1000 digits
JF-Expert Member
- Oct 16, 2012
- 7,201
- 9,529
Kwa mawazo yangu wazo la kusogeza mbele uchaguzi ni baya kwa sababu:
1. Linatoa loop hole ya kubadilisha term ya urais.
2. Hamna guarantee ya mabadiliko yeyote maana inategemea mno nia njema ya waliopo sasa madarakani.
3. Rais aliyepo hatakubali kuwa Rais wa kwanza wa CCM aliyedumu kwa muhula mmoja. Hilo CDM wasahau.
Badala yake CDM iweke nguvu katika kuhakikisha vyama vya upinzani makini vinapata wabunge na madiwani wengi. Muda uliobaki utumike katika kupata wagombea wanaokubalika na kujenga ushirikiano na vyama vingine. Wakiweza kupata wabunge makini watakuwa katika nafasi ya kusukuma jambo hili nje na nfani ya Bunge.
CDM itumie vilevile kupata resources za kujiendesha na kuwahamasisha wananchi.
Aidha, mwaka 2030 patakuwa na mabadiliko ya uongozi CCM na hivyo kukifanya kuwa vulnerable kuliko sasa kwa sababu patakuwa na mnyukano wa wanaoyaka kugombea urais.
Aidha, Rais wa sasa atataka kuacha legacy ya kuacha nchi yenye Katiba bora inayowapa watanzania uhuru wa dhati wa kuchagua viongozi wanaowataka ambao watawajibika kwao. Tukumbuke kuwa Samia alihusika sana katika juhudi zilizopita za kupata Katiba Mpya. Naamini angependa kumalizia kazi aliyoanza.
Mwisho, miaka mitano utaipa CDM muda wa kutosha wa kutibu majeraha ya uchaguzi wa Mwenyekiti wake na hivyo kuunganisha wanachama na wafuasi wake. Watakuwa wanajidanganya kama wataamini hayapo.
Amandla...
Hakuna mbunge wa CCM au diwani anayependa kushindwa kwenye uchaguzi .
Kwa hiyo huo ujinga wa kusema uweke nguvu kwenye udiwani na ubunge ni upuuzi mtupu.
Samia siotanganyika na katika Hali ya kawaida hana uwezo wa kuiongoza Tangayika na anawaogopa mafisadi kwa sababu anadhani kuwa Magufuli walimtishia kumbe ni mapenzi ya Mungu tu na sio nani wala nani ?
Hakuna mtu asiyeka ashinde hata zezeta ndani ya CCM lakini ashinde kwa haki.
Kama hawapo tayari kushinda kwa haki basi waendelee na madaraka mpaka watakapokuwa tayari kushindana na sio kuleta uchaguzi wa hadaa kuua ili kuua watu.
Hivi kama wanaua watu uchaguzi wa serikali za mitaa usio na mshahara watamuacha mtu kwenye uchaguzi wa kumpata Rais anayelipwa mamilioni ya pesa na Fungu la matumizi kubwa kuliko Wizara zote na halihijiwi wala kuulizwa matumizi yake . Wataacha mtu kwenye Ubunge mshahara mil. 18 kwa mwezi na posho ya jimbo juu na hakuna anayejoji matumizi yake maana wote ni wale wale .
Jiulize huyu ndiye Samia yule wa wakati anaingia Ikulu . Ni kitu gani kimembadili na kuwa na roho mbaya kuliko marais wote waliowahi kutawala Tanzania na hata Zanzibar .
Rais asiyejali raslimali za umma ,hajali uhai wa watu ,hasjali demokrasia ndani ya Chama chake ,hajali demokrasia nje ya chama chake . HAJALI MATUMIZI YA FEDHA ZA UMMA . Anachowaza ni kushinda uchaguzi tu.
Lakini pia ushindi wake hauna umuhimu wowote kwa nchi maana hana malengo yake binafsi na nchi hizi hasa Tanaganyika . Anajua wazi kuwa akifanya chochote na vyovyote siku akistaafu akirudi kwenye nchi ya Zanzibar hakuna mtu atakayeweza kumshitaki hata kama katiba itabadilishwa maana ile ni nchi nyingine na atakua kama yupo uhamishoni .
Labda tu kama patakuwa na mali zake zitaifushwe lakini kumfuata na kumkamata akiwa nchini nchi za nje sio Rahisi .
Kwa nini watanzania tuzuiwe kumchagua Rais na viongozi tunawataka .
Huo utamaduni wa CCM utauliza watu mpaka lini na kwa manufaa ya nani ?
Yaani Samia akikosa urais kwa haki atapata hasara gani wakati Nchi itabaki kuwa na amani .?
Au yeye ni nani katika hii nchi kwamba bila yeye kuendelea na urais ambao kimsingi hakuwahi kugombea wala kuomba nafasi ya urais lakini leo eti ni lazima aendelee .Aendelee kutoka wapi wakati awamu yake ni kuanzia 2025 ndipo atajipima kwa kuomba kura .? Nani anayemngangania mtu ambaye hata ndani ya chama chake hawezi kushinda ?
Kwa nini CCM ilete mtu asiyekubaliaka hata ndani ya chama chake halafu utegemee kuua watu ili awekwe madarakani ?
Hayo ni mapinduzi ?
Kwa nini yafanyike mapinduzi kwa mgongo wa uchaguzi halafu apachikwe raia kuongoza utawala wa kijeshi .
Hivi Kuna tofauti gani kati ya chaguzi za Rwanda ,Uganda na Somalia ,Sudani na Chaguzi za Tanzania?
Kwa nini tunamuona Kagame na Museveni ni Dikteta wakati anashinda kwa kura kama Tanzania inavyoshinda kwa chaguzi za Hadaa. ?
Yaani Samia anaingia madarakani kilaini kabisa halafu yeye anataka wenzake wa aingie kwa jasho na damu ? Kwa nini asiheshimu katiba iliyomweka madarakani ?
Kwa nini asijisikie vibaya kwa chaguzi za dhumlma zilizoleta mauaji kuanzia Zanzibar na Sasa Bara ?
Hivi haoni kuwa ni bahati tu huku bara hakuna watu wenye imani kali kama kule Zanzibar ambapo chuki za kisiasa zilizaa chuki za kidini mpaka makanisa yakawa yanachomwa Moto na mapadri kumwagiwa tindikali . Chuki za kidini kule Zanzibar wakati wa Mashehe wa uamsho yalisababisha nchi kuwa kwenye taharuki kubwa sana chanzo kikiwa ni kukosekana kwa haki wakati wa uchaguzi hali iliyowafanya wazanzibar wengi kukenga chuki dhidi ya watu wa bara na hata kuwaona kuwa wote ni makafiru wasiojua dini kutokana na matendo mabaya wakati wa uchaguzi.