Pre GE2025 Tundu Lissu: Tume ya Uchaguzi sio Huru, ni Tume ya Rais

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Report ya mwaka Gani hiyo???
 
Lucas Mwashambwa Lisu yupi alikwambia anahama muda wowote?

Hujui IPO amri isemayo " Usiseme Uongo"?
Kwani huoni mambo niliyoyaandika ndio ameendelea hata leo kulalamikia na kuonyesha hana imani nayo? Huoni hana imani na wasimamizi wa uchaguzi jambo ambalo nililieleza katika andiko langu? Sasa wapi nilipopotosha? Au amekanusha?
 
Katiba ya Kenya Unaijua au umeisoma Mkuu??

Nitakupa na Attachment ya katiba ya Kenya ili ikisaidie..

Sasa Nisikilize Uchaguzi wa IEBC (Tume Huru ya Taifa Ya uchaguzi isiyo na Mipaka) ya kenya Ambavyo hupatikana..

Rais Huteua watu wanne tu..
Ila watu wengine watatu hutoka Miongoni mwa Board ya Majaji (Maana Tume nzima Ina watu saba)... Na wao baada ya kuthibishwa na Bunge na Kuapishwa na JAJI MKUU huteua CEO wao na katibu wao na jopo zima

"The Commission is made up of seven commissioners and a CEO appointed by them (who also acts as the commission secretary). The 4 commissioners are appointed by the President of Kenya and other 3 appointed By Board of Justice and confirmed by the Kenyan Parliament. Each member serves a six-year term.They took an oath before Chief Justice

By law, no Commissioner can be a member of a political party, and at least four votes are required for any official Commission action. Once appointed, the new commissioners are sworn in by the chief justice in office at the time of their appointment."


Mkuu Katiba Ya Kenya Iko clear sana Yaani hauwezi kulinganisha na Ya Tanzania hata tu kwa kufumba macho
 

Attachments

uchaguzi mkuu ulopita, na bilasha aliongoza ujumbe wa EAC alitoka burundi
Hahah Mimi ntakupa Report Moja tu ya TEMCO zingine katafute Report zote zipo UDSM maktaba..
Acha report za matamshi kacbukue Report za maandishi mkuu..
 

Attachments

Mimi nimekupinga kuwa Lissu ndiye alimualika Rais atoke Tanzania kwenda Ubelgiji. Yeye Rais kwenye misele yake ndiye aliamua kwenda kumtembelea Lissu na siyo Lissu alimuita Rais.
Lissu alimualika mama, toka lini rais ampembejee lissu uko wapi belgium nije
 
Lissu alimualika mama, toka lini rais ampembejee lissu uko wapi belgium nije
Suit your self. Lakini suala la Lissu aliyekuwa uhamishoni kumualika Rais atoke Dar es Salaam aende Brussels kuitikia wito wa Lissu hiyo ngumu.
 
my friend
ajitokeze mtu yeyote yule mwenye sifa, vigezio na mwenye kutimiza masharti tajwa kwenye katiba hiyo, hiyo kazi ataiskia kwenye bomba tu, ispokua yule tu ambae amekua endorsed na president ambae pia atakua ametimiza vigezo na masharti ya kikatiba na si vinginevyo.

with no the hands of the president and the ruling party leader endorsement sahau iyo kitu 🐒

akina kalonzo na huyo raila wanalalamikia nini sasa, kwamba IEBC isukwe upya hali ya kua msoma katiba umesoma na kuona kwamba iko clear...

sasa si chairperson na makamishna wengine wateuliwe na waandae ukaguzi wa 2027, huko bungeni wanahangaika na by partisan talks na engagements za nini sasa 🐒

kwan walivyokua wanateu mahawara zao, spies, na wakuchezesha matokeo ya uchaguzi 2022, in favour of somebody, walitumia utaratibu wa inje ya katiba?
si ni Katiba hiyo hiyo unayosema iko clear 🐒

there is no way the hands of the head of state can be tied on the matter of very crucial institution like tume ya uchaguzi. There is no way 🐒
 

..wapinzani mpaka watangazwe washinde huwa ni option ya mwisho, baada ya Mkurugenzi kubanwa kila mahali, na Polisi kushindwa kuwadhibiti wafuasi wa mgombea wa upinzani.
 
Hahah Mimi ntakupa Report Moja tu ya TEMCO zingine katafute Report zote zipo UDSM maktaba..
Acha report za matamshi kacbukue Report za maandishi mkuu..
sasa si ndio yale yale tu ya Imani.

Report ya waangalizi wa uchaguzi wa Tz kutoka EAC na pengine ile ya EISA are not in favor of your thoughts and opinions, na kwahivyo unaweza kusema imechakachuliwa🤣

lakini sasa ile ya TEMCO, kwasabb Imeandikwa vitu unavyovipenda ndio the best report 🐒

The same thing,
mtu anaposema Tume Huru ya uchaguzi haiko Huru, na mwingine nae anaona iko huru kwa vigezo vyake na Imani yake 🐒
 
..wapinzani mpaka watangazwe washinde huwa ni option ya mwisho, baada ya Mkurugenzi kubanwa kila mahali, na Polisi kushindwa kuwadhibiti wafuasi wa mgombea wa upinzani.
basi si, wabane apo apo sasa 🐒
 
Iko simple tu Hiyo Jibu lake..
Kwa kuwa Rais ana anafasi 4 Za kuteua kati ya 7..
Huenda akateua Hizo nne ambazo ni crucial Na watu wanaoeleweka Japo wakawa Ni moles wake..

Hio haiepukiki kwa sababu katiba inampa mamlaka ya nafasi nne za kwake za kuteua..
Kwa hiyo anaweza akateua yeyto anayemtaka ila kumbuka wanaoteuliwa na Rais lazma wapite bungeni Kujadiliwa so utaratibu Huwa ni mrefu..

Na hata kama Kukitojea Lawama hatulaumu Mtu mmoja..

Tutalaumu IEBC ,Tukitoka hapo tutakuja kulaumu Baraza la Senetor na Bunge kwanini liliwapitisha,halafu tukitoka hapo tutamlaumu Jaji na mwisho kapita tutamlaumu aliye wapendekeza kati ya Jaji na Rais ..

Umeona mlolongo wa Lawama unavyokuwa mrefu mpaka kumfikia Judge na Rais..

Ila kwa Tanzania ni Moja kwa moja analaumiwa Rais kwa sababu yeye ndo anayewaapisha anawateua na anawafanyia vetting na anawathibitisha..

Sasa sinui umeelewa mfumo wa kenya??
 

12 April 2024

TUNDU LISSU - TUME HURU YA UCHAGUZI SIYO HURU, RAIS ANATEUA NA KUTENGUA WAJUMBE WAKATI PIA NI MGOMBEA KTK UCHAGUZI

View: https://m.youtube.com/watch?v=gbl_dbYBof0
Toka maktaba :
6 August 2022

Tundu Lissu: Idadi ya wabunge wa kuchaguliwa iwiane na idadi ya raia wanaowakilisha​


Makamu mwenyekiti wa CHADEMA Mh. Tundu Antipas Lissu akiangalia mgawanyo wa majimbo yenye watu wengi zaidi anagundua kuwa haiwakilishi na idadi inayostahili ya wabunge. Wilaya ya Temeke mkoa wa Dar es Salaam Mwanzo

Mfano mkoa wa Dar es Salaam ulitakiwa kuwa na wabunge wasiopungua 25. Lakini una wabunge wachache sana wakati ina idadi kubwa ya wapiga kura .

Mkoa wa Lindi yenye wabunge 9 huku idadi ya wapiga kura ni ndogo sana. Mkoa wa Tabora ina idadi ndogo ya wapiga kura lakini ina wabunge wa kuchaguliwa 12 huku mkoa wa Tanga wenye idadi ndogo pia ya watu ina wabunge 12. Mikoa hii iliyotajwa kama mfano wa uwiano usiolingana baina ya idadi ya wapiga kura na wingi wa wabunge pia ni maeneo yaliyo ngome ya CCM.

Na kwa hiyo mgawanyo wa majimbo umeiba uchaguzi kwa kutumia mifumo ya kikatiba na kitaasisi kwa maana Tume ya Uchaguzi ni ya rais na mwenye mamlaka ya kutengeneza mikoa ni rais na mteuzi wa viongozi wa Tume ya Uchaguzi ni rais pia. Orodha ya Jumla ya majimbo ya uchaguzi kwa kufuata na tovuti ya bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni majimbo 273 : source : Parliament of Tanzania

Huko nchini Kenya Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka ya Majimbo ya Uchaguzi yaani IEBC ndiyo yenye mamlaka ya kutengeneza mipaka ya majimbo ktk Kenya yote inayotumia formula ya idadi ya watu ktk sehemu ndiyo itatoa mwangaza kutakuwepo wabunge wangapi. Sababu ni kuwa nchini Kenya demokrasia inaangazia kuwa wabunge wanawakilisha watu kwa kura na siyo eneo.

Tofauti na Tanzania ambapo ambapo Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC haina nguvu kikatiba kutengeneza majimbo kwa kufuatana na idadi ya wapiga kura.

Mfumo huo wa kuangalia eneo hata kama lina wapiga kura wachache na kuwapatia idadi kubwa ya wabunge huku mikoa kama Dar es Salaam, Mwanza yenye idadi kubwa ya wapiga kura inapewa wabunge wachache sana.

Sababu ni kuwa imeonekana maeneo yenye watu wengi ambao ni wapiga kura huwa wana tabia au mazoea ya kuchagua wapinzani hivyo kwa Tanzania wengi hao wanapewa wabunge wachache ili kudhibiti idadi ya wabunge wa upinzani wanaoweza kuchaguliwa . Parliament of Tanzania

Wawakilishi wa waangalizi wa chaguzi toka ndani na nje wameona mapungufu haya ya kuwa kuna maeneo yana wapiga kura wachache sana lakini ina wabunge wengi, huku kuna maeneo yenye wapiga kura wengi inawakilishwa na wabunge wachache sana na hii Indonesia kukosekana uwiano kati ya idadi ya wabunge na wapiga kura wao.

Source : Forbs Media
Tume ya Uhusiano na Uratibu Rasimu ya Warioba ililenga kuhakikisha ... Warioba alisema idadi ya wabunge isizidi 75, Bunge Maalum likasema..... soma zaidi : source : Hotuba ya Jaji Josefu Warioba kuhusu Rasimu ya Katiba ya Tanzania
 
Mkuu Hata hiyo hiyo ya EAC na ya Ulaya pia Umeiona naomba uilete nikuonyeshe vipengele walivyoikosoa sana NeC
 
Mkuu Hata hiyo hiyo ya EAC na ya Ulaya pia Umeiona naomba uilete nikuonyeshe vipengele walivyoikosoa sana NeC
vibainishe tu daktari,

mambo haya ya uchaguzi, dosari na kasoro za hapa na pale haziepukiki kwasabb vinafanywa na wanadamu. hata uchaguzi wa kuchagua malasusa ulilalamikiwa, lakini pia TFF, uchaguzi wa ndani katika vyama vya kisiasa, hata kule TLS kulilalamikiwa, hata USA, Russia, Nigeria, DRC na kote ulimwengu dosari zipo...

so,
hayo malalamiko au report hayabatilishi ukweli kwamba uchaguzi ulifanyika.

Hayo yanatisaidia tu kujipanga vizur tuendako mbele. Na Tz chini ya Dr.Samia S.Hassan, tumeanza vizuri sana, tumeruhusu mikutano ya hadhara vyama vya siasa, kwa kurekebisha sheria za uchaguzi, lakini pia kwa nje tumethubutu kuibrand tume, kutoka Tume ya Uchaguzi, na sasa Tume Huru ya Uchaguzi ili iakisi mabadiliko yaliyofanyika na yajayo....

sasa wale wa imani haba kama ya akina Thomaso, kuamini hiyo tume ni huru kweli au ni kiini macho, hilo ni jambo lao binafsi 🐒

ushauri wangu wa bure kwao, ni kwamba wasizire wala kususia uchaguzi,

isije ikawa tumeshafanya uchaguzi, tumemaliza, ndio sasa wanakuja kugundua kwamba kumbe kweli ile ni tume huru ya uchaguzi na uchaguzi mkuu ulikua Huru, wa haki na wa wazi 🐒

wasilete fujo tu, wawe waungwana..
wasubiri uchaguzi mwingine 2028-2030🐒
 
Suit your self. Lakini suala la Lissu aliyekuwa uhamishoni kumualika Rais atoke Dar es Salaam aende Brussels kuitikia wito wa Lissu hiyo ngumu.
Maandalizi yalikuwa babkubwa sana jiridhishe kwa picha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…