Tundu Lissu, vita na Wasafi hutoiweza, utagalagazwa wewe na chama chako

Tundu Lissu, vita na Wasafi hutoiweza, utagalagazwa wewe na chama chako

sio "mume" sema "mmedandia gari kwa mbele"...BURNA BOY KWA AFYA YA JAMII
Hayo mambo tulishayaacha huko zamani sasa hivi music,michezo ni biashara hivyo diamond, music unamalengo makuu matatu kuelimisha,kuburudisha na ajila sasa mtu ukichagua music kama ajila kuna ubaya gani? , wakina roma na ney wamechagua music wa uhanaharakati na kuelimisha kwani kuna ubaya gani tubadilike.
 
Kwanza nyimbo zake za kitandani tu hazina lolote la kujifunza. Kmawe kura yangu siwezi kuwapigia wahuni. Angekuwa Christina Shusho ningempa kura.
Ujitambui wewe, malengo makuu ya music (1)Ajila (2)burudani (1)kuelimisha yeye amechagua muziki kuwa ni ajila.
 
Tundulisu si mungu wala malaika kwamba kila hoja yake iwe ya kusapotiwa na kila mtu,kama yeye alivyotembea nchi yote kuomba kura na ndivyo diamond anayo haki kuomba kura, na hoja ya kwamba analazimisha na uzalendo imetokana na baadhi ya wenye chuki na diamond kusema hawatompigia kura ndipo hao watetezi wa uzalendo walipoibuka lakini ukweli husiopingika no kuwa watu wanachuki binafsi na diamond kwa sababu za kibiashara,siasa na muziki kitu ambacho ni kawaida sana kwenye maisha lakini chuki zingebaki moyoni na sio kuanza kampeni kabisa kushawishi watu wasipige kura wazi wazi ni ujinga na aibu ikizingatiwa hiki si kipindi cha uchaguzi ni masuala ya burudani.
Mkuu niwapi Tundu lissu kasema tusimpigie kura Dangote? Tundu anamjibu Goodluck kwamba asilazimishe upendo..ana sissitiza kua uzalendo sio kuunga mkono kila kitu hata kama ni kiovu...anasema Chibu hajawahi simama kwenye haki...maanake chibu anafata maslahi binafsi...pia kasema hata yeye yaani yeye Tundu sio muumini wa Dangote..

Hebu nambie ni wapi kasema tusimpigie kura Dai..au wapi kasema wafuasi wachadema tusipige kura....

Hebu rudi kipindi cha JK kwani Dai hakusupport Chama pendwa!!!!!! uliwahi sikia kiongozi wa upinzani aliinua neno la kusema wazi kua haungi mkoni kundi flani la wasanii? na umejiuliza kwa nn kasema sasa..

Je uliwajiuliza kwa nn Roma alivyotekwa hao wasanii wako walikaa kimya..!!!!!

Kwahiyo acheni kuchanganya siasa na mambo binafsi...

Pumba kubwa kuna mtu hapo juu kafikia kusema eti Biyonce alisapoti Clinton na Trumpa akashinda...hapo unajiuliza huyu anawaza kwa kutumia nn?
 
Ningekubaliana na Lissu kama sababu za kutomuunga mkono Diamond zingekuwa ni performance ya kimuziki.Lakini kusema mtu yeyote ambaye yuko tofauti na CHADEMA sio mpenda haki huko ni kupotoka.
Ni wapi Lissu amesema shida yake ni kwamba Diamond "Yuko tofauti na CHADEMA"?

1622723882141.png


Lissu ameongelea "kusimama kwenye haki", unaweza kuwa tofauti na CHADEMA na bado ukasimamia haki
 
Lissu nakushauri kabisa achana na habari za Diamond maana vita yake hauiwezi. Diamond anafanya sanaa na anawapa watu burudani.

Team Wasafi ni jeshi kubwa na likishambulia linashambulia kama waveitnamu.

Yeye kuchagua chama cha CCM chama cha watoto wa mjini, kosa lake mpaka wewe na wafuasi wako wa Chadema kumshambulia mitandaoni ni lipi?

Mnahubiri haki ila haki ya wenzenu kuchagua wanachopenda hamuitaki. Huu mbona ni udikteta sasa, siku mkipewa nchi watu wasiounga mkono chama chenu hakuna rangi wataacha ona hapa. Hamna polisi hamna jela ila mnataka kila mtu aamini mnachoamini kwa mabavu akiwa tofauti ni adui.

Beyonce alimpigia Hillary Clinton kampeni za kufa mtu ila Trump akachukua nchi, Trump akumgeuza Beyonce adui wala Republican hawakuanzisha vita na Beyonce kwanza full unyamwezi yani Beyonce support bila kujali vyama.

Lissu na viongozi wa huko dizaini yako mnafanya vijana wa kisasa wasivutiwe na Chadema. Yani kwa kifupi mnatuonyesha nyie sio watu poa, kwenu huko ni vurugu, visasi, ukamanda, usela nnya ndio umejaa mpo so harsh 😖😖 mnayafanya maisha kama kitu kigumu sana.

Huyo Ney wenu mnaemsifia mkumbuke jina halisi ni Elibariki wa kulekule sasa kwanini asiwe Chadema.

Hili ni onyo Lissu fanya siasa zako na kina Polepole achana na Wasafi kama unahitaji kuungwa mkono na watoto wa mjini.


Yaani uelewa wako bado mdogo sana kusema ukweli tangu lini kumekuwa vita! sasa ukibisha ukweli utaonekana mjinga. Halafu hizi media ziko overrated hiyo Wasafi hata Tanzania kuna vyombo vya habari bora zaidi vingi tu!!!. Hii ni kampuni tu lakini bado sana hapo itakapo kuwa media company ya EA nzima ndiyo tutaweza kusema lolote sasa ni sehemu ya kuongea uzushi na umbeya tu kwa vijana
 
Wewe huelewi hata msingi wa hoja hii, Diamond ana uhuru wake wa kushabikia ccm haina shida, tatizo linakuja ni watu kulazimisha kwenye hiyo tuzo ya BET watu wampigie kura wote, chadema tumesema hatumpigii kwa kuwa kama msanii alishirikiana na watesi wetu na hakukemea maouvu ya dhahiri ya uvunjifu wa haki za watu, ndiyo msimamo wetu ninyi lumumba mpigieni , sisi hatumpigii mwimba nyegezi,Period.
Lissu anataka Diamond awe kama Nay wa mitego au Bob Marley ndio angemsapoti, yani ni kwamba chadema waislamu wasiswalishwe nyuma ya imamu ambaye ni ccm wanataka imamu awe kama Shehe Ponda.

Sasa hapo ndio kwenye tatizo kwa maana uhuru wa Diamond kushabikia ccm kwa chadema huo ni uadui.
 
Atahitaji kura za wananchi, acha ujuha wewe
Mwendazake kawaachia akili chafu.
Kura za wananchi wapi?

Maana yeye wanachi ni wale wlio chadema tu!

Alafu nilishakwambia hiyo mimba aliyokuachia mwenda zake inayokufanya kila kitu umtaje ilete huku mimi niileee ili umsahau.
 
Wangejifunza toka kwa wanamuziki wa congo walishindwa kufanya show yeyeto ulaya kwa vikwazo vya macombatanti, sababu ya kumsapoti dikteta Kabila.Watawala wanapita wananchi wanaishi.
 
Dhalimu magufuli hakushinda kwenye Rais bora wa Afrika pamoja na maccm kukesha usiku kucha karibu kila siku kumpigia kura mtandaoni. Rais wa Ghana aliyekuwa chaguo la Twitter Republic ndiye aliibuka mshindi.
Ccm wote wakiungana kumpigia atashinda tuzo.
 
Kwanza nyimbo zake za kitandani tu hazina lolote la kujifunza. Kmawe kura yangu siwezi kuwapigia wahuni. Angekuwa Christina Shusho ningempa kura.
Sasa muulize Lissu anajifunza nini kwenye nyimbo za Nay wa mitego ambazo anaimba maisha mafupi anakula ujana? muziki ni burudani ndio maana unaweza kusikiliza wimbo hata kwa lugha usiyoielewa na bado ukaburudika, sasa hayo ya kuelemika sijui yanatoka wapi.
 
Wangejifunza toka kwa wanamuziki wa congo walishindwa kufanya show yeyeto ulaya kwa vikwazo vya macombatanti, sababu ya kumsapoti dikteta Kabila.Watawala wanapita wananchi wanaishi.
Wakati hao akina Diamond wanafanya show kwenye kampeni za ccm watu si walijaa hadi mkawa mnasema wanategemea wasanii kwamba watu wanafuata wasanii tu?
 
Lisu tukimuonya pia kwamba tabia yake ya kupiganiwa urais wake na amsterdam mtu wa nje ya nchi anawapoteza watz wengi maana watamuona anatumiwa na mabebru.

Hili la diamond, akumbuke kwamba kuna mashabiki kibao wa diamond anao huko chadema, sasa hizi chuki zake kwa diamond haoni kama anawagawa watu wake?

Hivi inakuwaje chadema ile ya dr slaa imekuwa mrenda mrenda kiasi hiki?
Uzuri watu wanajua kutenganisha burudani na haki, wanaccm ndio huwa hawajui kutenganisha haya mambo. Pigeni propaganda mtakavyo ila Diamond hapewi kura na wapenda haki kwani ameamua kujiunga na kundi la watu waovu wa ccm fullstop. Anejiona shabiki wa Diamond asiipe kura cdm.
 
Uzuri watu wanajua kutenganisha burudani na haki, wanaccm ndio huwa hawajui kutenganisha haya mambo. Pigeni propaganda mtakavyo ila Diamond hapewi kura na wapenda haki kwani ameamua kujiunga na kundi la watu waovu wa ccm fullstop. Anejiona shabiki wa Diamond asiipe kura cdm.
Hata ukiwa malaika ukajiunga na shetani wewe ni shetani, kama alijiunga na watesi wa kupinga haki za watu naye ni mtesi tuu hastahili kupewa na wanachadema, ccm wampe
 
Ndiyo apambane na UNAFIKI wake wa kukaa kimya kuhusu maovu ya Watanzania wakati huo huo kukemea maovu dhidi wa Wanigeria.
Kwa utawala ule wa jiwe Nan angezubutu kwenda kinyume ....angepoteza kila kitu kina Roma na ney hawakuwa na Mali yoyote yakutisha kuogopa jpm ..hvyo diamond alisoma upepo wa kisiasa

 
Sio kila atachosema Lissu ndio kifuatwe na kila mtu, na sio kila anayekuwa kinyume chake anakuwa mhaini, akili kama hizi, ndio udicteta,

Lissu aamini anachoamini, na sio kulazimisha wengine kuamini anachoamini kwamba ni sahihi

Tutakuwa Taifa la kijinga Sana kama wote tutakuwa kama Lissu ama kama mawazo ya Wana chadema

Daimond atapigiwa Kura na Watanzania wapenda mziki na sio wanachama wa Chama cha awaye yote, mwanasiasa kuingia malumbano na mwanamziki, ni ujinga mtupu, Kwanza ieleweke, Lissu na Daimond ni watu wawili tofauti, na kila mmoja ako na mtazamo wake na focus zao ni tofauti

Halafu ukweli mwingine ni kwamba, Lissu Kwa namna yoyote Ile na Kwa Hali yoyote Ile, hawezi kumfikia Daimond kiuchumi na pengine kiushawishi hawezi, Ila atamzidi kielimu n.k

Kwa hiyo, niungane na mwandishi kuwa, Lissu ameamua kucheza Ngoma asiyoiweza
 
Simtetei Tundu Lissu wala Simtetei Daimond ila nadhani hili swali lisichukukiwe kisiasa na wanasiasa hawapaswi kuingilia kwa itikadi zao bali mashabiki waamue wenyewe, au watanzania waamue wenyewe ingawa daimond hakusimama kutete haki pale alipohitajika lakini sioni sababu ya wanasiasa kuhamasisha wananchi, nadhani mashabiki wenyewe tuna akili timamu za kuamua kumpigia burna boy kijana wa njombe
 
Uzuri watu wanajua kutenganisha burudani na haki, wanaccm ndio huwa hawajui kutenganisha haya mambo. Pigeni propaganda mtakavyo ila Diamond hapewi kura na wapenda haki kwani ameamua kujiunga na kundi la watu waovu wa ccm fullstop. Anejiona shabiki wa Diamond asiipe kura cdm.
Na Diamond atashinda hii tuzo asubuhi na mapema.

Nyumbu hawawezi kumzuia
 
Back
Top Bottom