Tundu Lissu: Wanaweza kuzima Intaneti kwa muda lakini sio kuzuia teknolojia

Tundu Lissu: Wanaweza kuzima Intaneti kwa muda lakini sio kuzuia teknolojia

Hii ni aibu sana kwa Mamlaka zilizoidhinisha mambo haya ya kishamba, hata baada ya Mwendazake kuondoka.

Kuzima mitandao kwa miaka hii ya kileo ni njia ya kienyeji mno. Huwezi kuzuia watu kusikia jambo kwa kuzima mtandao, ni LAZIMA UTASHINDWA NA KUAIBIKA TU .

Kiko wapi sasa?
 
Pongezi kwa serikali yangu tukufu,kuliko kiruhusu taifa letu linajisiwe Ni Bora wanefanya vyema kuzima mitandao .

Eti anahutubia taifa,huyu mtu yuko siriazi au hazijatimia?
 
Ajabu sana, nimejaribu kufungua twitter mida fulani ikagoma, nikahisi labda ni tatizo la network, kumbe system ya CCM bado inacheza michezo yao ya kishamba.

Kwa hili naamini sio Magufuli alieagiza twitter izimwe wakati wa uchaguzi mkuu, ni hiyo system primitive ya wasiojulikana ndio bado iko kazini.
 
Kweli nchi hii 2015 walipewa washamba sana. Hotuba iko kwenye www utaizuiaje? Atazima mtandao mpaka lini? Kitu kikishaingia kwenye net ndio basi tena. Wanasema hata uki-delete bado kitakuwemo tu!! Hoja haipigwi rungu. Hoja upigwa kwa hoja. Waandae hoja, wasiandae marungu.
 
Ukimwambia mtoto afungue vyumba vyote ila chenye alama Y usijaribu basi mtoto huanza na hicho chenye alama Y.Wanafanya watu kutaka kujua kunani.
Hii ndiyo kanuni ya "kumtungia binadamu sheria"...

Yaani, kwa kadiri unavyokaza sheria, ndivyo ambavyo mbinu za kuvunjwa sheria hizo zinavyobuniwa na kutiwa nguvu kuliko hata nguvu ya sheria yenyewe...!!
 
Back
Top Bottom