LGE2024 Tundu Lissu yuko sahihi, mfano Kilosa Kuna Vijiji 138 CHADEMA ina Wagombea 70, Kuna Vitongoji zaidi ya 800 CHADEMA ina Wagombea 200!

LGE2024 Tundu Lissu yuko sahihi, mfano Kilosa Kuna Vijiji 138 CHADEMA ina Wagombea 70, Kuna Vitongoji zaidi ya 800 CHADEMA ina Wagombea 200!

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Mchengerwa afumbia macho wahuni wakurugenzi walioteka nyara mchakato wa uchaguzi wa serikali ya mitaa 2024 walioamua kuwaengua wagombea

08 November 2024

Mchengerwa: Mgombea asiyeridhika na uteuzi akate rufaa​


View: https://m.youtube.com/watch?v=yBMTHBdD0T0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mohamed Mchengerwa amewataka wanaodai kuenguliwa katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa kuacha kulalamika pembeni badala yake watumie siku mbili zilizowekwa kikanuni kuwasilisha malalamiko yao.

Mbali na hilo, Mchengerwa amewataka wasimamizi wasaidizi katika maeneo yote kuhakikisha wanatenda haki na kuzingatia misingi ya 4R kama ambavyo kanuni, taratibu zilivyotoa miongozo ya nini cha kufanya.

Akizungumza na waandishi wa habari Dodoma leo Novemba 8, 2024 amesema zipo siku mbili za kupokea changamoto na malalamiko mbalimbali, kupitia taratibu ambazo wagombea wanatakiwa kuzifuata
 
katika ubao wa matangazo ili wagombea wawekewe pingamizi ikiwa lipo, na pia mkurugenzi au TAMISEMI haina mamlaka kisheria kuengua, kuweka pingamizi kwa wagombea asisitiza Tundu Lissu...

Sasa hawa wagombea wetu wamewekewa pingamizi na nani kwa siri kuu? ...

Muhuni wa Kilosa aliyejichukulia mamlaka badala ya wagombea wa CCM kuweka pingamizi dhidi ya wagombea wenzao wa CHADEMA ajitetea,


View: https://m.youtube.com/watch?v=MRNp4n_r5a0
Mkurugenzi Mtendaji DED wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa Ndg. Michael John Gwimile ambaye pia ni msimamizi mkuu wa uchaguzi wa serikali za mitaa 2024...
 
Msimamizi wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji Tarime ambaye ni mkurugezi DED Bi. Gimbana Ntavyo katika picha akiwa katika kikao kazi cha kawaida,

1731099939024.jpeg


Wakaazi wazungumza mambo yalivyo uchaguzi wa serikali za mitaa...


View: https://m.youtube.com/watch?v=7v7kCVHcuMs
 
..ok.

..Ccm 3200 mil.

..Cdm 100 mil.

..maana yake Ccm wakisimamisha wagombea 32, Cdm inaweza kusimamishwa mgombea 1.

..hata kama ulipata zero form 4 kama Mama Abduli utaelewa hisabati ndogo hapo juu.🤣
Mbona kuna Vyama vingi tu havina Ruzuku lakini vimesimamisha Wagombea Kibao 😂😂😂
 
Huu ndio utoto wa akili yako, au niuite uchizi.
Lissu huyo ndiye aliye sema hata hao wachache wa CHADEMA wanyimwe HAKI?
HAKI yao iko pale pale Vigezo na masharti kuzingatiwa 😄
 
Moja ya Sifa kuu ya Tundu Lissu ni Mkweli

Alisema CHADEMA bado haijawa na Wagombea wa kutosha kuikabili CCM

Hiyo imejionesha kwenye wilaya karibu zote

Mfano mzuri ni Kilosa Vijiji 138 Chadema ina wagombea 70 tu

Vitongoji zaidi ya 800 lakini Chadema ina wagombea 200 na ushee tu

Safari bado ni ndefu 🐼
Harafu wanadai wanataka kushika Dola ,hiyo Dola wataishika Kwa utaratibu gani? Hicho chama ni Cha matapeli ndio maana watu hawako tayari kuwafadhili kifedha.

Mwisho Tamisemi waacheni wagombea wa Upinzani washindane Kwa fair ground ,ccm haihitaji mbeleko mpaka hapo imeshinda.
 
Mkurugenzi wa Serengeti

9 November 2024
SABABU za WAGOMBEA WOTE CHADEMA SERENGETI KUENGULIWA - MKURUGENZI na MWANASHERIA WAFICHUA...



View: https://m.youtube.com/watch?v=afXE40-8t00
Uteuzi wa wagombea wilaya ya Serengeti wameenguliwa kwa sababu zifuatazo mkurugenzi DED na mwanasheria wa halmashauri ya Serengeti
  • Kujidhamini
  • Hawapo kwenye daftari la mkaazi la mtaa
  • Mihuri iliyotumika katika barua za wagombea
  • Kushindwa kutimiza vigezo
  • Ukataji rufaa kanuni ya 18 ngazi ya chini kwa msimamizi msaidizi ngazi ya kata na wilaya
  • N.k
 
Moja ya Sifa kuu ya Tundu Lissu ni Mkweli

Alisema CHADEMA bado haijawa na Wagombea wa kutosha kuikabili CCM

Hiyo imejionesha kwenye wilaya karibu zote

Mfano mzuri ni Kilosa Vijiji 138 Chadema ina wagombea 70 tu

Vitongoji zaidi ya 800 lakini Chadema ina wagombea 200 na ushee tu

Safari bado ni ndefu 🐼
Utawekaje wagombea mahali ambapo wananchi hawajaukubali upinzani,waoga kupindukia,wanaogopa kuvunjwa miguu.
 
Chama cha ADA- TADEA mkoani Arusha

9 November 2024
MWENEZI wa TADEA TAIFA AWAPASUKIA TUME ya UCHAGUZI BILA WOGA - MAJINA ya WAGOMBEA WAO KUKATWA...


View: https://m.youtube.com/watch?v=BQpZfiC5LRw

Katibu mwenezi taifa wa chama ADA-TADEA Bw. Zuberi Mwinyi abainisha kuwa viongozi 93 wamekatwa nchini kote na kama chama wameandika barua kupinga kuenguliwa wa wagombea wao kwa kisingizio shughuli yake ni mjasiliamali, kuandika nafasi mwenyekiti badala ya uenyekiti

ADA TADEA imesimamisha wagombea 520 nchi nzima ...
 
9 November 2024
CCM ARUSHA WALIA na kulaani TUME ya UCHAGUZI HURU - WAWAKILISHI WAO wa SERIKALI za MTAA WAKATWA MAJINA...


View: https://m.youtube.com/watch?v=snTQVvXaxS0
Msimamizi msaidizi ngazi ya mtaa wamewaengua na kutowateua wagombea wa CCM ngazi ya mtaa serikali za mitaa ...

CCM yaomba wasimamizi wasaidizi kurejea maamuzi yao na kama haki haitapatikana CCM itakwenda ngazi ya juu ya kamati ya rufaa ngazi ya wilaya ili wagombea wa CCM walioenguliwa wapate haki yao asema katibu muenezi wa CCM wilaya ya Arusha
 
09 November 2024

Mtaa wa Mtambani,
Kata ya Mzimuni, Kinondoni
Dar es Salaam

ACT Wazalendo wapiga kambi Ofisi ya Mtendaji kupinga kuenguliwa



View: https://m.youtube.com/watch?v=QcxgZcJIKMc
Inadaiwa msimamizi wa uchaguzi alifunga ofisi hadi saa tano asubuhi wakati kanuni ilitakiwa awepo ofisini saa mbili ya asubuhi na kupotea, kisha baadaye kurejea saa 6 mchana na askari polisi kupokea barua za mapingamizi ...

Madudu mengi wajitokeza wasimamizi wasaidizi wengi hawaelewi kanuni na mamlaka yao ili kutekeleza haki bila kujali vyama .... wakosoa serikali kujikita sababu zisizo za kweli kudai kukosea ujazaji fomu ...
 
09 November 2024

Serikali Imepanga na Kutekeleza Njama Kuhujumu Wagombea wa ACT Wazalendo, HAIKUBALIKI


View: https://m.youtube.com/watch?v=4WMBRZPpa3A
Kiongozi wa ACT-Wazalendo Bi. Dorothy Semu ... wagombea wetu wengi wamenyimwa nafasi ya kugombea uongozi kwa kuenguliwa na takwimu zinaonesha asilimia 60 ya wagombea wa ACT Wazalendo wameenguliwa kwa sababu zisizo za kikanuni bali za kisiasa na hivyo ACT Wazalendo inamuomba rais Samia Hassan kuingilia kati ili ufumbuzi wa kisiasa upatikane wagombea wetu waweze kushiriki uchaguzi wa 2024 wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji nchini Tanzania ametoa rai hiyo kiongozi huyo wa ACT-Wazalendo .
 
Ukubwa wa ACT Wazalendo Kigoma wadhihiri

View: https://m.youtube.com/watch?v=X39XiI7SRDA
tumezunguka kata zote 139 za mkoani Kigoma na tunashiriki kindakindaki uchaguzi wa serikali za vijiji, vitongoji na mitaa hayo amesema kiongozi wa ngome ya vijana ACT Wazalendo Abdul Nondo, na kiongozi mstaafu Zitto Kabwe walipotembelea maeneo Kagunga n.k mkoani Kigoma kuonesha utayari wa kushinda uchaguzi wa serikali za mitaa 27 November 2024

BREAKING NEWS 9 November 2024
1731165881814.jpeg
 
Chadema sio c
Moja ya Sifa kuu ya Tundu Lissu ni Mkweli

Alisema CHADEMA bado haijawa na Wagombea wa kutosha kuikabili CCM

Hiyo imejionesha kwenye wilaya karibu zote

Mfano mzuri ni Kilosa Vijiji 138 Chadema ina wagombea 70 tu

Vitongoji zaidi ya 800 lakini Chadema ina wagombea 200 na ushee tu

Safari bado ni ndefu 🐼
CHADEMA sio Chama dola. Baada ya matukio ya hivi karibuni wako ambao watasita kujitambulisha na chama chao. Wao wanatakiwa wagombee katika majimbo ambayo wana matumaini na watu wana muamko nao.

Hata Marekani Republicans na Democrats hawagombee katika majimbo yote.

Amandla...
 
AHADI KEMKEM ZA SERIKALI YA CCM

March 2024
KINANA AHUTUBIA MKUTANO MKUU wa ACT - WAZALENDO - ATOA AHADI ya RAIS SAMIA MBELE ya ZITTO KABWE...


View: https://m.youtube.com/watch?v=ias34Vw-hoc

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, kanali mstaafu Abdulrahman Omar Kinana amewahakikishia Watanzania kuwa serikali inayoongozwa na Rais Dr. Samia Suluhu Hassan, imedhamiria kufanya uchaguzi huru na wa haki kuanzia wa serikali za mitaa mwaka huu 2024 na uchaguzi mkuu wa 2025.

Kinana ameyasema hayo leo Machi 5, 2024, jijini Dar es Salaam alipokuwa akitoa salamu akimwakilisha Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Dr. Samia S. Hassan katika Mkutano Mkuu wa Chama cha ACT -Wazalendo.


Abdurahman Kinana aipa 5 ACT Wazalendo​

March 5, 2024
DAR ES SALAAM:


CHAMA cha ACT Wazalendo kimepongezwa kwa kuwa chama cha mfano kufanya siasa za hoja na si vihoja.
1731166814518.jpeg


Hayo yamesemwa leo Machi 5, 2024 na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Omar Kinana akimuwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan katika Ufunguzi wa Mkutano wa Taifa wa Chama cha ACT Wazalendo jijini Dar es Salaam.

Amesema “ACT kimekuwa chama cha hoja na si vihoja, tumekuwa tukiwafuatilia, na sisi CCM hatuichukulii ACT kirahisi,”amesema Kinana na kuongeza .
“Kila ilipotokea fursa ya kuunda serikali ya umoja Zanzibar ACT imekuwa tayari mstari wa mbele, kuna wakati mlipitia kipindi kigumu kidogo mkashusha tanga mkapandisha tanga, halikuwa jambo rahisi mlifanya hivyo bila mifarakano mkafanya kwa umoja na maslahi ya chama chenu,”amesema.
Aidha, Kinana amesema kipindi chama hicho kimeondokewa na kiongozi wake Mkuu Maalim Seif Sharif Hammad ambaye alikua nguzo kuu ya chama hicho baadhi walijiuliza itakuwaje ACT Wazalendo bila Maalim Seif.


“Nahakika wanachama wenu walijiuliza itakuwaje bila Maalim Seif, ila marehemu Seif Sharif Hammad hakujenga mtu alijenga chama, alijenga taasisi, chama chenu kimeendele kuwa imara, nawapongeza viongozi, pia mdogo wangu Zitto Kabwe kwa uongozi madhubuti wenye busara nyingi na kukiwezesha chama hiki kuwa chama kilichotulia,”amesema Kinana.
Aidha, amesema Zitto amekubali kuzingatia matakwa ya katiba, baada ya vipindi viwili ameamua kukaa pembeni sio kustaafu kwa kuwa umri wa kustaafu bado.


“Baba wa Taifa ( Mwalimu Julius Nyerere) alipokuwa anaondoka kwenye uongozi wa Urais akabaki kuwa Mwenyekiti wa chama, wapo waliohoji kwa nini amestaafu Urais lakini bado yupo kwenye Chama?
“Akawajibu ‘before you step down step aside’, naamini Zitto hatokuwa kiongozi lakini atakuwa mshauri mzuri wa chama chake,”amesema Kinana.
1731166884407.jpeg

Aidha, amempongeza pia Mwenyekiti wa chama hicho, Duni Haji Duni, licha ya kupitia mambo mengi mazuri na mabaya, na mengine mazito ya kuuzunisha lakini amebaki imara ameweka mbele maslahi ya watanzania kuliko maslahi yake binafsi
 
Mbona kuna Vyama vingi tu havina Ruzuku lakini vimesimamisha Wagombea Kibao 😂😂😂

..Ccm jaribuni kujiendesha kwa ruzuku kiduchu, au sifuri, kama wanayopata vyama vya upinzani tuone mtafika wapi.


..au waachiene wapinzani wamiliki Tume ya Uchaguzi, Polisi, na mahakama, tuone kama Ccm wote hamtaacha siasa.
 
Mfano umetolewa hapo kwetu Kilosa!
Wilaya ya Kilosa ni Wilaya kongwe sana hapa TZ, lakini ni Wilaya iliyoko nyuma sana hapa nchini kimaendeleo na kila kitu kiujumla, Wilaya hii imetawaliwa shikiliwa na CCM kwa asilimia karibia 85 hadi 90.
Mimi ni mzaliwa wa hapo lakini sitegemei kuwepo hapo hata kwa muda wa mwezi tu, nimekimbilia huku usukumani napata pesa ya tonge langu na familia yangu kwa raha zangu, nipo huku zaidi ya miaka 30 sasa.
 
09 November 2024
Kilindoni, Mafia
Mkoa wa Pwani
Tanzania

MAFIA YAKUMBWA NA RUNGU LA WAGOMBEA KUENGULIWA

Mwenyekiti wa chama cha ACT- Wazalendo jimbo la Mafia mkoa wa Pwani Tanzania alaani wagombea wa ACT Wazalendo kuenguliwa


View: https://m.youtube.com/watch?v=DXMtSznvxf0

ACT Wazalendo yenye ngome imara ya wananchama na wapenzi kisiwani Mafia mkoa wa Pwani waelezea vituko vya wasimamizi wasaidizi kuwaengua wagombea wa chama cha ACT Wazalendo kwa sababu za kibaguzi, maana sababu wanazozitaja wasimamizi wa uchaguzi hazitumiki kwa wagombea wa CCM...

Pia sababu hizo ni haramu na siyo zilizotamkwa katika kanuni na sheria za usimamizi wa chaguzi za mitaa, vijiji na vitongoji kwa ajili ya uchaguzi wa November 2024 kama zilivyotolewa na waziri wa Ofisi ya Rais TAMISEMI
 
Back
Top Bottom