 iliendelea , Mbowe hajaawahi kuhudhuria mikutano hiyo wala kusema chochote iwe kwa NRNE wala kesi ya kubumba ya mwenyekiti wake ghafla tu tukamuona kaibuka Dodoma kwenye dira ya Samia na kupiga nae picha juu!
Mnataka kumlazimisha afanye kitu ambacho yeye hakubaliani nayo? Huo ungekuwa unafiki na kinyume na msimamo wa chama kinacho jiita Chama cha DEMOKRASIA na Maendeleo. Hata Lissu alipiga picha na Samia wakati Mbowe yuko rumande.
Huhitaji hadi hapo kujua msimamo wa Mbowe juu ya NRNE.
Hamna anaejua. Inawezekana kuwa hakukubaliani nao toka mwanzo lakini alikubali uamuzi wa Kamati Kuu kwa maana aliheshimu Demokrasia. Sasa hivi hawajibiki kuunga mkono maana yeye sio sehemu ya uongozi Mkuu wa Chama. Kukaa kwake kimya ni ishara tosha kuwa bado anaheshimu msimamo wa jumla wa chama chake.

Amandla...
 
Hawakuhama baada ya Mbowe kushindwa uchaguzi. Baadhi yao kama Catherine Ruge, Sigrada walikubali nafasi ndani ya Chadema ya Lissu. Wanadai walihama baada ya kuona kuwa wanatengwa na hawasikilizwi na uongozi mpya.

Zaidi ya Yericko, niambie kuna kiongozi gani wa Chaumma anayeishambulia Chadema? Ulitegemea waunge mkono NRNE wakati msimamo wao dhidi yake ulichangia sana wao kuondoka Chadema?!!!

Kwa nini aitaje na kuiunga mkono hadharani? Angalau yeye hakuzunguka kupinga na kuusemea ovyo msimamo wa chama chake kama alivyofanya Lissu kuhusu Maridhiano.! Inawezekana kuwa hakubaliani na hali ilivyo sasa ndio maana amenyamaza. Hiyo ni haki yake.

Mnataka kumlazimisha afanye kitu ambacho yeye hakubaliani nayo? Huo ungekuwa unafiki na kinyume na msimamo wa chama kinacho jiita Chama cha DEMOKRASIA na Maendeleo. Hata Lissu alipiga picha na Samia wakati Mbowe yuko rumande.

Hamna anaejua. Inawezekana kuwa hakukubaliani nao toka mwanzo lakini alikubali uamuzi wa Kamati Kuu kwa maana aliheshimu Demokrasia. Sasa hivi hawajibiki kuunga mkono maana yeye sio sehemu ya uongozi Mkuu wa Chama. Kukaa kwake kimya ni ishara tosha kuwa bado anaheshimu msimamo wa jumla wa chama chake.

Amandla...

Ukinisoma vizuri utaelewa kwamba kwa nafasi aliyokuwa nayo Mbowe kama mwenyekiti aliposhindwa alibaki kama mjumbe wa kudumu wa kamati kuu.

Yeye kama mjumbe wa kamati kuu tangu January 21 , mwaka 2025 umemuona wapi akishiriki shughuli za chama?

Pili kama hashiriki shughuli za chama ana maana gani , je sio mwanachama hai?

Tatu kama hashiriki shughuli za kichama je ana chama kipya kisirisiri?

Nne msimamo wa chama ulikua ni NRNE yeye kama mjumbe wa kamati kuu kukaa kimya maana yake haungi mkono maazimio ya kamati kuu yaliyopitishwa December 2024 yeye akiwa mjumbe wa kamati kuu na mwenyekiti.

Tano , chama kiligoma kuitambua serikali haramu ya Samia [ndio haramu maana unaweza kuunda serikali ila isiwe halali maana imeingia kwa njia zisizo za kidemokrasia] je inakuaje mjumbe wa kamati kuu anashiriki katika shughuli ambazo chama kimezi-boycott?

Mkuu najua unaujua ukweli ila unashindwa kukiri maana wewe na wenzio mliokua team ya Mbowe bado hamjapona maumivu ya kushindwa uchaguzi mimi kwa leo naishia hapa ila nakukumbusha anachokifanya Mbowe hata mtu yoyote mwenye akili timamu anajua Mbowe alikuwa kinyume na maazimio ya chama ya NRNE hasemi waziwazi ila kiutashi unamuona tu kwa kushiriki shughuli hizo mbili za serikali haramu ila mahakamani haendi kutoa support kwa mwenyekiti wake hii si sawa hata kidogo kama kweli aliyoyaongew siku anakubali kushindwa uchaguzi wa wazi na wa kidemokrasia basi asimgejitenga na kukinzana na misimamo hii ya chama.

Ninakupa mfano huu , Uhuru Kenyatta na William Ruto waliunda Jubilee coalition 2016 na wakashinda uchaguzi 2017 .

Baada ya Uhuru kufanya handshake na Raila 2018 , Ruto alianza kuipinga na baadae hata ile BBI ya Uhuru na Odinga Ruto aliipinga waziwazi na hata kuna mikutano kiti cha naibu rais [DP] cha Ruto kilikua kinabaki wazi kwa kutokana na mgomo baridi kutohudhuria vikao baadae watu kuomba afukuzwe ila aliishia kujitoa Jubilee mwenyewe kuelekea uchaguzi wa 2022 na akagombea kupita chama kipya cha UDA alichokianzisha.

Na uchaguzi wa 2022 ilibidi Uhuru amuunge mkono mgombea mwingine ambaye Raila Odinga na sio Ruto aliyeenda kuunda UDA na kugombea baada ya kutoka Jubilee iliwashangaza watu kwamba rais anayemaliza muda wake anamuunga mkono mgombea mwingine na sio naibu wake ambaye aligombea pia.

Hivyo anachokifanya Mbowe wala hakinishangazi na sioni ni kipya.
 
Hilo halina ubishi.
Yeye kama mjumbe wa kamati kuu tangu January 21 , mwaka 2025 umemuona wapi akishiriki shughuli za chama?
Kamati Kuu ina wajumbe wangapi? Je wote wanashiriki kwenye shughuli za Chama? Uliwahi kusikia Mtei akishiriki shughuli za chama? Mara nyingi viongozi waliopita wanakaa pembeni kwa kutotaka kuwa nexus ya watu wanao tofautiana na uongozi uliopo. Wanakaa pembeni maana huu ni wakati wa washindi kuonyesha umahiri wao. Wakitaka kumshirikisha watamkaribisha, lakini hata siku moja hawezi kujipeleka. Tuambie kama kuna siku uongozi wa chama chake wamesema kuwa walimualika akakataa. Mbowe alisimangwa hata wakati wa msiba wa Mkwe wake. Wakina Hilda walijaza airwaves wakimshutumu kuwa alikuwa na nia ya kukabidhi shughuli nzima kwa CCM na serikali yake! Mimi binafsi ningependa kujua Chadema walichangia kiasi gani kwenye msiba wa Mtei.
Pili kama hashiriki shughuli za chama ana maana gani , je sio mwanachama hai?
Ukisikia ni mjumbe wa Kamati Kuu wa kudumu ina maana kuwa yeye siku zote ni mwanachama hai.
Tatu kama hashiriki shughuli za kichama je ana chama kipya kisirisiri?
Sio lazima ujue ana shiriki vipi katika shughuli za chama chake. Nakumbuka kuwa alichangia Mkutano mmoja wa Bawacha. Sigrida alipomshukuru kwa mchango wake mbele ya Lissu alishambuliwa sana na hao waliojiona kuwa sasa Chadema ni yao. Yeye ni mwanachama kama walivyo mamilioni ya wanachama wenzake. Aliaga kuwa atatjikita zaidi kwenye mambo ya biashara na ndivyo anavyo fanya. Mbowe aliongoza CDM kwa zaidi ya miaka 2o lakini mwisho wa siku akalaumiwa na kuitwa msaliti wa Chama. Hilo hilo linaweza kutokea akijitokeza zaidi kwenye shughuli za chama. Mtasema kuwa amepewa pesa na wakina Abduli kukihujumu chama. Na angelaumiwa kwa yote ambayo anapitia Mwenyekiti wake. Mbowe angeanzisha chama kipya ingejulikana tu.
Nne msimamo wa chama ulikua ni NRNE yeye kama mjumbe wa kamati kuu kukaa kimya maana yake haungi mkono maazimio ya kamati kuu yaliyopitishwa December 2024 yeye akiwa mjumbe wa kamati kuu na mwenyekiti.
Sio lazima aunge mkono maazimio yote ya Kamati Kuu. Kilicho muhimu ni kuwa haendeshi kampeni ya kuyapinga kama alivyofanya Lissu kwenye suala la maridhiano.
Tano , chama kiligoma kuitambua serikali haramu ya Samia [ndio haramu maana unaweza kuunda serikali ila isiwe halali maana imeingia kwa njia zisizo za kidemokrasia] je inakuaje mjumbe wa kamati kuu anashiriki katika shughuli ambazo chama kimezi-boycott?
Niambie wapi CDM imetangaza ku boycott shughuli zote za serikali. Chadema haikuanza leo kutotambua serikali iliyokuwepo. Kama kuna hilo agizo, CDM wana uwezo kabisa wa kumuadabisha. Mbona hawafanyi hivyo?
Mkuu najua unaujua ukweli ila unashindwa kukiri maana wewe na wenzio mliokua team ya Mbowe bado hamjapona maumivu ya kushindwa uchaguzi mimi kwa leo naishia hapa ila nakukumbusha anachokifanya Mbowe hata mtu yoyote mwenye akili timamu anajua Mbowe alikuwa kinyume na maazimio ya chama ya NRNE hasemi waziwazi ila kiutashi unamuona tu kwa kushiriki shughuli hizo mbili za serikali haramu ila mahakamani haendi kutoa support kwa mwenyekiti wake hii si sawa hata kidogo kama kweli aliyoyaongew siku anakubali kushindwa uchaguzi wa wazi na wa kidemokrasia basi asimgejitenga na kukinzana na misimamo hii ya chama.
Hizo ni ndoto. Mbowe amekubali mualiko kama kiongozi wa jamii. Kwa nini mnaumia sana na Mbowe kutokwenda Mahakamani? Mnashangaa nini wakati humu hamuachi kumuandama kwa matusi? Mpaka sasa hivi hamjaweza kueleza kesi ya Lissu itafaidika nini na Mbowe kuwepo Mahakamani. Huo mnaoita kuwa uchaguzi wa haki na wazi usingefanyika asingekiwezesha chama chake. Na sekretarieti yake ya wakina Mnyika, Mrema, Kigaila ndio ilisimamia uchaguzi wote. Walihakikisha kuwa unakuwa wa haki pamoja na shutuma za upande wa pili kuwa walikuwa na mpango wa kuuhujumu.
Ninakupa mfano huu , Uhuru Kenyatta na William Ruto waliunda Jubilee coalition 2016 na wakashinda uchaguzi 2017 .

Baada ya Uhuru kufanya handshake na Raila 2018 , Ruto alianza kuipinga na baadae hata ile BBI ya Uhuru na Odinga Ruto aliipinga waziwazi na hata kuna mikutano kiti cha naibu rais [DP] cha Ruto kilikua kinabaki wazi kwa kutokana na mgomo baridi kutohudhuria vikao baadae watu kuomba afukuzwe ila aliishia kujitoa Jubilee mwenyewe kuelekea uchaguzi wa 2022 na akagombea kupita chama kipya cha UDA alichokianzisha.
Huu mfano una husiana vipi na yanayoendelea ndani ya Chadema? Kwani Ruto alifukuzwa? Huyo Ruto unayemtolea mfano, amesema jana kuwa baada ya kushinda uchaguzi alimfuata Kenyatta Ichaweri kujaribu kumshawishi amsaidie katika kutunga vision mpya ya nchi yao. Alimfuata pia mpaka ofisini kwake. Niambie lini Lissu alimfuata Mbowe kumuonyesha kuwa ana nafasi bado katika chama chake na mchano wake ni muhimu na unaheshimiwa na CDM? Hapa, the onus ilikuwa kwa mshindi kumshirikisha aliyemshinda. Mbowe ni muasisi wa CDM na hawezi kukiacha.
Na uchaguzi wa 2022 ilibidi Uhuru amuunge mkono mgombea mwingine ambaye Raila Odinga na sio Ruto aliyeenda kuunda UDA na kugombea baada ya kutoka Jubilee iliwashangaza watu kwamba rais anayemaliza muda wake anamuunga mkono mgombea mwingine na sio naibu wake ambaye aligombea pia.

Hivyo anachokifanya Mbowe wala hakinishangazi na sioni ni kipya.
Ukweli hapa umeniacha kapa. Sielewi point yako.

Amandla...
 
Back
Top Bottom