BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Makamu huyo Mwenyekiti wa CHADEMA amesema kama Mkataba huo utavunjwa sasa kutakuwa na Kesi lakini haitaligharimu Taifa fedha nyingi japokuwa kutakuwa na mikwaruzo
Amesema jambo lifanyike wakati huu ambao Muwekezaji hajaleta Vifaa vyake na hivyo hatodai fidia kubwa kuliko Serikali ikisubiri miaka 10 au 20, fidia itakuwa kubwa na hakutokuwa na Fedha Serikalini
Ikumbukwe kuwa licha ya kuwepo hoja nyingi kutoka kwa Wananchi wa Kawaida, Wanasiasa na Wanasheria kuhusu utata wa Makubaliano hayo, Serikali inaendelea na hatua mbalimbali ikiwa ni pamoja na kupata ridhaa ya Chama Tawala (CCM).