Pre GE2025 Tundu Lissu: Tume ya Uchaguzi sio Huru, ni Tume ya Rais

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Tundu lissu Wakimsikiliza tutaokoa pesa nyingi za Watanzania na kuwa na uongoi wenye Tija
 
Huyo si kwamba hajui ila ni Chawa
 
Asante kwa andiko hili. Huu ndio ukweli.
Upinzani ni biashara kama biashara zingine. Wapo likizo 11months.

Kama wananchi ‘maamuzi magumu ndio uponyaji’
Wahalifu wanateuliwa wapo kimya

Wengine tukiandika haya washika filimbi wanafuta.
 
Kwenye nchi ambayo Ina utawala wa Sheria ambapo Rais ndiye anayeapishwa kuilinda katiba ya nchi haiwezekani iwepo ogani au mamlaka yoyote ambayo haiwajibiki kwa mkuu wa nchi (Rais) hiyo haiwezekani.

Ogani au mamlaka yoyote kuwa huru kiutendaji inawezekana lakini inapotenda shughuli zake tayari inakuwa inawajibika kutimiza mipango ya nchi ambapo msimamizi mkuu wa nchi ni Rais kwahyo huwezi kutenganisha majukumu yoyote yaliyopo ndani ya nchi na ofisi ya Rais.

Mifumo ya nchi yetu kiutawala na kiutendaji hata kama itatenganishwa ili kila mfumo au ogani ifanyekazi kwa uhuru wake Bado ni ngumu kuitenganisha na Rais. Mfano Tuna mihimili mitatu bunge, mahakama na Serikali; Sasa mahakama haiwezi kuwajibika bila kumzingatia msimamizi mkuu wa Sheria wa nchi lakini pia je mahakama inaundwajwe na watumishi wake wanapatikanaje?
Ukiacha kuhusu mahakama Bado tunaona chama chenye wabunge wengi ndo kinachokuwa na Rais kwahyo watunga Sheria wetu wakiwa bungeni tusitegemee kuwaona wakawa tofauti na Rais wao lakini pia katiba inampa mamlaka Rais ya kuteua baadhi ya wabunge kuingia kwenye muhimili wa serikali kama mawaziri.

Lakini pia Rais anawajibu wa kutengeneza timu yake ya kufanya nae kazi kitaifa, kimikoa, na kiwilaya na hizo timu lazima ziwajibike kufuata maagizo ya Rais ndani ya eneo husika katika kuwahudumia wananchi.

TUJIULIZE:
1. Ili tume ya taifa ya uchaguzi iwe huru itakaa ndani ya nchi au nje ya nchi?
2. Je ili tume iwe huru iundweje?
3. Ikiwa vyama vya siasa kupitia wawakilishi wake vitahusika kufanya uchaguzi wa kuunda NEC (mwenyekiti na wajumbe wake) je tunaweza kuwa na uhakika gani kwamba hao watu wa NEC hawatakuwa na mapenzi na itikadi za chama chochote?
3. Ikiwa wakati wa uchaguzi tutakuwa na wagombea wawili nafasi ya urais mfano Makonda (CCM) na Lisu (Chadema) harafu matokeo ya uchaguzi NEC wakatangaza Lisu ameshinda urais lakin Makonda akawa na ushahidi na vielelezo vya kwamba uchaguzi haukuwa wa haki na yeye ndiye aliyeshinda uchaguzi je ni mahali gani sahihi ambapo Makonda anaweza kupeleka mashitaka yake ili aweze kupatiwa haki yake??
4. Ikiwa NEC itashindwa kusimamia na kumtangaza mshindi halali wa uchaguzi kutokana na mapenzi na itikadi je ni mahakama zipi sahihi kwa kupeleka mashitaka kati ya mahakama za ndani au za umoja wa Afrika au za umoja wa mataifa?
5. Je katiba ya nchi yetu inasemaje na inatao miongozo gani katika kuiwajibisha tume ya taifa ya uchaguzi endapo haitatenda haki?
6. Je nchi yetu Ina mahakama maalumu kwaajili ya mashitaka ya vyama vya siasa? Kama jibu ndio je zinaundwaje? Kama jibu hapani je ni kwanini?
7. Je tunawezaje kuwa na tume huru bila kuwa na miongozo ya kikatiba?
8. Je nchi haiwezi kuwa na utaratibu mwingine wa kuwapata mawaziri nje ya bunge kama inavyowezekana kwa kuwapata wakuu wa mikoa na wilaya? Kwani haiwezekani mawaziri kupatikana nje ya bunge na kuja bungeni wanapohitajika tu kwaajili ya kutoa majibu na kutekeleza shughuli za serikali bungeni?

MWISHO: Ishu sio tume huru Bali ishu ni kwamba ipo kanuni ipi inayoweza kutumika kuiwajibisha NEC na kutengua matokeo batili yaliyo tangazwa na NEC baada ya uchaguzi?? Je ni mahakama zipi sahihi zitakazotumika kuitafsiri hiyo Sheria au kanuni kwaajili ya kutoa hukumu ya utenguzi wa matokeo feki?
Je tume inatoa muda gani wa kusubiri mashitaka (kama yatakuwepo) kutoka kwa walioshindwa uchaguzi kabla ya aliyetangazwa kushinda uchaguzi kuapishwa?

BADO TUNAJITAFUTA.
 
Unaandika kama vile umekatwa kichwa vile! Bila shaka una phd ya unafiki.
 
Unaandika kama vile umekatwa kichwa vile! Bila shaka una phd ya unafiki.
sina mihemko hata ukiniita aje dhidi ya kusema ukweli 🐒

si ni ukweli ndivyo ulivyo mchungu, unaamsha mihemko 🤣

Tume huru ya uchaguzi ni huru tangu kimuundo hadi kiutendaji, that is the fact...

kwani ukikataa, ukizira au kugomea ukweli huu kuna ubaya wowote?
muhimu kua mstahimilivu japo huzuiwi kua na mihemko 🐒
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…