Msisahau kwamba akina Tundu Lisu walizushiwa makesi ya makosa ya kutisha mara baada ya uchaguzi. Aliyewazushia hayo makesi hayupo lakini uzushi wenyewe bado upo, haujafutwa. Wataweza kukamatwa wakirudi. Kama viongozi wanapenda Lisu na Lema warudi basi ni kiasi cha kuwafutia madai ya makesi tu. Ni makesi ya kisiasa, yaliyolenga kuwafunga maisha.
Kama Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hasan anataka kujenga tena umoja basi aanze kwa kuwafutia viongozi wa upinzani hizo shutuma za kisiasa zilizoanzishwa chini ya uongozi uliopita. Maana polisi bado wana amri ya kuwakamata.