Pre GE2025 Tundu Lissu: Tubadilishe tarehe ya Uchaguzi Mkuu kwa Miaka miwili ili tuwe na tume Huru

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Hakuna mbunge wa CCM au diwani anayependa kushindwa kwenye uchaguzi .
Kwa hiyo huo ujinga wa kusema uweke nguvu kwenye udiwani na ubunge ni upuuzi mtupu.

Samia siotanganyika na katika Hali ya kawaida hana uwezo wa kuiongoza Tangayika na anawaogopa mafisadi kwa sababu anadhani kuwa Magufuli walimtishia kumbe ni mapenzi ya Mungu tu na sio nani wala nani ?

Hakuna mtu asiyeka ashinde hata zezeta ndani ya CCM lakini ashinde kwa haki.

Kama hawapo tayari kushinda kwa haki basi waendelee na madaraka mpaka watakapokuwa tayari kushindana na sio kuleta uchaguzi wa hadaa kuua ili kuua watu.

Hivi kama wanaua watu uchaguzi wa serikali za mitaa usio na mshahara watamuacha mtu kwenye uchaguzi wa kumpata Rais anayelipwa mamilioni ya pesa na Fungu la matumizi kubwa kuliko Wizara zote na halihijiwi wala kuulizwa matumizi yake . Wataacha mtu kwenye Ubunge mshahara mil. 18 kwa mwezi na posho ya jimbo juu na hakuna anayejoji matumizi yake maana wote ni wale wale .

Jiulize huyu ndiye Samia yule wa wakati anaingia Ikulu . Ni kitu gani kimembadili na kuwa na roho mbaya kuliko marais wote waliowahi kutawala Tanzania na hata Zanzibar .
Rais asiyejali raslimali za umma ,hajali uhai wa watu ,hasjali demokrasia ndani ya Chama chake ,hajali demokrasia nje ya chama chake . HAJALI MATUMIZI YA FEDHA ZA UMMA . Anachowaza ni kushinda uchaguzi tu.

Lakini pia ushindi wake hauna umuhimu wowote kwa nchi maana hana malengo yake binafsi na nchi hizi hasa Tanaganyika . Anajua wazi kuwa akifanya chochote na vyovyote siku akistaafu akirudi kwenye nchi ya Zanzibar hakuna mtu atakayeweza kumshitaki hata kama katiba itabadilishwa maana ile ni nchi nyingine na atakua kama yupo uhamishoni .
Labda tu kama patakuwa na mali zake zitaifushwe lakini kumfuata na kumkamata akiwa nchini nchi za nje sio Rahisi .

Kwa nini watanzania tuzuiwe kumchagua Rais na viongozi tunawataka .

Huo utamaduni wa CCM utauliza watu mpaka lini na kwa manufaa ya nani ?
Yaani Samia akikosa urais kwa haki atapata hasara gani wakati Nchi itabaki kuwa na amani .?
Au yeye ni nani katika hii nchi kwamba bila yeye kuendelea na urais ambao kimsingi hakuwahi kugombea wala kuomba nafasi ya urais lakini leo eti ni lazima aendelee .Aendelee kutoka wapi wakati awamu yake ni kuanzia 2025 ndipo atajipima kwa kuomba kura .? Nani anayemngangania mtu ambaye hata ndani ya chama chake hawezi kushinda ?

Kwa nini CCM ilete mtu asiyekubaliaka hata ndani ya chama chake halafu utegemee kuua watu ili awekwe madarakani ?
Hayo ni mapinduzi ?
Kwa nini yafanyike mapinduzi kwa mgongo wa uchaguzi halafu apachikwe raia kuongoza utawala wa kijeshi .

Hivi Kuna tofauti gani kati ya chaguzi za Rwanda ,Uganda na Somalia ,Sudani na Chaguzi za Tanzania?
Kwa nini tunamuona Kagame na Museveni ni Dikteta wakati anashinda kwa kura kama Tanzania inavyoshinda kwa chaguzi za Hadaa. ?

Yaani Samia anaingia madarakani kilaini kabisa halafu yeye anataka wenzake wa aingie kwa jasho na damu ? Kwa nini asiheshimu katiba iliyomweka madarakani ?

Kwa nini asijisikie vibaya kwa chaguzi za dhumlma zilizoleta mauaji kuanzia Zanzibar na Sasa Bara ?
Hivi haoni kuwa ni bahati tu huku bara hakuna watu wenye imani kali kama kule Zanzibar ambapo chuki za kisiasa zilizaa chuki za kidini mpaka makanisa yakawa yanachomwa Moto na mapadri kumwagiwa tindikali . Chuki za kidini kule Zanzibar wakati wa Mashehe wa uamsho yalisababisha nchi kuwa kwenye taharuki kubwa sana chanzo kikiwa ni kukosekana kwa haki wakati wa uchaguzi hali iliyowafanya wazanzibar wengi kukenga chuki dhidi ya watu wa bara na hata kuwaona kuwa wote ni makafiru wasiojua dini kutokana na matendo mabaya wakati wa uchaguzi.
 
Kuna viongozi wenu huko CCM wana watoto wenye uraia wa US, mbona hatuoni ni nongwa, sembuse watoto kuwa ughaibuni kwa masomo!

Mtanzania wa kweli? Familia yake ni raia wa USA, yeye anaishi Ubeleji, utamwitaje Mtanzania wa kweli? Wewe na mimi wenye familia na ndugu zetu hapa tutaitwaje sasa?
 
Haya maandishi yamejaa ujumbe mzito.
Mungu akubariki sana.
Moderators ikiwapendeza wekeni huu mchango "sticky" pale juu.
 
Ndugu 1000 digits , haya madini leo ni baraka sana kwangu na naamini kwa yeyote mwenye akili timamu na mzalendo wa kweli wa Tanzania, yatakuwa baraka kwake pia.
Mungu aendelee kukubariki.
 
And what if nothing has been changed ?
Najua hiki chama watasusia tu uchaguzi.
 
Reactions: Tui
Jamaa kapanda mashua ya vibwengo.Kwani 2025 walikuwa hawajui kuna Uchaguzi?
Anajua hawajitayarisha na hawana pesa za kampeni na uchaguzi wenyewe. Wanajaribu ku buy time.
If you fail to plan you plan to fail.
 
Sijawahi kwa kweli. Sasa kama unatishiwa na Katibu Kata, Katibu Tarafa, mgambo, msimamizi wa uchaguzi kufanya maovu na unakubali, utaweza kweli kusimama kidete ili uchaguzi usifanyike? Kama unaweza mnashindwa kuwabana hao mgambo, katibu kata na wengine ili haki ifanyike? Najua sio vituo vyote vinaweza kufanya hivyo lakini kuna maeneo ambayo watu wake ni majasiri na wanaweza mtu wao anatangazwa. Msimamo huo uonyeshwe toka kwenye watu kuandikishwa, na urudishaji wa fomu. Kutegemea kuwa Lissu na wenzake ndio watakaoleta mabadiliko peke yao ni kuota ndoto mchana.

Amandla...
 
🀣🀣🀣🀣🀣🀣🀣😁😁😁😁😁😁😁
 
Reactions: Tui
Jamaa kapanda mashua ya vibwengo.Kwani 2025 walikuwa hawajui kuna Uchaguzi?
Anajua hawajitayarisha na hawana pesa za kampeni na uchaguzi wenyewe. Wanajaribu ku buy time.
If you fail to plan you plan to fail.
Uko sahihi mia kwa mia
 
Reactions: Tui
Tundu Lissu ana mahesabu Makali!
... yaani anajua ndani ya miaka hiyo miwili Makali ya zuia misaada ya Trump yatakuwa yameishawalegeza CCM, kwahiyo yeye atamshinda Mama Samia kirahisi sana!

πŸ‘Š 🀣✌️
 
Tundu Lissu ana mahesabu Makali!
... yaani anajua ndani ya miaka hiyo miwili Makali ya zuia misaada ya Trump yatakuwa yameishawalegeza CCM, kwahiyo yeye atamshinda Mama Samia kirahisi sana!

πŸ‘Š 🀣✌️
Inaelekea wewe hujui kuwa mirija ya marafiki zake na lisu ya kueneza ushoga duniani pia imekatwa!
 
Inaelekea wewe hujui kuwa mirija ya marafiki zake na lisu ya kueneza ushoga duniani pia imekatwa!
Hii propaganda yako ishapitwa na wakati. Nakushauri utafute nyingine ili uendelee kupata chumvi kutoka kwa wanaokutuma kuchafua viongozi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…