Tundu Lissu samehe, Shukuru Mungu upo hai

Mhe Lissu tunajua kabisa kuwa waliokuumiza wako ndani ya Ardhi ya Tanzania hata kama hawapo hai.

Samehe ilimradi wewe ni mzima na Mungu anakulinda kwa gharama zake yeye.

Ulipigwa Risasi, Ukanyimwa pesa za matibabu, ulinyimwa mshahara, Ukanyimwa ubunge wako, Ulinyimwa uhuru wa kuishi nchini mwako,Ukanyimwa na mafao yako.

Kwa hakika Spika Ndugai ameshiriki ubaya huu na ninamtaja moja kwa moja kwa sababu alishiriki kukunyima stahiki zako. Mungu atamwadhibu kwa fimbo yake, wengine wasiojulikana Mungu atabeba roho zao moja baada ya mwingine na kwa ghadhabu kali.

Wewe samehe yote yaliyokukuta. Dua zetu zote bado ziko kwako Mungu anakulinda kwa mapenzi makubwa.
Aliyeagiza apigwe yeye ndiyo anaoza vizuri
 
Mkuu, Lissu atakuwa kashasamehe yote, ila ambacho kila binadamu huwa analilia ni Justice.. akiwa bado hai anataka ajue ni kina nani wale waliojiunga na kuamua kumfanyia kitu kama hicho, kwamba asiishi duniani kabisa, je kwa nini na kwa kosa lipi hasa?

Serikali ikiamua inaweza kuwapata wote mara moja ni suala la uamuzi tu - hilo ndilo Lissu analowaomba watawala mara kwa mara, na sisi watanzania tunataka kujua pia ni kina nani na walipata udhubutu au mamlaka hayo kutoka wapi.
Makonda na Ndugai hilo lipo wazi
 
Mhe Lissu tunajua kabisa kuwa waliokuumiza wako ndani ya Ardhi ya Tanzania hata kama hawapo hai.

Samehe ilimradi wewe ni mzima na Mungu anakulinda kwa gharama zake yeye.

Ulipigwa Risasi, Ukanyimwa pesa za matibabu, ulinyimwa mshahara, Ukanyimwa ubunge wako, Ulinyimwa uhuru wa kuishi nchini mwako,Ukanyimwa na mafao yako.

Kwa hakika Spika Ndugai ameshiriki ubaya huu na ninamtaja moja kwa moja kwa sababu alishiriki kukunyima stahiki zako. Mungu atamwadhibu kwa fimbo yake, wengine wasiojulikana Mungu atabeba roho zao moja baada ya mwingine na kwa ghadhabu kali.

Wewe samehe yote yaliyokukuta. Dua zetu zote bado ziko kwako Mungu anakulinda kwa mapenzi makubwa.
Mkuu wa wasiojulikana Yuko burigi kazungushiwa mabati
 
Magufuli tayari keshapata adhabu yake bado akina Ndugai, Makonda, Mambosasa, Mroto, Heri etc.
Usiwahusishe watu bila ushahidi. Mateso ya Lisu ni matokeo ya maisha aloishi. Mungu atamlipia kama kuna ubaya wa watu juu yake na wote walotenda Mungu ndo anajua lakini kutaja watu hapa haipendezi.Kinachonifurahisha kwa Lisu ni mtu mwenye furaha hata alipokuja sote tulimuona bila shaka uso wake unaonesha alivyo ndani yake.
 
Kusamehe kuendane na kulipa gharama za matibabu,kuwajibisha wahusika na kumlipa mafao yake ya Ubunge
 
Usiwahusishe watu bila ushahidi. Mateso ya Lisu ni matokeo ya maisha aloishi. Mungu atamlipia kama kuna ubaya wa watu juu yake na wote walotenda Mungu ndo anajua lakini kutaja watu hapa haipendezi.Kinachonifurahisha kwa Lisu ni mtu mwenye furaha hata alipokuja sote tulimuona bila shaka uso wake unaonesha alivyo ndani yake.
Ingekuwa ni wewe ndiye mhusika sasa hivi ungekuwa gerezani lakini kwa kuwa ni hao niliowataja ndio maana hata uchunguzi tu wa uongo na kweli hamna ila Mungu analipa.
 
Back
Top Bottom