Sikubaliani na wewe kabisa. Naona unataka kumuangushia jumba bovu Lissu. Yani serikali ya CCM ikope halafu lawama apewe Lissu.
1. Hivi ulishawahi kujiuliza Lissu alifikaje ubelgiji?. Lissu alienda ubelgiji kwa matibabu baada ya kupigwa risasi. Alipigwa risasi kwenye nchi yake ili afe Mungu akamponya Leo unaleta stories kana kwamba Lissu alikimbia ubelgiji akiwa mzima. Hilo ulizungumzi Bali unazungumza kana kwamba Lissu alienda ubelgiji kwa matembezi wakati alienda akiwa mgonjwa.
2. Kuhusu mabalozi kuhudhuria kesi ya Mh Mbowe. Unatakiwa ujiulize ni nani aliyefungua kesi ya ugaidi na kwa lengo gani?. Juzi hapa kulikuwa na kelele za mbowe aombe msamaha kwa Rais, ili asamehewe lakini wapi?. Mabalozi kuhudhuria kesi Ni kujiridhisha na madai ya ugaidi Kama Ni kweli au la. Maana kuhudhuria kwao kesi hakubadilishi maamuzi ya mahakama.
3. Umedai EU wanataka kuihujumu Tanzania. Lakini je unafahamu EU Ni mdau mkubwa wa maendeleo wa Tanzania. Mikopo mingine na misaada mingi tumepata kutoka EU. Swali langu ni kwamba Kama EU analengo la kutuhujumu kwanini tunakopa kwao au kupokea misaada kutoka kwao.
4. Wewe binafsi unadai kuna shida kwenye mradi wa umeme wa Julius Nyerere kwamba hatujafanya upembuzi wa utoshelevu wa maji kwenye mto rufiji, na kwamba hakuna uhakika was maji kutoka milele. Lakini unakuja Tena na kudai nchi za ujerumani na ubelgiji zinatataka kuhujumu mradi wa umeme. Mkopo wa kujenga huo mradi unajua unatoka wapi? Ukijua usingesema unachosema.
5. Kuhusu Lissu kusindikizwa na balozi wa ujerumani uwanja wa ndege. Lazima utambue Lissu aliyopitia hapa nchini. Kwanza kapigwa risasi, pili kanyimwa matibabu, tatu kaondolewa kwenye ubunge , nne kufanyiwa vitimbi alipogombea urais wa Tanzania na tano polisi kugoma kufanya upelelezi wa jaribio la kumuua mpaka leo. Hivi ukiwa katika mazingira hayo Ni wapi salama pa kukimbilia?. Nyumbani kwenu hawakutaki kwanini usikimbilie kwa jirani. Lissu angekuwa hajafanyiwa yote matano Hapo juu na akakimbilia ubalozi wa ujerumani hata Mimi ningeshangaa.
6. Halafu mwisho, unadai serikali ya ubelgiji pamoja na ujerumani wanataka waifanye Tanzania Kama Congo. Unadai Wanataka kumuweka Lissu madarakani ili azuie miradi isiendelee. Naomba ujue kwamba serikali huwa Ina mpango ya miaka mitano, na mipango hii upitishwa na Bunge. Rais hawezi kutoka alikotoka akazuia mpango wa Taifa. Pia Tanzania haipati Rais kutoka jalalani, Bali kuna mfumo halali wa kumpata Rais ingawa saa zingine una madhaifu. Pia Kongo ni tofauti na Tanzania maana hakuna Vita vya wenyewe kwa wenyewe na system ya kuendesha nchi Ni tofauti.
Naomba nitoe ushauri, kwa Sasa vyombo vyote vya maamuzi vipo asilimia 98 Chini ya CCM kuanzia bunge mpaka halmashauri na wenyeviti wote wa mitaa na serikali. Nadhani kwa Sasa jicho letu tuelekeze kwao watuletee maendeleo na sio kuanza kutafuta watu wa kuwatupia lawama ambao hawapo kwenye vyombo vya maamuzi . Kuanza kumlaumu Lissu aliyepo nje ya system wakati wewe una mamlaka asilimia Mia ni kukuimbia majukumu.
Kwanza kabisa ningekuomba kutambua kuwa katika demokrasia haijalishi serikali imeundwa na Rais wa chama gani, serikali ni serikali, ni chombo ambacho kinampa Rais aliyechaguliwa na wananchi mamlaka ya kukitumia chombo hicho kuiongoza nchi.
Ndiyo nakubali kuwa Lissu alikwenda Ubelgiji kutibiwa baada ya kupigwa risasi na watu wasio julikana. Hayo mambo ya kuponywa na Mungu ningeomba kwa leo tuyaache kwanza maana ni kitu ambacho kinajulikana kuwa mtu anaweza akapata janga, liwe kama hili la kupigwa risasi, kupata ajali ya gari au kuugua ghafla na mengineyo na mwishowe akapona au kufa vile vile.
Bada ya kupona kwake tukaona mwenzetu ame anza pilika pilika za kusafiri nchi tofauti kubwa duniani na kufanya kampeni ya kumkandia na kumchafua Rais wetu mpendwa hayati Magufuli, ambaye alichaguliwa kidemokrasia na watanzania na mgombea wao ku-aknowledge, badala ya kurudi nyumbani kuja kuendelea na shughuli zake za kuleta maendeleo ya nchi.
Vitu kama hivi kwa kawaida havifanywi na watu wenye nia ya kuongoza nchi kwa kupata ridhaa ya wananchi anaotaka kuwaongoza, bali vinafanywa na watu ambao wanataka kujikwamua kutoka kwenye makucha ya wakandamizaji.
Jamaa nafikiri alishauriwa vibaya na alifikiri Tanzania ni nchi rahisi sana kutwaa madaraka kirahisi namna hiyo.
Sawa mbona hatukuwaona hao mabalozi wakilundikana mahakamani Kenya ambako pia kulikuwa na kesi kama hii ya ugaidi dhidi ya Alshabab?
Au kwanini hawakulundikani Ujerumani au Ufaransa ambako nako Kesi kama hizi za kigaidi zimekuwa zikisikilizwa mara kwa mara? Kwanini Tanzania?
Msomi, acha kelele za chura kumzui Tembo asinywe maji bwawani, wewe hujui strategies za mataifa yenye nguvu ya kibepari kama Amerika na mengineyo. Hiyo ni njia ya kutoa vitisho kwa serikali yetu ili isalim amri na kumwachia huru Mr. Mbowe ili waendelee na lengo lao la kuwa na usukani kwenye nchi yetu. Mbowe na chama chake CHADEMA kimewafungulia mlango waingie ili waweze kutu-control sisi. Kama hulitambui hilo shauri lako, lakini iko siku utakuja kunikumbuka kama watafanikiwa.
Umeshawahi kusikia kuwa French wanaingiza Dola Bilion 500 kila mwaka kutoka nchi wanazodai ni
Francophone na kuwarudishia kiasi cha Dola bilioni 30 tu kama msaada? Ningekuomba kwenye swala hili la kimataifa juu ya
terror na
ukandamizwaji wa kiuchumi unaofanywa na nchi tajiri kama Amerika na nchi za EU, jiongeze kidogo naona bado hujapata knowledge na information ya kutosha kuhusu mipangilio yao juu ya mambo ya misaada na jinsi inavyo work. Mawazo na fikira zako ziko bado so local.
Kwa kuanzia naomba msikilize Dr. Arikana Chiombori Quao kwenye hizii clips mbili;
Sikiliza msomi wangu, kama una m-quote mtu basi naomba m-quote right. Mimi nimeuliza tu kama hiyo miradi tunayo jivunia tumeiangalia vizuri upande wa risk analysis zake na hasa bwawa la umeme la Nyerere. Unapo kwenda kuchukua mkopo wowote ule bank lazima wakifanyie assessment kipengele cha risk analysis ya concept na business plan ya project yako vinginevyo itakuwa vigumu kutoa hela zao.
Ndiyo, kama tunavyo jua Bwawa la Umeme la Nyerere linategemea zaidi maji ya mto Rufiji na hasa vyanzo vyake ambavyo kulingana na mabadiliko ya mazingira hatutaweza kuwa na uhakika kama yataendelea kutiririka milele bila kuwa na ukomo. Nasema hivi kwa sababu nakumbuka nilipoupanda Mlima kilimanjaro mwaka 1986 kwenye kituo cha Kibo (
Kibo hut) wakati ule kilikuwa kimezungukwa na barafu kote, lakini nikiziangalia clips na pics za watu wanaopanda Mlima Kilimanjaro hivi sasa sioni barafu tena. Labda kidogo kwa mbali juu.
Hii ni picha ya Kibo Hut sasa
Hiyo inanipa shida kubwa kuamini kama maji ya mto Rufiji yataendelea hivyo hivyo kutiririka kama hivi sasa kwa mda mrefu mpaka tutakapo kuwa na uwezo wa kurudisha pesa za investiment tutakazo kuwa tumeziingiza kwenye project hiyo na kupata faida.
No, unasahau kuwa Lissu aliruhusiwa kuja nchini na akaendesha kampeni zake za kugombea u-Rais murua na hakuna lolote baya ambalo lilimtokea wakati wote wa kampeni? Na utakumbuka pia wakati wa kampeni mara nyingi alikuwa ana i-provoke serikali ili vyombo vya dola vimtie matatani na hivyo kutoa signal ulimwenguni kuwa serikali ya Magufuli ina wanyanyasa wapinzani na wao wachukue hatua dhidi ya Rais. Serikali ilibaki cool na kumpotezea.
Katika kampeni zake zote hakuna kitu chochote substancial alichokuwa anakihutubia kwa wananchi zaidi ya matusi, kashfa kwa Rais Magufuli na uongo mkubwa kama vile; juu ya kuuawa kwa maelfu ya watu huko kibiti ambao alishindwa kuthibitisha.
Watanzania walivyo kuwa na nyodo, wakampotezea tu. Amehangaika wee mpaka akachoka mwenyewe.
Kwenye matokeo akadai kuwa kura zilichakachuliwa, ni upuuzi na ujinga mtupu. Ndiyo hayo ya akina Trump,
ameshindwa kukubali kuwa ameshindwa kuwa-convince watanzania kumpigia kura na hawakujua kwa lipi wampe kura zao? Kukubali kushindwa hiyo ndiyo demokrasia yenyewe mnayo ipigia kelele.
Angalia mwenyewe hizi picha mbili za kupigwa risasi Lissu. Kwenye hiyo picha ya juu inaonyesha mguu wake wa kulia kwenye paja ndiyo umejeruhiwa vibaya sana. Sasa nikuulize swali kutokana na hizo picha, hivi Lissu alikaa upande gani kwenye gari lake? Na dereva wake upande gani wa gari?
Maana matobo au matundu ya risasi yaliyo haribu gari lake kwenye mlango na dirisha yanaonyesha upande wa kushoto wa hilo gari ndiko risasi zilimmiminikia, kama yeye mwenyewe anavyo sema. Sasa katika risasi zote 36 zilizo pigwa zililenga paja lake tu la kulia, wala kweye paja na bega la kushoto na kichwani hazikumfikia?
If that is the case, basi hiyo itakuwa Physics ya hali ya juu ambayo mimi katika maisha yangu ya masomo ya sayansi niliyo yapitia ndani na nje ya nchi sijawahi kusikia. Isitoshe aina ya silaha AK 47 Kalashnikov (picha ya tatu chini) ya mrusi ni deadly weapon ambayo kulingana na picha ya majeruhi sidhani kama huyo anaye tegemea kuwa Rais wenu angetoka salama na kutuonyesha majeruhi ya pajani.
This is absurd!
Halafu kulingana na nature ya picha na nguvu ya silaha AK-47 dereva naye angetobolewa vibaya sana. Uelewe tu kuwa risasi kutoka kwenye hiyo silaha zinaingia na kutoka kwenye mwili wa binadam kamba butter.
Na kama risasi za hiyo weapon zingemwingia kwenye paja lake la kulia, kama anavyodai, basi wasinge toa risasi hata moja kutoka kwenye mwili wake, zote zingepita na kujeruhi mapaja yote mawili vibaya sana. Paja la kushoto ndiyo zaidi, kwani risasi zingetokea huko.
Tumia common sense yako na kipaji mungu amekupa ku-reason your self na sio kukubali tu kulishwa mantangu pori kwa vile CCM huipendi.
Picha ya Lissu hospitalini
Picha ya gari la Lissun kuonyesha matundu ya risasi kwa karibu
Picha ya gari zima la Lissu
AK-47 Kalashnikov
Sijasema serikali ya Ubelgiji, nimemaanisha serikali ya Ujeruman na EU hata Amerika na UK kwa ujumla wake wangependa iwe hivyo, sio siri, lakini tu wanashindwa kwa sababu bado hawajapata entry point.
Ni kweli hakuna Rais ambaye anaweza kutoka alikotoka akaja kazuia mpango wa Taifa na ni kweli pia Tanzania haipati Rais kutoka jalalani, bali kuna mfumo halali wa kumpata Rais ingawa saa zingine una madhaifu, lakini hata hivyo naomba utambue kuwa ni kweli wanataka kumweka Lissu madarakani kinguvu, ili kwanza wao wenyewe wazuie miradi yetu ya naebdeleo isiendelee na sio Lissu halafu washike hatam ya ku-control upatikanaji wa
natural resources zetu kwa maendeleo yao kirahisi.
Unajua katika ulimwengu wa leo Europe na baadhi ya nchi tajiri huko Asia na Amerika kwa asilimia kubwa bila
natural resources kutoka Afrika hazitaweza maintain mfumo huu wa maisha walio nao sasa? Niambie kama Belgium ina dhahabu? Kama jibu ni sio, kwanini sasa dhahabu kubwa ipatikane Congo DRC, lakini soko kubwa la kubadilishana thamani liwe Beligium na sio Congo?
Sisi sio kwamba hatukatai kuwa na ushirikiano nao wa kibiashara, ila tunachota ni kuwa huo ushirikiano wa kibiashara uwe on the
Winn Winn basis. Wao kitu kama hiki hawakitaki na wala hawataki ku-accept, kwasababu wanajiona wao ni superior na wana nguvu kubwa za kijeshi, kwa hali hiyo hawawezi wakawa sawa na sisi.
Mimi sio muumini wa CCM, ningetamani kuwa na vyama vyenye nguvu vya upinzani kama wakati ule wa Dr. Slaa. Lakini sasa kwa vile wapinzani na hasa Kamanda wako Lissu, Lema na wengine kuwa traitors, hiyo siikubali hata mara moja, kwani najua viongozi wowote duniani ambao wanasaidiwa na nchi tajiri za kigeni kuwa madarakani, lazima watafanya mambo kulingana na matakwa ya wale wanao wasaidia kifedha na kiulinzi. Na katika hali kama hii afazali tuendelee na CCM kuliko kuwa watumwa wa ukoloni mambo leo na kufanya mambo yanayo pangwa na kumletea faida beberu kupitia vibaraka.
Si unaona nchi nyingi zinavyo hathirika zenye traitors? Na kama Lissu na makamanda wengine wanataka kweli kuleta mabadiliko ya katiba basi wachukue mfano mzuri wa Wazambia. Rais mpya wa Zambia hakwenda kwa mabeberu na kumkandia Rais wao huko, alibaki nchini na kufanya mbinu za kuwashawishi wananchi juu ya hali halisi ya maisha na hali ilivyokuwa tete kidogo kwao walienda South Afrika na South Afrika sio nchi ya kibeberu kwa sasa, inatawaliwa na marafiki zetu, watu wa race yetu. Wanaotuelewa na sisi kuwaelewa.
Kwa siri yako tu, hakuna bunge ambalo liko kwa ajili ya maslahi ya maisha ya mtu wa chini. Kama mabunge ya nchi tajiri yanashindwa kutetea maslahi ya watu walio wachagua kwa kufanya kazi yake ipasavyo, sembuse mabunge ya nchi hizi zetu masikini? Kwani mipango ya miaka mitano ya serikali ndiyo msaafu ambao lazima utekelezeke hata kama umepitishwa na Bunge? Sielewi hiyo sentensi umeitoa wapi?
Ndiyo, Congo sio Tanzania, lakini hata Congo ilikuwa ina Rais shujaa ambaye naye alidhamiria, kama Ris wetu hayati Nyerere, kuleta umoja wa Wacongo. Wabelgiji na Waamerika walimuua na kumweka kibaraka wao Mobutu Seseko ambaye alitawala kwa mabavu na ukandamizaji wa watu wake kwa maslahi ya Mabeberu wake na baada ya kifo chake ndiyo unavyoona nchi imeingia kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Nasi tukimwacha kibaraka kama Lissu na wengineo wasaidiwe kushika Dola itatutokea hivyo hivyo, tutajikuta tunaingia kwenye mkumbo huo huo wa utawala, Believe me!
Lissu hata wapinga na akifanya hivyo watamtoa, aidha kwa kumuua au kwa kumwekea mizengwe ili wamweke mwingine, hizo ndiyo systems zao zilivyo za kutu-control sisi. Na mali asili zetu zikiisha wanatuacha na kuendeleza uovu wao kwingine!
Kama wao wanania kweli ya kusaidia waafrika si waende Tunisia wakawasidie wao. Si nchi ambayo ina demokrasia Afrika? Kwanini hawaendi huko? Kwa sababu Tunisia haina rasilimali kama nchi yetu, brother. Amka!
Nakusihi usiangalie tu siasa za Tanzania peke yake na kusikiliza BBC, CNN, DW na Al Jazeera. Hivi vyombo ni vyao na viko kwa madhumuni ya kupiga propaganda nzuri kuhusu nchi zao na mabaya kuhusu sisi. Hivyo vyombo haviko huru huko kwao vinatumikia serikali zao kwa maslahi ya nchi zao na watu wao sisi wanatudanganya tu.
Kwa vile bado nakuona hujawa matured kutambua mambo mabaya na mazuri ya dunia hii nimefurahishwa sana na kufarijika mno na hoja yako. Ningependa sana kukusaidia ili upate uelewa mkubwa wa kisiasa na uchumi wa dunia ili baadae mungu akikujalia uje kuwa kiongozi wetu mzuri ambaye atatukwamua sisi kutoka kwenye hii dilema ya maisha.
Ielewe history ya ancient Egypt na maendeleo ya ancient Egypt, historia ya influence ya
Emperor Alexander The Great wa Ugiriki kwenye mfumo mzima wa maisha ya binadam duniani, kuenea kwa dini ya kiislam mpaka Europe, warumi na Ukristo, influence ya ukristo duniani na maendeleo ya wazungu Europe, Amerika, Asia na Afrika na angalia mfumo mzima wa kiuchumi wazungu walivyo pitia hasara walizo sababisha na faida waliyo ipata na kadhalika na kadhalika. Utagundua kitu tu, niamini!