Tundu Lissu: Salamu za sikukuu ya Noeli na Mwaka Mpya kwa wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)

Tundu Lissu: Salamu za sikukuu ya Noeli na Mwaka Mpya kwa wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)

Kwa wewe Technicallly, pumba tupu, yeye akae angojee pesa za wakimbizi tu huko Belgiam. Yaani siku hizi amekuwa lofa wa kutegemea wale wale aliokuwa anawalaumu kwamba wanafanya ubadhirifu wa pesa za Watanzania kwa kutumiwa. Lakini yeye TL hatumiwi. Aendelee kuota jonzi tu.

Hapa naona furushi la maneno ya kipuuzi.
 
Naomba kuelimisha maana ya MB, kwa jinsi ninavyojua mimi nadhani MB ni mbuge, na Lisssu nowadays is not mbuge

Sisi tuliompigia kura tunajua bado ni mbunge wetu. Huyo mliyempa ubunge hatujamchagua sisi wananchi.
 
Salaam safi kabisa hizo ndugu yetu Tundu Lissu.

Mungu aendelee kukuongoza na kukusizishia akili, werevu na busara!

Adui anatapatapa, amejaa kiu ya damu! Inampofusha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa kiasi kikubwa na katika maeneo mengi, viongozi wa Chama wa ngazi mbali mbali walikuwa wa kuteuliwa au kuteuana, hata kwa nafasi ambazo, kikatiba, zilikuwa ni nafasi za kuchaguliwa.

Ilibidi iwe hivyo kwa sababu, katika maeneo mengi, hatukuwa na wanachama wenye sifa za, au utayari wa, kuwa viongozi wa Chama. Kama mnavyofahamu, sehemu kubwa sana ya viongozi na watendaji wa Chama chetu wanafanya kazi zao kwa kujitolea, bila kutegemea malipo ya mshahara au posho yoyote.
Kumbe unatambua kwamba sometimes as a society inatakiwa kufanyika maamuzi magumu ata ambayo yanaweza yasionekane ni ya kidemokrasia Kwa mustakabali mzuri Kwa jamii.. Panua huo wigo wako wa uelewa Hadi kwenye uongozi wa Nchi..maybe mechanism hiyo hiyo utumiwa na vyombo vyetu nyeti na NEC katika kufanya Mambo.
 
Nawapongeza Chadema kutimiza miaka 27 katika ulingo wa siasa za Tanzania.

Lakini najaribi kufikiria 2015 Chadema ilitaka kupewa ridhaa ya kuongoza Tanzania bila ya kuwa na uwakilishi wa nchi nzima. Mh. Lissu anathibitisha hapa kwa kusema chama kilikuwa hakina watu wenye sifa za kichagulia, ndio maana waliishia kuteuwana tu. Ni bora Lissu ametupa picha halisi la ndani ya Chadema, huwezi kushida uchaguzi wa Tanzania kama huna uwakilishi wa kila kona nchi zima.
Kujionesha kuwa mpinzani TZ yahitaji ujasiri ndugu. Usione madai eti CCM ina wanachama wengi ni maslahi tu na uoga.

Fikiria itokee CCM iwe chama cha upinzani. Watu watahama hutaamini.

Na CCM imetengeneza mazingira mengi tu ya kulazimisha wanachama. Sihitaji kufafanua hapa lakini huku mitaani na vitongojini tunakutana nayo kila siku.

Na watanzania wengi wanakwambia yanini misukosuko, bora nakula ugali na watoto wangu. Wanajua na wanashuhudia wapinzani wanapopata misukosuko. Ni kete nzuri kwa CCM na balaa kwa upinzani.

Usalama wa CCM ni kuendelea kukalia usukani milele vinginevyo wakiteleza tu, haohao wanao pepea matawi ya miti na kanga sasa watadai marekebisho katika daftari la usajili wa vyama.

Kutegemea siku moja upinzani uwe na mizizi kila eneo kama CCM ni ndoto na hasa kwasababu CCM haitaruhusu hilo.

Ukipita vijijini utaona majengo mengi yana chata za CCM ukiuliza vizuri hata wana CCM wa hapo mahali wanakwambia ni uporaji tu. Leo watu wapo kimya sababu CCM ina nguvu kupitia dola na wa TZ kwa asili sio wakorofi. Isitokee CCM ikawa upinzani itakuwa shida.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom