BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
“Ukiangalia taarifa ya watazamaji wa uchaguzi wa kitaifa na kimataifa tangu mwaka 1995 wote wamesema Tume ya Taifa ya Uchaguzi siyo huru, na wamesema siyo huru kwa sababu, moja ni tume ya Rais kwa maana kwamba wajumbe wake wote ni wateule wa Rais , mtendaji wake mkuu ni mteule wa Rais, watumishi wake wote ni watumishi wa serikali,"
"Kwa Katiba yetu watumishi wa serikali ni wateule wa Rais au wanafanya kazi kwa niaba ya Rais na Rais ndiye mamlaka yao ya nidhamu. Kwa hiyo wote waliotazama uchaguzi, wa kimataifa na kitaifa wamesema kwa kigezo hicho cha kwanza cha mamlaka ya uteuzi hii siyo tume huru'
"Tume ya Warioba ilifanya kazi kubwa sana ya utafiti kwenye hili suala la Tume ya Uchaguzi, kuna juzuu nzima ya Tume ya Warioba kuhusu masuala ya uchaguzi wa nchi yetu na ililiangalia hili suala kwa undani sana, na tume ya Warioba vilevile ilisema hii tume siyo huru kwa sababu ni tume ya Rais , wajumbe wake wote ni watumishi wa Rais , Mtendaji Mkuu ni mtu wa Rais, watumishi wote ni watu wa Rais na katika utendaji wake haina uhuru wowote”- Tundu Lissu."
“Watumishi wa tume, wajumbe wa tume wote na watumishi wake wote kuanzia msimamizi wa kituo mpaka Mwenyekiti wa Tume mamlaka yao ya nidhamu ni Rais, wasimamizi wote wa chaguzi (Wasimamizi wa uchaguzi ni wale wanaotangaza matokeo kwenye majimbo), wakurugenzi wote ni wateule wa Rais na wanaondolewa na Rais, kwa hiyo kwenye suala la uwajibikaji wa wajumbe na watumishi hii si tume huru ni tume ya Rais, na mwisho kwenye masuala ya fedha tume huru inakuwa na utaratibu tofauti wa kupata fedha zake kutoka serikalini, tume inakuwa na bajeti yake yenyewe na hiyo bajeti ikipitishwa, tume inakuwa na mamlaka kamili na ya kipekee ya kutumia hizo fedha tume, haiendi kupanga foleni kwenye ofisi ya TAMISEMI au Ofisi ya Waziri Mkuu au Ofisi ya Rais kupata mgao ili iendeshe uchaguzi au iandikishe wapiga kura, inatakiwa isimamie fedha zake kama zilivyopitishwa kwenye bajeti bila kutegemea mamlaka nyingine"
“Kwa mujibu wa katiba yetu tume ina uwezo wa kutengeneza majimbo ya uchaguzi lakini lazima ipate ridhaa ya Rais, kwa maana nyingine ni kwamba Rais asipotoa ridhaa tume haina uwezo wa kutengeneza majimbo ya uchaguzi, sasa kwa wasiofahamu wanaweza wasielewe umuhimu wa suala hili, chaguzi huwa zinaanza kushinda au kushindwa kwenye utengenezaji wa majimbo, kuna ‘uchafu’ mwingi kwenye utengenezaji wa majimbo ya uchaguzi katika nchi yetu na haya ni maneno ya waangalizi wa uchaguzi zetu tangu mwaka 1995, tume haina uhuru wa kutengeneza majimbo , kimsingi majimbo yanatengenezwa na Rais na watu wake kwa sababu, Rais asipotoa ridhaa hakuna kinachofanyika"
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara Tundu Lissu amezungumza hayo Ijumaa, 12 Aprili, 2024 katika kipindi cha Power Breakfast kinachorushwa na kituo cha habari cha Clouds FM.
====================================
The Warioba Commission conducted extensive research on the issue of the Electoral Commission. There is a whole volume of the Warioba Commission dedicated to the electoral matters of our country, and it examined this issue in great detail. The Warioba Commission also stated that this commission is not independent because it is the President's commission. All its members are presidential appointees, the Executive Director is appointed by the President, and all its staff are presidential personnel. In its operations, it lacks any independence. - Tundu Lissu.