Tundu Lissu yupo sahihi, tunapinga umungu mtu ndani ya vyama vyetu sio CHADEMA tu bali hata CCM

Mwabukusi for president of URT


JESUS IS LORD&SAVIOR
 

Tunasimama na TAL:

Mbowe ajiuzulu mara moja kama Mwenyekiti wa CHADEMA
 
Tlaatlaah Njoo huku kûna swali Lako
mapinduzi ni falsafa hususani katika uongozi wa vyama hususani CCM.

lakini pia ni dhana ya mabadiliko kutoka kwenye hali fulani, mathalani ya udhalimu kwenda kwenye ahueni...

actually,
chimbuko lake hasa nadhani ni katika kujikomboa kutoka kwenye utumwa ulokua umepambwa na ubaguzi, udhalimu, unyonyaji, na kujiweka huru, katika usawa, haki, kujitegemea n.k.

hata hivyo,
tafsiri huru kulingana na maoni, mtazamo na mazingira ya mtafsiri ni muhimu sana kuheshimiwa 🐒
 

Vizuri.
 
katika siasa, Mbowe ni zaidi ya TAL

Katika Angle Ipi?

Unajua hata hivi Leo ukipiga Kura humu JF Kwa weñye iD fake LISU anaushawishi kuliko Mbowe.
Unajua ni Kwa nini?

Mbowe ni Kiongozi mzuri Kwa sababu ya utulivu wake wa kimaamuzi.
Sio Mkali Sana na Msimamo wake ni ule wa Kawaida.
Tofauti na LISU àmbaye NI aina ya Watu weñye Msimamo Mkali Jambo ambalo linaweza kumfanya asifanye maamuzi Kwa utulivu

kiuongozi kama ningeambiwa niwapange Mbowe na LISU Kwa cheo Basi Mbowe angepaswa awe Rais alafu LISU awe Waziri Mkuu. Ili LISU apate wa kumfunga speedGoverner.

Lisu na Magufuli wanafanana Kwa namna Fulani hasa ya Ukali na kuwa very strictly
 
Mimi nataka CHADEMA isambaratike tu maana ni chama kisicho na msaada wowote ule katika ustawi wa demokrasia hapa nchini..kazi yake kubwa ni kuzusha uongo uongo, uchonganishi,undumila kuwili, unafiki,kudandia matukio badala ya kuwa na sera na ajenda za kueleweka na kugusa maisha ya watanzania.

CHADEMA acha ife na kupasuka pasuka tu.
 

Hauko peke yako, CCM na hata wale wengine; tangu lini mlifurahia Lissu kuwa hai?
 

Ungeweka na kile original alichokisema Tundu Lissu huko space wakati akihojiana na wale jamaa waliokuwa wanamuuliza maswali, basi utagundua kuwa uchambuzi wako uko nje kwa 95% kumhusu TL na alichokisema..

Nilifuatilia mjadala/mahojiano hayo mwanzo mwisho. Wale jamaa walikuwa wanauliza swali hili moja tu muda mrefu kwa kurudiarudia ili mradi aseme;

1. Ana ugomvi na Freeman Mbowe M/Kiti wake (hoja ambayo alishaitolea maelezo mara kibao akihojiwa na TV mbalimbali, kwenye mikutano yake nk kwa uwazi kabisa kuwa hana ugomvi wala mgogoro wowote na mwenyekiti wake isipokuwa kutofautiana ktk mitizamo ambako kuko kila mahali palipo na watu wawili au zaidi..)

2. Na kwa sababu hiyo ☝🏻☝🏻, ktk namna ya kurudiarudia swali hilo pengine walitaka aseme kuwa yuko tayari kutoka CHADEMA na kwenda kwingine hususani CCM kitu hawakukipata toka kwake..

Baada ya kuwachoka na swali lao la kujirudia rudia, ndipo akiwa na hasira kidogo na mfadhaiko ndani yake, akaanza kuwapa elimu na historia yake kisiasa pamoja na historia yote kwa ujumla akiwatumia kina, Hayati Oscar Kambona, Julius K. Nyerere na kauli yake maarufu ya;

"....CCM sio mama yangu, ikitoka ktk misingi yake ninaachana nayo......."

Aidha aliendelea kuwapa elimu vijana wale kwa kuwaambia kuwa, vyama vya siasa ni taasisi za kihiari. Mtu hujiunga kwa hiari na anaweza kutoka kwa hiari yake, kwa kufukuzwa kwa kufuata taratibu halali au kuondolewa kwa mizengwe. Yote haya yapo na yanatokea ktk vyama vya siasa..

Akasema pia kwamba, yeye Tundu Lissu alijiunga CHADEMA miaka 20 iliyopita kwa kuvutiwa na misingi ya kuanzishwa kwake..

Na kama CHADEMA itatoka ktk misingi hiyo, basi anakubaliana 100% na Baba wa taifa Hayati Mwl. J. K. Nyerere kuwa chama cha siasa (cha kwake ni CHADEMA) si dini na wala si mama yake, anaweza kuachana nacho kwa sababu ya kutoka ktk msingi wa kuanzishwa kwake na yeye kujiunga nacho. Hoja ya "MIUNGU WATU" ni yako haikutoka kwenye kinywa cha Tundu Lissu na ndiyo maana huna ushahidi huo wa aidha video au sauti tu akitamka hivyo..

Shida ya wale vijana waliokuwa wakihojiana na Tundu Lissu ni moja..

Hawakumuuliza swali moja muhimu sana Tundu Lissu baada ya kusema kuwa;

".....Siku CHADEMA ikitoka ktk misingi na itikadi yake, atatoka kwa kuwa CHADEMA siyo dini ya Mungu wala si mama yake...".

Swali hilo lilipaswa kuwa;

"...Vipi Mh. Tundu Lissu unadhani kwa sasa CHADEMA bado imesimama ktk misingi ya kuanzishwa kwake...?"

Namna ambavyo angejibu swali hili, basi wangeweza kuwa na hitimisho zuri sana ya aidha atatoka kesho au leo na wana mgogoro na mwenyekiti wake au la. Na kwa jinsi Tundu Lissu alivyo honest and genuine bila woga wala hofu, wala asungemung'unya maneno, anggesema hapohapo kwa uwazi na mchana kweupe kwamba ameichoka CHADEMA au la, kuna Mungu mtu au la...

Lakini hawa waswahili wakapitwa na fursa hiyo muhimu sana na badala yake wanaanzisha majungu na uzushi tu..

Na watu kama wewe Robert Heriel Mtibeli wajuvi wa kucheza na lugha ni rahisi kuwa - manipulate watu kwa uongo...

Lakini kiukweli hata wewe ni walewale, tatizo lako ni Freeman Mbowe. Huyu ndiye unayem - label kama "Mungu mtu" ukweli ukiwa ni ZERO. Na kuhalalisha hoja yako ukaingiza na CCM ndani yake..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…