mwanamwana
JF-Expert Member
- Aug 1, 2011
- 1,309
- 4,798
Tundu Lissu Makamu akizungumza kupitia clubhouse leo Desemba 23 amesema kuwa
"Nimepewa taarifa na mtu wa heshima sana kuhusu maandalizi ya vurugu kwenye uchaguzi.
Kuna watu wanaandaliwa waje waingie ukumbini kama wanachama, kumbe wapo kwa kazi maalum ya kutorosha masanduku ya kura, watakapogundua kwamba mambo ya upande wao hayako sawa na mhusika amenidokeza kwamba, vyovyote itakavyokuwa, tuhakikishe uchaguzi unafanyika wakati wa mchana na ameonya uchaguzi usifanyike usiku kwa sababu kuna possibility ya wenzetu kuzima taa zote ili kufanikisha utoroshaji wa kura ama kuingiza ndani kura feki.
Tafadhari hizi tumezipokea; lakini Katibu Mkuu wa Chama anapaswa kutoa ufafanuzi kuhusu huu mchakato wa uchaguzi utakavyokuwa ili kuhakikisha unakuwa huru na wa haki".