Ukweli sisi unaotupigania hatujui tunataka nini , wengi wetu ni keyboard warriors tunahamasishana mitandaoni . Lakini on the ground , wengi wetu ni watumwa wa huu mfumo wa fisiemu .Tunakukumbuka Siku za kesi pekee, lakini shauri likihairishwa tunarudi kujifungia kwenye vibanda vyetu kuendelea na maisha huku wewe ukiendelea kuteseka.
Mkuu sisi hatustahili kuwa na wewe kama mtetezi wetu, sisi ni mbumbumbu , na kwa hakika huenda ungekuwa unatoka katika moja ya nchi dume Hadi Leo tunavyoongea , ungekuwa umeshafanikisha malengo yako yakuwapatia wananchi uhuru wao wa maoni na Haki ya kuishi bila hofu.
Nakusihi muheshimiwa , Mungu atakapokuvusha katika jaribu hili gumu , na utakapokuwa huru hachana na harakati zakutupigania sisi wajinga .Nenda katunze wanao wenye bahati ya kuwa na baba Bora , nenda katunze mkeo mh. Hacha sisi wanafiki waoga ,maisha yatunyooshe , hacha maji tuite mma , hacha fisiemu watukamue mpaka makende.