Tundu Lissu: Ukiwa na Rais mwizi mnawezaje kuwa salama? Katiba bora ni kuzuia Marais wezi

hizo ni ndoto za mchana huwezi kushindana na mtu anayeshika dola hata awe anapendwa kaisi gani mama anamchana mchana kweupeee watu wanarudi ikulu anabaki analalama tu huko kama mtu aliyefumaniwa akioga nje lisu hana lolote ni maneno matupu
Bila shaka ulipokuwa darasa la 3 au 4 hukusoma na kuilewa methali hii rahisi isemayo

"...siku ya kufa nyani, miti yote huteleza..."

Nyani ni bingwa wa kutembea na kuruka juu ya miti. Unaweza kusema kwenye pori la miti, nyani ndiyo maeneo yake ya kujidai.

Yaani humwambii kitu. Mtu aweza kusema "ni ngumu sana kumuua nyani kwenye pori la miti"

Yes, ni ngumu lakini kumbe anaweza kuuwawa..

Na ikifika siku yake ya kufa, miti yote humkataa (huteleza)!

Unaweza kuwa na fedha, dola, and mention anything else. Lakini ikifika siku ya kufa kwako (kutoka kwako madarakani), hayo yote yatakukataa mchana kweupe.

Roman Empire iko wapi? Utawala wa Makaburu SA uko wapi? Kina Idd Amin Dada wako wapi? Kina Adolf Hitler wako wapi? Kina Mobutu Seseseko wako wapi? Kina John Pombe Magufuli wako wapi?

Hujaelewa tu maana yake mpaka hapo?

Ndugu mihambope, ishi na furahia leo lakini huwezi kuyajua ya kesho..!!

Waache hawa waonevu waishi na kufurahia leo.

Labda wanaweza kusema kama usemavyo wrwe kuwa, "hiyo ni ndoto ya mchana".

Utashangaa mno kuja kujua kumbe hata ndito za mchana, hutoa ujumbe wa ukweli..!

Mwisho wao upo na unakuja kama tufani..
 
Nadhani wataishia kupata kura za ndugu zao pekee...........Lissu ni genius, jamaa anajua na ana uwezo mkubwa wa kushawishi raia kuliko CCM wote combined.
 
Haya mambo muwe mnawasimulia wajinga na mbumbumbu.

Kila mara Huwa nawaambia Katiba Mpya haijawahi zuia watu kuiba Wala haileti ugali mezani.

Mfano mzuri ni Kenya na Ghana Wana Katiba Mpya na wizi,ugumu wa Maisha,Ufisadi nk vinaendelea kama kawa aheri ya Tanzania πŸ‘‡πŸ‘‡


Watu wajinga na mbumbumbu ndio hutumiwa na Wanasiasa Kwa Ajili ya kufika wanapotaka ila mwisho wa siku nawahakikishia mtaandamana na mtaishia hivyo hivyo hakuna kitakachobadilika,kawaulizeni Ma hustler wa Kenya.
 
Bila shaka mjinga na mbumbumbu hapa ni wewe. Jisome na jisikilize kwa makini tena, utagundua kuwa wewe ndiye mjinga na mbumbumbu...!!

Nakushauri kabla hujaamua kusema kitu mbele ya hadhara kujibu hoja ya mtu mwingine, basi jifunze kusikiliza kuhakikisha umeelewa ulichosikia kwanza..

Kwa hili mimi nina hakika kabisa kuwa ume - comment out of your ignorance bila hata kusikiliza na kuielewa mantiki ya hoja ya Tundu Lissu..

Bila shaka wewe ChoiceVariable ni miongoni mwa wale "wajinga" wenye hoja za kijinga kama vile eti "katiba haikuletei chakula mezani, au maji, au haikujengei barabara au shule"
=============================================
BACK TO THE TOPIC:

Umekurupuka ndugu.

Kwani mantiki ya hoja ya "wizi ya ma - Rais wetu" haiko ktk namna ulivyoielewa wewe..

Bali Tundu Lissu anajua fika kuwa binadamu kiasili ni mwizi. Lakini inawezekana kutengeneza mfumo wa kuidhibiti (control) asili hii ya wizi wa mwanadamu huyu kwa kutengeneza sheria nzuri za udhibiti. Kwa hili linawezekana kwa kutengeneza mfumo wa kisheria na kikatiba unao - limit matendo ya wizi ya hawa ma - Rais..

Mfumo wa kisheria na kikatiba ambao hampi kinga ya kutoshitakiwa kiongozi awaye yeyote kwa makosa yake anayotenda. Kwamba yeyote anayevunja sheria au katiba kwa kujiingiza kwenye jinai ashughulikiwe kwa mujibu wa sheria na katiba bila kujali nafasi na cheo chake, awe ni Rais au waziri na hata mfalme..!!

Na maswali unayopaswa ujiulize wewe ndugu ChoiceVariable halafu ujijibu mwenyewe ni hayaπŸ‘‡πŸ»πŸ‘‡πŸ»

1. Je, hivi ndivyo ilivyo hapa kwetu Tanganyika?

2. Je, si kweli kwamba karibu viongozi wakuu wote wa nchi hii wenye dhamana ya kusimamia rasrimali za nchi yetu wamejwekea kinga ya kutoshitakiwa katika mahakama yoyote kwa uovu wao wowote wataotenda?

3. Sasa kwanini watu hawa wasiibe na hata kuuza nchi na wananchi wake kwa nchi za kigeni Ulaya, Amerika na Uarabuni?

4. Huo ufusadi wa Ghana na Kenya unaotumia kama kigezo cha utetezi wa wendawazimu unaoendelea hapa nchini kwetu unajua umeshughulikiwaje kwa mujibu wa sheria na katiba zao?

β€ŠNB:
SIKIA BWANA
: Tundu Lissu anaeleweka vizuri sana. Anafungua ufahamu na akili za watu kuliko kawaida tofauti na unavyodhani. Huwezi kuua hoja zake kwa propaganda zako uchwara..!

Na kama unataka kujibu hoja zake, nakupa changamoto moja, kuwa JIPANGE VIZURI, usikurukupe usije kuonekana kituko katikati ya waungwana..

Na muhimu zaidi ni jifunze kumsikiliza kwa makini kisha m - challenge kwa kujibu hoja ili hadhira isikuone mjinga na mpumbavu.

La unamuona Tundu Lissu kuwa ni mwendawazimu, then unahangaikia nini kutafuta habari zake?
 
La unamuona Tundu Lissu kuwa ni mwendawazimu, then unahangaikia nini kutafuta habari zake?
Umemjibu vizuri sana huyo 'Choice...', lakini hawez (la hasha, HATAKI)i kuelewa; kama wasivyotaka kuelewa wote wanaofaidika na Katiba hii iliyopo sasa na hawataki kusikia chochote juu ya Katiba Mpya.

Lakini, bado pia nina wasiwasi juu yako, pamoja na kutoa majibu mazuri sana kwa huyo mtu, kama kweli unaamini uwepo wa Katiba Mpya, na sheria nzuri, ndiko kutakakoondoa uozo tuliofikia hapa kwetu.
Hata pakiwepo na 'mfumo' mzuri unaozuia rushwa na uchafu mwingine wowote, lakini wanaousimamia mfumo huo hawana dhamira ya dhati ya kuufanya ufanye kazi, bado matatizo yatakuwa palepale.

China hawana Demokrasia, kama tunavyoimbishwa hapa na kwingineko uzuri wa kuwa na Demokrasi.
Wachina (raia wa kawaida), kama tulivyo kwisha wajuwa kwa kuishi nao hapa kwetu, ni watu wenye tabia ya ukwapuzi sana. Wako tayari kuzoa kila kitu ukitazama pembeni na kuwaachia wao wafanye bila ya kuwachunga vizuri. Hawa hawa wachina, huko kwao hawathubutu hata kuiba kuku wa mtu...; sasa nikuulize, kwa nini iwe hivyo.

Hivi juzi juzi mwana mama mmoja tajiri mkubwa Vietnam, Truong My Lai (bilionaire wa Real Estate), pale Vietnam kapewa hukumu ya kunyongwa kwa utapeli mkubwa aliokuwa akishiriki katika shughuli zake za kibenki. Hii inaashiria kwa yeyote, kuwa ukishiriki kwenye rushwa na ufisadi, mwisho wako hauwi salama.

Kwa hiyo, uwepo wa Katiba na sheria nzuri, ni mwanzo mzuri, lakini siyo mwisho wa tatizo. Dawa ni kuhakikisha kwamba Katiba hiyo na sheria hizo zinafanya kazi sawasawa.
Huo mfano wa Kenya na Ghana, aliokupa huyo chawa 'Variable', ni sahihi kabisa, kwa sababu hakuna utekelezaji wa matakwa ya Katiba hizo na sheria zake, hasa katika eneo hilo la ukwapuzi wa mali za umma.
Kenya na Ghana wanaweza kuwa wametumia hizo Katiba zao kwenye maswala mengine, kama chaguzi; lakini hao wanaochaguliwa kuingia madarakani, wanaziweka pembeni kuhusu maswala ya wizi na takataka nyinginezo. Kwa bahati mbaya, hatujaona katiba hizo zikitumiwa na wananchi kuwawajibisha hawa viongozi wapya kwa kushindwa kuzisimamia Katiba zao.
 
Watu wajinga na mbumbumbu ndio hutumiwa na Wanasiasa Kwa Ajili ya kufika wanapotaka ila mwisho wa siku nawahakikishia mtaandamana na mtaishia hivyo hivyo hakuna kitakachobadilika,kawaulizeni Ma hustler wa Kenya.
Bahati mbaya sana, wewe mwenyewe hujatoa njia mbadala kwa sababu unafaidika na kilichopo sasa. Huu ndio ubinafsi unaowaharibu nyote mnaojiita 'chawa'.
 
Ameyaona au kaota haya.. wezi lini tena!!!!
πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…

Kazi iendelee...
Muwe mnafuatilia au hata kujisomea kabla ya kuingia kwenye mjadala. Na usikute wewe ni Mbunge au kiongozi fulani mkubwa tu huko CCM lakini huna maarifa na ufahamu ktk kichwa chako...

1. Rais Benjamin Mkapa - Alitumia mamlaka yake ya Urais mwaka 2004/2005 kuwezesha kuiba toka BoT USD 100M sawa na zaidi ya Tshs 133bn Ili zi - facilitate kampeni za CCM ktk uchaguzi mkuu wa 2005 uliomwingiza Jakaya Kikwete (CCM) madarakani. Mkapa kaandika na kukiri ndani ya kitabu chake - MY LIFE, MY PURPOSE alichokiandika kwa mkono wake mwenyewe...!!

2. Jakaya Mrisho Kikwete - Mwaka 2008 aliiba au kuwezesha kuibwa kwa fedha zaidi ya Tshs 130bn kupitia mkataba hewa wa kampuni hewa (Richmond) na kuishia kumtoa kafara waziri wake mkuu wakati huo hayati Edward Lowassa..

Aliiba au kuwezesha kuibwa kwa fedha zaidi Tshs 300bn toka BoT katika skendo maarufu mwaka 2013/2014 inayojulikana kama Tegeta Escrow Account..

3. John P. Magufuli: Mara baada ya kifo chake mwaka 2021, inasemekana (still disclosed infos) kiasi cha USD 40M sawa na karibu TZS 970bn kilikutwa nyumbani kwake Chato. Unadhani hizo ni mishahara yake? Kama ni kweli (na 99% yaweza kuwa kweli) maana yake huyo alikuwa mwizi tu pia..!

5. Samia Suluhu Hassan: Inasubiriwa lakini unadhani kwa kugawa bandari zetu bure, kugawa mamilioni ya ekari za misitu yetu na kugawa mbuga zetu za wanyama Loliondo, Manyara na Ngorongoro sisi Watanganganyika kwa shoga zake wa Uarabuni unadhani kapewa nini yeye na CCM yake?

Tutajua tu specific alipewa nini hata kuwa loose kiasi cha kuipiga bei Tanganyika akiiacha Zanzibar nyumbani kwao..
 
Asante sana Mh. Tundu Antiphas Lissu, taratibu Watanganyika watazinduka na kuelewa kile unachokipigania kwa niaba yao. Ujumbe wako murua unafuatiliwa na kujadiliwa na wengi ingawa wapo wengine ambao, kwa ujinga, unafiki na uoga wao, wameweka pamba masikioni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…