Mlengo wa Kati
JF-Expert Member
- Feb 16, 2011
- 2,730
- 492
Naona unanjaa vipi unataka chakula gani? UMESHALIPIWA usiogope! sema tu, sisi huku tunawanunulia wote wenye njaa. HUKATWI!
Acha mipasho wewe binti
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Naona unanjaa vipi unataka chakula gani? UMESHALIPIWA usiogope! sema tu, sisi huku tunawanunulia wote wenye njaa. HUKATWI!
Huyu jamaa ni mnafiki yeye si alisema muungano umevunjika sasa mambo ya kwenda Znz yametoka wapi au anatafuta "sympathy" ya wa Zanzibar.
Huyo ni muongo tu hata aitishe press conference ya dunia nzima. TEC na CCT wameshirikishwa au hawakushirikishwa?
Akili za Bavicha upeo wako ndiyo ulipoishia.Kikwete sasa! Mnafiki, mlindwa na majini, mzandiki, mpeleka umbea majuu ndo maana Kagame kamwita 'snitch'!
Huyo ni muongo tu hata aitishe press conference ya dunia nzima. TEC na CCT wameshirikishwa au hawakushirikishwa?
Wakuu kamanda Lissu anafanya press, sasa hivi Makao Makuu ya Chadema na haya ndiyo amezungumza;
- Wadau wa Zanzibar hawajashirikishwa hata kidogo na hawakuwepo kwenye ratiba ya Kamati.
- Kamati ilipanga kwenda Zanzibar kutembea na sio kuonana na wadau, kwa sabab walitakiwa pkutembelea miradi ya TASAF, OFISI YA MAKAMU WA RAIS NA OFISI YA BUNGE.
- Wakakataa na kuomba kwa katibu wa Bunge kuwaona wadau wa Zanziba, Katibu wa Bunge alikubali.
- Walitengeneza orodha ya wadau.
- Yalianza maneno pembeni kuwa hakuna usalama Zanzibar wakati huohuo Kamati ya Ulinzi na Usalama ilikuwa Zanzibar.
- Wakazuiliwa kwenda na hivyo hakuna mdau wa Zanzibar aliyehusishwa.
- Kama haya ni makosa uzandiki na unafiki unatoka wapi wakati hoja ya kwenda Zanzibar yeye aliyeitoa?
Nitaendelea kuwapa update
- Kama hakuna ulazima kwa mujibu wa kanuni kwenda Zanzibar ofisi ndogo za Bunge Zanzibar zina maana gani, kwa hili rais amepotoka na hajui analolifanya.
- Hawajawahi kukutana na mjumbe wa Baraza la wawakilishi Zanzibar, na hata M/sheria amekiri.
UTEUZI KWENYE TUME YA KATIBA
- Hoja ni mamlaka ya Rais kuteua wajumbe 166
- Walipinga 2011 Ikaondolewa na wakairudisha tena kwenye muswada huu
- Uteuzi wa wajumbe wa Tume usilinganishwe na uteuzi wa wajumbe wa Bunge la Katiba. Ushahidi wa TEC , CCT na Shirikisho la walemavu kutoteuliwa pamoja na kupeleka majina kwa Rais ulitolewa kwenye Kamati ya Bunge, uongo wake unatoka wapi?
- Shirikisho la walemavu halikumpendekeza Al Shaimar Kwegir na hivyo Rais aliteua watu alkyewaona yeye wanafaa. Uongo unatoka wapi?
Maneno ya Rais,
- Hatamuita mzindiki, mnafiki wala mwongo ila ametoa hitimisho kwa maneno ya sikia sema (hearsay) kwa sababu ametumia maneno "nimeambiwa, nimesikia na nimejulishwa" mara tisa kwenye hotuba yake.
Kuhusu kuwa na mazungumzo ya pamoja;
- Kama ana nia njema basi asiusaini muswada na Katiba inamruhusu kufanya hivyo.
- Akiusaini ataendekeza mambo ya kiccm na hana haja ya kuaminiwa tena.
- Kamati ya Sheria na Utawala ya Bunge inakutana kuanzia kesho na hivyo anasubiri sheria husika iliyopitishwa kinyemela kurudishwa Bungeni.
Mwisho. Anakaribisha maswali;
- Ukiwa na mchakato mbovu yatatokea mambo kama ya Zimbabwa na Kenya kwa sababu mwanzoni hakukuwa na mchakato shirikishi.
- Wanachokifanya CCM sasa ndicho walichokifanya KANU kule Kenya
Hiyo kitu Lissu alipaswa kupotezea tuu, kila kitu kipo wazi, waliompa Rais habari ndo hawakumueleza hali halisi.
Huyo ni muongo tu hata aitishe press conference ya dunia nzima. TEC na CCT wameshirikishwa au hawakushirikishwa?
Lissu anashindana na tembo...
Eti analeta mambo ya "hearsay" anafikiri yuko mahakamani hapo? mijitu miongo, minafiki na mizandik tu, hata uitie ndani ya chupa itachomoa kidole.
Kweli watu wanajuwa kutafuta kura, imekuwaje leo Mh lissu aliyesema Muungano umekufa na hauna maana leo anatetea nafasi ya Zanzibar katika Muungano au ni Muungano gani huo?
KA-USHAURI KANGU KWAKO MH. Lisu, usibishane na mkuu wa kaya. Umeshamwonesha kuwa alidanganywa, sasa yeye aamue tu. Akiendelea kuwasikiliza wanaomzuga haikuhusu tena. Wewe sasa ng'ang'ania katiba mpya tu. Ndungai anajiandaa kukupinga kule mjengoni, jiulize utafanya nini kumhusu huyu ndungai kwani lazima akukomoe tu.
Kale ka simu kake alikokaficha chini ya makaratasi ya mezani ili asome meseji kutoka kwa huyo remote controla wake bado anako na bado atakatumia. Atakapo wapandisheni munkari anategemea hilo ili mtoke hayo Maccm yaupindishe tena je ukirudi na kusema hiyo ni faulo mkuu wa kaya atakusikiliza? Andaa mbinu mpya achana na kubishana na mkuu wa kaya. Ukimya si woga, ni busara pia.
Rais kasema mswada urudi bungeni,hapa huyu Mzandiki anatafuta umaarufu tu binafsi
Lissu habari ya TEC na CCT izungumze vizuri lasivyo bado unaonekana ni Mzandiki!
Tundu Lissu ni mnafiki na mzandiki tu.
Wazanzibar wenyewe wanasema hawakushirikishwa au kuna wazanzibar wengine zaidi ya Wazenji?.
Hata mzazi wako anaweza kuwa mzandiki lazima Useme ukweli! Mzandiki ni mzandiki tu! Lissu ni mzandiki aseme wajumbe wa kutoka TEC au CCT wapo au hawapo kwenye tume ya Jaji Warioba