Tundu Lissu: Tutazipima kauli za Kikwete kwenye Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala!

Tundu Lissu: Tutazipima kauli za Kikwete kwenye Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala!

Huyu jamaa ni mnafiki yeye si alisema muungano umevunjika sasa mambo ya kwenda Znz yametoka wapi au anatafuta "sympathy" ya wa Zanzibar.

Acha ujinga ndugu! Gangamala kwenye hoja. Sio mnaruka ruka nje ya hoja. Mambo ya mi-CCM na akina Bulembo usilete kwenye jukwaa la wenye akili.

Watu wanazungumza kwa FACTS na sio oohhh sijui nimeambiwa, sijui nimesikia!! Hata mahakamani ushahidi wa kusikia au kuambiwa ni ushahidi UFU.

Mwambieni Mwenyekiti wenu asiwe MZURURAJI. Ndio maana kila uchao anaingizwa MKENGE kiasi kwamba anakosa kuaminiwa na waTanganyika.

Aliomba kazi IKULU ili atumikie waTanganyika na sio kuwa mzururaji na kukaimisha taasisi ya urais. Kiasi kwamba taasisi ya urais imepoteza maana, ambapo kwamba hata Mwigulu anajiona ana faa kuwa rais.
 
Huyo ni muongo tu hata aitishe press conference ya dunia nzima. TEC na CCT wameshirikishwa au hawakushirikishwa?

kichwa chako ni kama nazi ndani kimejaa maji aisee kwani fuatilia ikibidi kamuulize majibu yapo kweli Lissu ni kiboko yenu mpaka ------ anafikia hatua ya kumtajataja kwenye hotuba yake inamaana library ya hotuba za rais ------ mojawapo ina jina la kamanda lissu, mbowe hakika maccm mmepata tiba mlidhani hii ni nccr au cuf siyo.
 
Huyo ni muongo tu hata aitishe press conference ya dunia nzima. TEC na CCT wameshirikishwa au hawakushirikishwa?

Wazanzibar wenyewe wanasema hawakushirikishwa au kuna wazanzibar wengine zaidi ya Wazenji?.
 
Wakuu kamanda Lissu anafanya press, sasa hivi Makao Makuu ya Chadema na haya ndiyo amezungumza;

- Wadau wa Zanzibar hawajashirikishwa hata kidogo na hawakuwepo kwenye ratiba ya Kamati.
- Kamati ilipanga kwenda Zanzibar kutembea na sio kuonana na wadau, kwa sabab walitakiwa pkutembelea miradi ya TASAF, OFISI YA MAKAMU WA RAIS NA OFISI YA BUNGE.
- Wakakataa na kuomba kwa katibu wa Bunge kuwaona wadau wa Zanziba, Katibu wa Bunge alikubali.
- Walitengeneza orodha ya wadau.
- Yalianza maneno pembeni kuwa hakuna usalama Zanzibar wakati huohuo Kamati ya Ulinzi na Usalama ilikuwa Zanzibar.
- Wakazuiliwa kwenda na hivyo hakuna mdau wa Zanzibar aliyehusishwa.
- Kama haya ni makosa uzandiki na unafiki unatoka wapi wakati hoja ya kwenda Zanzibar yeye aliyeitoa?

Nitaendelea kuwapa update

- Kama hakuna ulazima kwa mujibu wa kanuni kwenda Zanzibar ofisi ndogo za Bunge Zanzibar zina maana gani, kwa hili rais amepotoka na hajui analolifanya.
- Hawajawahi kukutana na mjumbe wa Baraza la wawakilishi Zanzibar, na hata M/sheria amekiri.
UTEUZI KWENYE TUME YA KATIBA
- Hoja ni mamlaka ya Rais kuteua wajumbe 166
- Walipinga 2011 Ikaondolewa na wakairudisha tena kwenye muswada huu
- Uteuzi wa wajumbe wa Tume usilinganishwe na uteuzi wa wajumbe wa Bunge la Katiba. Ushahidi wa TEC , CCT na Shirikisho la walemavu kutoteuliwa pamoja na kupeleka majina kwa Rais ulitolewa kwenye Kamati ya Bunge, uongo wake unatoka wapi?
- Shirikisho la walemavu halikumpendekeza Al Shaimar Kwegir na hivyo Rais aliteua watu alkyewaona yeye wanafaa. Uongo unatoka wapi?

Maneno ya Rais,
- Hatamuita mzindiki, mnafiki wala mwongo ila ametoa hitimisho kwa maneno ya sikia sema (hearsay) kwa sababu ametumia maneno "nimeambiwa, nimesikia na nimejulishwa" mara tisa kwenye hotuba yake.

Kuhusu kuwa na mazungumzo ya pamoja;
- Kama ana nia njema basi asiusaini muswada na Katiba inamruhusu kufanya hivyo.
- Akiusaini ataendekeza mambo ya kiccm na hana haja ya kuaminiwa tena.
- Kamati ya Sheria na Utawala ya Bunge inakutana kuanzia kesho na hivyo anasubiri sheria husika iliyopitishwa kinyemela kurudishwa Bungeni.

Mwisho. Anakaribisha maswali;

- Ukiwa na mchakato mbovu yatatokea mambo kama ya Zimbabwa na Kenya kwa sababu mwanzoni hakukuwa na mchakato shirikishi.
- Wanachokifanya CCM sasa ndicho walichokifanya KANU kule Kenya

Rais kasema mswada urudi bungeni,hapa huyu Mzandiki anatafuta umaarufu tu binafsi
 
Hiyo kitu Lissu alipaswa kupotezea tuu, kila kitu kipo wazi, waliompa Rais habari ndo hawakumueleza hali halisi.

Hapana mkuu, Rais mwenyewe aliwahi kutoa ushauri .."ya kusikia changanya na ya kwako" imekuwaje yeye amesikia kila kitu alichoongea juzi? Kama kila kitu amesikia amechanganya wapi na ya kwake? Ni vipi pale anapokuwa amepotoshwa na hivyo yeye kuonekana kituko?

Uoungozi wetu wa sasa una walakini.
 
Eti analeta mambo ya "hearsay" anafikiri yuko mahakamani hapo? mijitu miongo, minafiki na mizandik tu, hata uitie ndani ya chupa itachomoa kidole.
 
Kweli watu wanajuwa kutafuta kura, imekuwaje leo Mh lissu aliyesema Muungano umekufa na hauna maana leo anatetea nafasi ya Zanzibar katika Muungano au ni Muungano gani huo?
 
Eti analeta mambo ya "hearsay" anafikiri yuko mahakamani hapo? mijitu miongo, minafiki na mizandik tu, hata uitie ndani ya chupa itachomoa kidole.

Kikwete naye sasa! Uuuuuwwwiii! Nimeambiwa .. . . . .
Nimeambiwa . . . . . .
Nimeambiwa . . . . . .
Nimeambiwa . . . . . .
Nimeambiwa . . . . . .
 
Kweli watu wanajuwa kutafuta kura, imekuwaje leo Mh lissu aliyesema Muungano umekufa na hauna maana leo anatetea nafasi ya Zanzibar katika Muungano au ni Muungano gani huo?

Lissu anataka Tanganyika ije, wapuuzi hawataki.
 
Update:
- Pindi Chana anayesema kuwa Lissu hakuwepo kwenye kikao, aeleze yeye alikuwa wapi na kumkaimisha Ngeleja?
- Malalamiko ya TEC na TCC yalitolewa na Rev. Dr Charles Kitima, Mchungaji Rohho na mwakilishi wa Walemavu na hivyo madai hajayatoa yeye.
- Maandamano ya tar 10 yapo palepale.
- Mapolisi yanasema Rais amekataza maandamano, kwa sheria ipi inayompa Kikwete mamlaka kuzuia maandamano? Na hotuba ya Kikwete haina kitu kama hicho, kwa hiyo polisi na waongo.
- Kwa nini Rais asimuite Waziri wa Sheria Zanzibar Mzandiki?
- Rais alinukuliwa akisema ni heri Dr Slaa awe Rais kuliko yeye kuwa Mbunge, kwa manenoya sasa aliyoyasema basi kwa Tundu Lissu ni heshima kubwa kwa sababu anathibitisha aliyoyasema 2010.
- Kwa Rais kuendelea kusikiliza ya kuambiwa, ni ujinga achanganye na za kwake.
- Bungeni kipindi hiki hakutakuwa na mjadala kwa sababu hawatatoka.

Press imefungwa rasmi.

Kibaja.
 
KA-USHAURI KANGU KWAKO MH. Lisu, usibishane na mkuu wa kaya. Umeshamwonesha kuwa alidanganywa, sasa yeye aamue tu. Akiendelea kuwasikiliza wanaomzuga haikuhusu tena. Wewe sasa ng'ang'ania katiba mpya tu. Ndungai anajiandaa kukupinga kule mjengoni, jiulize utafanya nini kumhusu huyu ndungai kwani lazima akukomoe tu.
Kale ka simu kake alikokaficha chini ya makaratasi ya mezani ili asome meseji kutoka kwa huyo remote controla wake bado anako na bado atakatumia. Atakapo wapandisheni munkari anategemea hilo ili mtoke hayo Maccm yaupindishe tena je ukirudi na kusema hiyo ni faulo mkuu wa kaya atakusikiliza? Andaa mbinu mpya achana na kubishana na mkuu wa kaya. Ukimya si woga, ni busara pia.

Well said mkuu, personally sioni sababu ya kufanya press conference, watanzania was Leo so wale was zama I kanumba soul hats kama zona kasoro zake bado zimesaidia sana. Ukweli upo wazi LA msingi no kujipanga name kutengeneza strategies za kuwashinda hawa wapuuzi na wab ubunge vilaza (compliment to Ney wa Mitego)
 
Wazanzibar wenyewe wanasema hawakushirikishwa au kuna wazanzibar wengine zaidi ya Wazenji?.

Uzandiki wa Lissu upo kwenye habari ya TEC na CCT na sio habari ya zanzibar! Usilete uzandiki wa kuchanganya maneno
 
Hata mzazi wako anaweza kuwa mzandiki lazima Useme ukweli! Mzandiki ni mzandiki tu! Lissu ni mzandiki aseme wajumbe wa kutoka TEC au CCT wapo au hawapo kwenye tume ya Jaji Warioba

ila si mzandiki,,,,,,,mzandiki ni huyu anayechekea wauza unga
 
Back
Top Bottom