Bush Dokta
JF-Expert Member
- Apr 11, 2023
- 24,831
- 45,154
Hii ni endelevu haina mwisho......tutaiacha tutaachia watoto nao watadai tudaini tume yenu huru ya uchaguzi
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hii ni endelevu haina mwisho......tutaiacha tutaachia watoto nao watadai tudaini tume yenu huru ya uchaguzi
12 April 2024
TUNDU LISSU - TUME HURU YA UCHAGUZI SIYO HURU, RAIS ANATEUA NA KUTENGUA WAJUMBE WAKATI PIA NI MGOMBEA KTK UCHAGUZI
View: https://m.youtube.com/watch?v=gbl_dbYBof0
Toka maktaba :
6 August 2022
Tundu Lissu: Idadi ya wabunge wa kuchaguliwa iwiane na idadi ya raia wanaowakilisha
Makamu mwenyekiti wa CHADEMA Mh. Tundu Antipas Lissu akiangalia mgawanyo wa majimbo yenye watu wengi zaidi anagundua kuwa haiwakilishi na idadi inayostahili ya wabunge. Wilaya ya Temeke mkoa wa Dar es Salaam Mwanzo
Mfano mkoa wa Dar es Salaam ulitakiwa kuwa na wabunge wasiopungua 25. Lakini una wabunge wachache sana wakati ina idadi kubwa ya wapiga kura .
Mkoa wa Lindi yenye wabunge 9 huku idadi ya wapiga kura ni ndogo sana. Mkoa wa Tabora ina idadi ndogo ya wapiga kura lakini ina wabunge wa kuchaguliwa 12 huku mkoa wa Tanga wenye idadi ndogo pia ya watu ina wabunge 12. Mikoa hii iliyotajwa kama mfano wa uwiano usiolingana baina ya idadi ya wapiga kura na wingi wa wabunge pia ni maeneo yaliyo ngome ya CCM.
Na kwa hiyo mgawanyo wa majimbo umeiba uchaguzi kwa kutumia mifumo ya kikatiba na kitaasisi kwa maana Tume ya Uchaguzi ni ya rais na mwenye mamlaka ya kutengeneza mikoa ni rais na mteuzi wa viongozi wa Tume ya Uchaguzi ni rais pia. Orodha ya Jumla ya majimbo ya uchaguzi kwa kufuata na tovuti ya bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni majimbo 273 : source : Parliament of Tanzania
Huko nchini Kenya Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka ya Majimbo ya Uchaguzi yaani IEBC ndiyo yenye mamlaka ya kutengeneza mipaka ya majimbo ktk Kenya yote inayotumia formula ya idadi ya watu ktk sehemu ndiyo itatoa mwangaza kutakuwepo wabunge wangapi. Sababu ni kuwa nchini Kenya demokrasia inaangazia kuwa wabunge wanawakilisha watu kwa kura na siyo eneo.
Tofauti na Tanzania ambapo ambapo Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC haina nguvu kikatiba kutengeneza majimbo kwa kufuatana na idadi ya wapiga kura.
Mfumo huo wa kuangalia eneo hata kama lina wapiga kura wachache na kuwapatia idadi kubwa ya wabunge huku mikoa kama Dar es Salaam, Mwanza yenye idadi kubwa ya wapiga kura inapewa wabunge wachache sana.
Sababu ni kuwa imeonekana maeneo yenye watu wengi ambao ni wapiga kura huwa wana tabia au mazoea ya kuchagua wapinzani hivyo kwa Tanzania wengi hao wanapewa wabunge wachache ili kudhibiti idadi ya wabunge wa upinzani wanaoweza kuchaguliwa . Parliament of Tanzania
Wawakilishi wa waangalizi wa chaguzi toka ndani na nje wameona mapungufu haya ya kuwa kuna maeneo yana wapiga kura wachache sana lakini ina wabunge wengi, huku kuna maeneo yenye wapiga kura wengi inawakilishwa na wabunge wachache sana na hii Indonesia kukosekana uwiano kati ya idadi ya wabunge na wapiga kura wao.
Source : Forbs Media
Tundu lissu Wakimsikiliza tutaokoa pesa nyingi za Watanzania na kuwa na uongoi wenye Tija
Kiukweli chama hiki kimekuwa Baraka kwa watanzania waliokata tamaa.Tanzania imepata bahati kuwa na chama cha siasa CHADEMA.
Huyo si kwamba hajui ila ni ChawaKWenye hili naomba Nipingane na wewe..
Tanzania hatuna Tume Huru Endapo Mgombea Wa urais (Mmoja ya wagombea) Ndio Anayechagua Tume na Tume iko chini yake..
Tume Huru wakati Tamisemi "Serikali" Ndo inasimamia Uchaguzi wa Serkali za Mitaa..?
Kuhusu Kuwa Huru kwa Jina Kweli jina lake limeitwa Tume huru...Je iko Huru??
Mimi ninaweza kuita au kuandika Tanzania Ni Nchi tajiri na TunaIzidi Dollar kwa Thamani ila je Kiuhalisia Tunaizidi Dollar??
Asante kwa andiko hili. Huu ndio ukweli.Chadema ni waramba asali mara munamsifu mama na kumtukuza, hamuishi vikao na Samia Ikulu, mulisema Chadema hatapiga magoti kwa serikali ya ccm, hatimae Tundu Lissu alimualika mama belgium bila kuweka wazi hadi leo waliongea nini belgium, lakini mbowe alipotoka jela breki ya kwanza Ikulu, alibadilisha koti na tai akiwa Ikulu ndio akaenda nyumbani kwake sasa mnalalamika nini.
Mmeramba asali sasa wanaoumia ni wananchi, Tundu Lissu haya anaongea sio kutoka moyoni ni kama anamfurahisha mfalme, chadema sasa ni CCM B hawaeleweki, Zamani chadema ikitetea Zanzibar huru sasa wanawatukana wazanzibari waziwazi baada mama kuwa Rais, Chadema haieleweki
Nafkiri Tanzania vyama vya upinzani hasa Chadema kimekosa muelekeo, Watanzania wanahitaji upinzani mpya usio na unafiki ndani yake, Chadema muda wake umekwisha, Mbowe sasa anakazia suruali tu muda wote Ikulu hana tena habari ya Katiba wala Tume huyu ya Uchaguzi. Mbowe siye tena yule wa zamani kwisha habari yake.
Unaandika kama vile umekatwa kichwa vile! Bila shaka una phd ya unafiki.kwahivyo kua na mihemko ndio unaona sifa?
uhuru ni pamoja na kuzira, kususa au kugomea uchaguzi kwan kuna shida gan,
au umelazimishwa kuamini uhuru wa hiyo tume 🐒
yaani wewe ukishinda uchaguzi ndio tume inakua huru, ukishindwa uchaguzi ndio inakua sio Huru 🤣
useless and none sense
sina mihemko hata ukiniita aje dhidi ya kusema ukweli 🐒Unaandika kama vile umekatwa kichwa vile! Bila shaka una phd ya unafiki.