Tundu Lissu: Tutamkabili Dr Samia kama tulivyomkabili Hayati Dr Magufuli kwenye Uchaguzi Ujao, tumejipanga

Hapa Lissu kapotea!

Umkabili Samia kwenye uchaguzi wenye tume ile ile iliyojaa maafisa vipenyo wa serikali wenye viapo vya utii kwa rais??

Wakurugenzi na PoliCCM wanalinda vibarua vyao unatarajia ushindi gani?

Hapo baada ya uchaguzi tutarajie wimbo ule ule wa miaka yote "TUMEIBIWA" halafu inapita miaka mingine mitano mnajiingiza kwenye igizo hili linaoitwa uchaguzi.

CHADEMA walitakiwa wasusie uchaguzi huu bila tume huru na mfumo mpya wa kueleweka.
 
Kwenye vita lazima adui umpe ujumbe kuwa wewe sio mnyonge
 
Hapa Lissu kapotea!

Umkabili Samia kwenye uchaguzi wenye tume ile ile iliyojaa maafisa vipenyo wa serikali wenye viapo vya utii kwa rais??

Wakurugenzi na PoliCCM wanalinda vibarua vyao unatarajia ushindi gani?

Hapo baada ya uchaguzi tutarajie wimbo ule ule wa miaka yote "TUMEIBIWA" halafu inapita miaka mingine mitano mnajiingiza kwenye igizo hili linaoitwa uchaguzi.

CHADEMA walitakiwa wasusie uchaguzi huu bila tume huru na mfumo mpya wa kueleweka.
Kususa nikumpa adui muda zaidi wakuendelea kukutesa.Dawa ni kupambana naye hivyo kwasababu muda wa ushindi huwezi kuujua.Unaweza ukasusa kumbe ndio siku ngome ya adui inaanguka.
 
kauli hiyo ya Lissu anaonesha kuwa kishashindwa.

Simshangai, nafahamu anaelewa kuwa Tanzania ni Republic siyo democracy, Rais haamuliwi na masanduku ya kura. Anateuliwa, kura ni za kupatia takwimu za uongozi tu.
Dakika 90 ndio zitakazoamua.Bado ni mbali sana kuongea chochote.
 
Bora ungegombea ubunge uwe na mchanango wa maana Bungeni ila huku kwenye Urais si tuu hutapata kura za kutosha Bali ndio itakuwa mwisho wa siasa zako.
Mwenda kuzimu aliishia kuchomoka betri la tiger sembuse wewe unaetoa hewa chafu kwenye jicho la tatu?
 
Kususa nikumpa adui muda zaidi wakuendelea kukutesa.Dawa ni kupambana naye hivyo kwasababu muda wa ushindi huwezi kuujua.Unaweza ukasusa kumbe ndio siku ngome ya adui inaanguka.
Sisi tunamtegemea Mungu. Tunaamini Giza haiwezi kuishinda Nuru
 
Kususa nikumpa adui muda zaidi wakuendelea kukutesa.Dawa ni kupambana naye hivyo kwasababu muda wa ushindi huwezi kuujua.Unaweza ukasusa kumbe ndio siku ngome ya adui inaanguka.
Njia pekee ya kuleta chaguzi huru ni hadi yatokee kama ya Kenya 2007/2008
 
Mwaka 2025 ni Mwaka wa Ukombozi, hakuna mwaka mwingine,
Unajitahidi kwa uandishi ulio nyooka kidogo; ingawa uliniudhi sana kwa ile lugha yenu ya huko mlikotoka. Unapokubali kuwa mtu wa hapa, basi huko kwingine achana nako kabisa.

Kuhusu Lissu. Huyu ni kiongozi tofauti kabisa na hawa wengine wa hivi karibuni tulio wahi kuwa nao.

Kama siyo huyu atakaye tusaidia kuwaondoa hawa watekaji wa CCM; hasa hasa huyu 'Chura Kiziwi', basi nchi hii itakuwa na bahati mbaya sana kwenda mbele..
Tumpe ushirikiano Tundu Lissu; hata kama ni kwa kazi moja tu ya muda mfupi; kuondoa utawala huu usio wajali waTanzania.
 
Alipigwa spana hadi betri iligoma
Mkuu 'Erythro', Tundu Lissu kajibu swali ambalo nimekuwa nikiuliza hapa JF kwa karibu mwaka mzima sasa bila ya kupata jibu la kueleweka. Yeye kalijibu swali hilo hilo kwa sekunde chache tu! Swali na jibu vinahusu uchaguzi wa serikali za mitaa, na hata ule wa wabunge na rais hapo mwakani. Kaeleza wazi kwamba CCM wamo kazini kutumia njia zile zile walizo zizoea kwenye chaguzi zote, na jibu lake kalitoa bila ya kumung'unya maneno.

Ninachoona mimi hapa JF ni kwamba CHADEMA hawahitaji tena uwakilishi wa chama hicho kwenye jukwaa hili. Ndiyo maana kila siku tunakutupia lawama wewe hapa kwa makosa tu!
 
Back
Top Bottom