Tundu Lissu samehe, Shukuru Mungu upo hai

Fundi Madirisha

Senior Member
Joined
Jun 30, 2020
Posts
184
Reaction score
988
Mhe Lissu tunajua kabisa kuwa waliokuumiza wako ndani ya Ardhi ya Tanzania hata kama hawapo hai.

Samehe ilimradi wewe ni mzima na Mungu anakulinda kwa gharama zake yeye.

Ulipigwa Risasi, Ukanyimwa pesa za matibabu, ulinyimwa mshahara, Ukanyimwa ubunge wako, Ulinyimwa uhuru wa kuishi nchini mwako,Ukanyimwa na mafao yako.

Kwa hakika Spika Ndugai ameshiriki ubaya huu na ninamtaja moja kwa moja kwa sababu alishiriki kukunyima stahiki zako. Mungu atamwadhibu kwa fimbo yake, wengine wasiojulikana Mungu atabeba roho zao moja baada ya mwingine na kwa ghadhabu kali.

Wewe samehe yote yaliyokukuta. Dua zetu zote bado ziko kwako Mungu anakulinda kwa mapenzi makubwa.
 
Lisu anataka aingie madarakani alipe kisasi cha kuwapiga watu shaba,na hii ni sera yetu kama chama VISASI
 
Ndu-guy atakuwa anafahamu A to Z.
Part aliyoshiriki kwa nafasi yake itamgharimu sana,Mwendazake cha mtoto.
 
Ndugai naye aadhibiwe kwa style ile ile ya March 17.
 
Magufuli tayari keshapata adhabu yake bado akina Ndugai, Makonda, Mambosasa, Mroto, Heri etc.
 
Mhe Lissu tunajua kabisa kuwa waliokuumiza wako ndani ya Ardhi ya Tanzania hata kama hawapo hai.

Samehe ilimradi wewe ni mzima na Mungu anakulinda kwa gharama zake yeye.

Ulipigwa Risasi, Ukanyimwa pesa za matibabu, ulinyimwa mshahara, Ukanyimwa ubunge wako, Ulinyimwa uhuru wa kuishi nchini mwako,Ukanyimwa na mafao yako.

Kwa hakika Spika Ndugai ameshiriki ubaya huu na ninamtaja moja kwa moja kwa sababu alishiriki kukunyima stahiki zako. Mungu atamwadhibu kwa fimbo yake, wengine wasiojulikana Mungu atabeba roho zao moja baada ya mwingine na kwa ghadhabu kali.

Wewe samehe yote yaliyokukuta. Dua zetu zote bado ziko kwako Mungu anakulinda kwa mapenzi makubwa.
Amina, Ila Watanzania na dunia haitosau unyama huu.
 
Mkuu, Lissu atakuwa kashasamehe yote, ila ambacho kila binadamu huwa analilia ni Justice.. akiwa bado hai anataka ajue ni kina nani wale waliojiunga na kuamua kumfanyia kitu kama hicho, kwamba asiishi duniani kabisa, je kwa nini na kwa kosa lipi hasa?

Serikali ikiamua inaweza kuwapata wote mara moja ni suala la uamuzi tu - hilo ndilo Lissu analowaomba watawala mara kwa mara, na sisi watanzania tunataka kujua pia ni kina nani na walipata udhubutu au mamlaka hayo kutoka wapi.
 
Back
Top Bottom