Tundu Lissu: Tutazipima kauli za Kikwete kwenye Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala!

Tundu Lissu: Tutazipima kauli za Kikwete kwenye Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala!

Big-in,
najua unaandika hayo uloandika kwa kutumia mikono,lakiniakili inayofikiri kichwani inajua ukweli kuwa TL ni mwanasheria makini kuliko wote kwa sasa tanzania.

Ndio kuna wansheria wengi mno nchi hii wenye PhDs na hata maprofesor lakini what they do is negligible. Kama wengi wallioko magambani wamejaa phds za kariakoo na/ama wanazitumia kuliibia taifa na hawana msaada kwabisa kwa nchi, hawa hatuwataki.
Namkumbuka Masumbuko Lamwai... Yaani walimkaba kwenye urekchara pala UDSM na wakamtimua kwenye nyumba ya chuo... Akaenda Zanzibar, wakahakikisha anakula jeuri yake, and then wakamtumia mtu kumweleza kilichokuwa kinajili.... Akarudi magambani na sasa eti ni mwanasheria mkuu wa chama... HALAFU YUPO KIMYAAAAAAAAAA KAMA KAHANA NCHI VILEEEE

Lisu hawawezi kumfanyia hayo...
 
The man z the proud of Tanzania....ni kielelezo cha IQ ya mtanzania......kama watanzania wote tukitumia elimu zetu kwa kuyaweka maslahi ya nchi yetu mbele kama TL nchi yetu itaheshimika ndani na nje.....leo akina kagame na wengine wanafikia mpaka kutoa matusi kwa rais wetu kwa sababu ya watawala kushindwa tumia akiri linganifu na za mtanzania kujiongoza na kuongoza taifa.......ubora wa tundu lisu si ndani ya bunge pekee bali hata nje ya bunge.....refer kLissu ni kielelezo botaeria na angestahili kiwa mwanasheria Mkuu wa serikali wawekezaji uchwara na wezi wangesepa
 
mtaumiza vichwa sana nyie wenye rangi ya visamvu. Lissu ni baba yenu.
 
Amemfundisha spika sheria,amemfundisha mwanasheria wa serikali sheria, amemfundisha waziri mkuu sheria, amewafundisha kina ndugai, wasira, lukuvi, nk. "na sasa anamfundisha rais wetu sheria. Jamani si aongezewe mshahara

"Katika watu wanaohitaji maombi ni Lissu".....By Lema.
 
Huyu jamaa ni mnafiki yeye si alisema muungano umevunjika sasa mambo ya kwenda Znz yametoka wapi au anatafuta "sympathy" ya wa Zanzibar.

Tulia wewe,acha GT wachangie mambo ya Lissu. Akili ndogo kama zako haziwezi kamwe kumuelewe Tundu Lissu wakati anaongea, chukua mf. mwingine wa ndugai na Mr. Dhaifu wanavyopataga shida kuelewa nn Mh. Lissu anachoongea.
 
mimi kama mtanzania wa kawaida nisiyekuwa na chama ninamkubali sana Tundu lisu kwa hoja yake imesimamia ukucha mpaka kikwete anaishia kutapatapa na kutiririka matusi badala ya hoja..nadhani kikwete alikosea njia kushinda na Lisu kwani siyo weight yake, TL ni heavy weight champs kwa hoja na hua anatoa facts zaidi na siyo maneno niliambiwa kama kikwete alivyo fanya kwenye hotuba yake. Inanskitisha sana kuona kiongozi wa nchi anaendesha nchi kwa kuambiwa ndyo maana mamuzi yao huwa mabaya na mabovu kutokana na watendaji wa serikali wasiyokuwa na nia njema na watanzania.

Umenena #fact
 
Tulia wewe,acha GT wachangie mambo ya Lissu. Akili ndogo kama zako haziwezi kamwe kumuelewe Tundu Lissu wakati anaongea, chukua mf. mwingine wa ndugai na Mr. Dhaifu wanavyopataga shida kuelewa nn Mh. Lissu anachoongea.

kweli mkuu,rais kwny speech yake ameonyesha hamuelewagi TL.af ameisifia kambi ya upinzani kwa mazuri yaliyowasilishwa,alafu kwny yale anayodhani co mazuri kayatumia kumtukana TL,jiulize kwa nini hajaitukana kambi rasmi.Rais ana ghubu la wifi
 
Bavicha sounds...hivi TEC na CCT wameshirikishwa au hawakushirikishwa?

Kushirikshwa kwa TEC au CCT haiwezi kubadili azma nzima ya CCM kuyumbisha mchakato mzima wa katiba mpya. Msiwe mnang'ang'ania TEC na CCT. Wananchi wanachochukia ni ghilba ya CCM kwenye issue ya katiba mpya kwa mapana yake na si vinginevyo. Tukubali chama tawala haina njema na katiba mpya!
 
MNADHIMU wa kambi rasmi ya upinzani bungeni, Tundu Lissu, amesema kuwa watapima kauli ya Rais Jakaya Kikwete kuhusu muswada wa sheria ya mabadiliko ya katiba, watakapokutana leo katika Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Lissu alisema kuwa Rais Kikwete katika hotuba yake kwa taifa juzi alisema kuwa suala hilo linazungumzika.

"Mimi ninataka kuona leo kwenye Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala liwepo suala hilo katika ratiba kati ya mambo yatakayojadiliwa tayari kwa ajili ya kurejesha muswada bungeni.

"Kama suala hilo halitakuwepo, basi hotuba ya rais itakuwa ni porojo za Magogoni (Ikulu). Rais asiposaini muswada huo ataonyesha nia nzuri aliyokuwa nayo, na hayo tuyaone katika ratiba ya kamati," alisema.

Lissu ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA) na msemaji mkuu wa kambi hiyo kwa Wizara ya Katiba na Sheria, alieleza mshangao wake kwa Rais Kikwete kuhutubia taifa kwa habari za kuambiwa, kuelezwa na kufahamishwa bila yeye kujiridhisha.

Alisema kuwa rais alimtuhumu kwa kumuita "mzushi na muongo mtupu mwenye kauli za kinafiki, fitina na uzandiki wa hali ya juu", lakini akahoji ni kwanini anawataka wapinzani wakae mezani wazungumze naye wakati ni waongo.

"Hoja zangu zilihusu Zanzibar kutokushirikishwa katika mchakato wa kuboresha muswada wa mabadiliko ya sheria, nilisema hakuna mdau hata mmoja au mtu binafsi aliyeonana na wajumbe wa kamati.

"Kwa upande wa bara kulikuwa na wadau 22, ukijumlisha na vyama vya siasa 22, hivyo bara peke yake tulisikiliza wadau 44. Je, fitina, uzandiki na uongo anauosema Kikwete upo wapi?" alihoji.

Lissu alitaja baadhi ya taasisi za bara walizokutana nazo kuwa ni Ongeza Elimu ya Juu, vyama vya siasa na watu binafsi mfano Jaji Mkuu mstaafu, Barnabas Samatta na Prof. Issah Shivji.

Alisema kuwa kwa Zanzibar walipewa ratiba ya kutembelea miradi ya Tasaf, ofisi ndogo ya Bunge na ofisi ya Makamu wa Rais, na kwamba walilalamika kubadilishiwa ratiba hiyo wakiwa Zanzibar.

"Tuliambiwa na Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashililah tungepewa fedha za kukaa Zanzibar hata kwa wiki nzima, na tulilipwa fedha nyingi tofauti na tunavyolipwa kwa utaratibu wa kawaida," alisema.

Lissu alisema kuwa Kikwete aliwahakikishia Watanzania kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ilishirikishwa, lakini Waziri wa Sheria wa Zanzibar alisema kuwa walipelekewa muswada na Mwanasheria Mkuu, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), Wiliam Lukuvi na kuwataka watoe maoni siku hiyo hiyo.

Kwamba Wazanzibari waliona mambo manne waliyopelekewa katika muswada wa mabadiliko ya sheria hayakuwa na shida wakasema sawa, lakini muswada uliopelekwa bungeni ulikuwa na mambo zaidi ya 11.

"Je, hapa kuna uzandiki? Unafiki uko wapi? Je, na waziri huyo wa Zanzibar naye ni mwongo?" alihoji.

Aliongeza kuwa Rais Kikwete katika hotuba yake alisema ‘ameambiwa', ‘ameelezwa' na ‘amefahamishwa', maneno ambayo ameyatamka mara tisa, na hivyo kuhoji inakuwaje rais anahutubia taifa kwa maneno ya kuambiwa ambayo kisheria hayana nguvu?

"Rais ana uwezo wa kukataa muswada na ana mamlaka ya kukataa mambo ya kijinga yanayopitishwa na wabunge. Tunaomba asisaini muswada huo.

"Rais wetu afanye kama Obama aliyenukuliwa siku za hivi karibuni akisema wabunge wakipitisha mambo ambayo hayana tija kwa taifa hatasaini," alisema.

Akizungumzia athari za haraka kama rais atasaini muswada huo, Lissu alisema nchi itapata katiba mbovu ya hovyo na matukio ya vurugu kama ya Zimbabwe na Kenya yatajitokeza Tanzania.

Alisema kuwa nchi hizo zilifikia hapo baada ya serikali kujidai inahodhi muswada wa katiba, ikijipendelea yenyewe badala ya kusikiliza wananchi waseme.

Kuhusu wadau ambao waliwasilisha majina halafu rais akateua kadiri alivyoona bila kuteua majina hayo, Lissu alisema hayo hayakuwa mawazo yake, bali waulizwe mwakilishi wa Baraza la Maaskofu Katoliki, Dk. Charles Kitima na Mchungaji Rohho wa CCT.

Kwa wawakilishi wa Shirikisho la Vyama Vya Wenye Ulemavu (Shivyawata), Lissu alidai kuwa walisema kuwa Alshaymar Kweygir, rais ndiye anajua alivyomteua kwani hawakumpendekeza.
 
Huyu jamaa ni mnafiki yeye si alisema muungano umevunjika sasa mambo ya kwenda Znz yametoka wapi au anatafuta "sympathy" ya wa Zanzibar.

Ukiwa na akili ndogo huwezi kumuelewa huyu jamaa kweli nakuambia. Jiulize muswada unarudi bungeni kwa hoja ya nani? Jk anajifanya kumnanga huku anatumia hoja zake kufanya maamuzi. Ajabu sana!
 
Bila KIKWETE kututajia nani alikuwa "akimwambia" na atuhakikishie kama alichanganya na "zake",tutashindwa kumtofautisha na "Mbayuwayu"
 
Bila KIKWETE kututajia nani alikuwa "akimwambia" na atuhakikishie kama alichanganya na "zake",tutashindwa kumtofautisha na "Mbayuwayu"

mkuu mimi naamini hata kama utachanganya watu wa ukoo wenu wote hamuwezi kufikia akili ya jk ni kiongozi wa pekee sana japo wapo watu ambao hawamwelewi.
 
lissu ni mwongo.mnafiki.mfitini, mzushi mzandiki first class
Na Abdallah Bulembo je? Kama Lissu ni mwongo mbona hoja zake zimekubaliwa na rais kwamba zinazungumzika na zirudishwe kujadiliwa? We mbona unataka kuturudisha nyuma?
 
Back
Top Bottom