Sasa tunapigania kipi hapo, Tume huru au Uhuru wenyewe?? Hivi hiyo tume huru huchukua siku ngapi kupatikana?? Wiki? Mwezi? Mwaka? Maana nadhani siku zimekwisha hakuna tena muda wa kuipata.
Miaka mingine 5 ya mkulu nadhani nchi itakuwa ishanyooka hadi kupinda
Uhuru ni neno pana, inategemea unataka kumaanisha nini! Uhuru wa Tanganyika (Tanzania) ulipatikana mwaka 1961. Kabla ya hapo Tanganyika ilitawaliwa kimabavu na wakoloni, ambao ni Wajerumani na baadaye waingereza!
Swali je, ndani ya Tanzania huru wananchi wake wanaishi kwa uhuru kama walivyokubaliana katika Katiba na sheria walizojiwekea!? Uhuru wa kutoa maoni, uhuru wa kupata na kutoa habari, uhuru wa kuabudu, uhuru wa kuchagua na kuchaguliwa katika chaguzi n.k!
Pia uhuru tunaungalia katika vyombo vya kusimamia na kutoa haki, mfano mihimili ya Mahakama na Bunge inafanyakazi kwa uhuru kama katiba,sheria na kanuni zake zinavyotaka!?
Hapa ndipo suala la Tume ya Uchaguzi inakuja! Kwa kuwa uchaguzi unahusisha wadau mbalimbali, wenye misimamo tofauti ambao kazi yao nikuwashawishi wananchi ili wawachague ili wawe viongozi wao, swali ni je, viongozi Tume wanapatikanaje, wanaaminika na wananchi kuwa wanaweza kusimamia chaguzi bila upendeleo!?
Kwa asili binadamu ni mbinafsi na ni mchoyo (selfish and greedy), ndiyo maana unasikia kauli kuwa, "haiwezekani nikuteue na mshahara nikulipe halafu umtangaze mpinzani". Kwa maana nyingine kiongozi anayetoa kauli hiyo, anawaamrisha wampendelee hata kama wananchi wanaona hafai kuemdelea kuwaongoza!
Je muda ni mfupi haitoshi kuwa na tume huru!? Hapana, kwani inachukua mda gani kubadili shetia na kanuni ili kukidhi madai ya Tume huru!? Tatizo ni hofu ya walio madarakanani, kuwa wakiridhia mchakatato wa uchaguzi uwe wa wazi, yawezekana wakatupwa nje ya uongozi wa nchi! Na kwa wanasiasa hiyo ndiyo ajira yao!
Kwa hiyo, Tume isiyo huru ni nyenzo ya kuwarejesha madarakani viongozi tulio nao hata kama hawakubaliki! Hii ni hulka ya asili ya wanadamu ya ubinafsi na uchoyo ambayo viongozi wengi wameshindwa kuidhibiti hata hufikia kuwa wakatili wa kutisha dhidi ya wanadamu wengine ili waendelee kusalia madarakani!
Wasalimie!