Uchaguzi 2020 Tundu Lissu yupo tayari kwa urais wa Tanzania, hatanii

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu yupo tayari kwa urais wa Tanzania, hatanii

Huyu atatuvuruga tu watz, atulie kwanza akue kisiasa. Bado anamijihasira na hakika hata hiyo baadae akiupata uraisi nchi itazama ktk wimbi la udini na ukabila.
 
Huyo mropokaji aendelee kujifurahisha
Watu wanakuja kwenye mkutano wako na mabango ya kukusifu Kisha unawaambia yapelekeni vitandani kwenu myatandike mlalie na wake zenu'' ccm wanapigia makofi na vigeregere kauli hiyo" kwa akili hizi nakuelewa sana unapomuita Lissu mlopokaji maana nahakika huwa humuelewi
 
View attachment 1486569
Nilimsikiliza Mheshimiwa Tundu Lissu na nasikitika kwamba sikubaliani naye jinsi alivyoeleza shutma juu na dhidi ya Mwalimu Julius Nyerere, Baba na Muasisi wa Taifa letu.

Inajulikana na umma wa Watanzania, kwamba mimi binafsi, kama Waziri wa Fedha, nilitofautiana na Mwalimu, nikajiuzulu Uwaziri Decemba,1979, nikimwomba ateuwe Mtanzania mwingine atakayeshauri mambo ya Uchumi na Fedha. Lakini tuliendelea kuwasiliana kwa maelewano bila chuki, na hata aliniteuwa niwe Mwakilishi wa Tanzania na Afrika inayoongea Kiingereza katika IMF (Shirika la Fedha Duniani) chini ya miaka mitatu baadaye Novemba, 1972.

Nimekuwa na mawasiliano na maelewano mazuri sana na Mwalimu hata baada ya kuasisi CHADEMA, Julai 1992 na tulipokamilisha Katiba na Sera za Chadema, nilimtembelea Nyumbani kwake Butiama nikampa azisome ajionee jinsi tulivyonuia kuwahudumia Wananchi wetu. Hata siku moja siwezi kumtusi Muasisi wa Taifa letu. Iwe ni mwiko pia kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo kumtusi Baba wa Taifa.

Ningewashauri uongozi wa Chadema na hasa Vijana wa M4C (Vuguvugu la Mabadiliko) tuendelee na uhamasishaji : kwa umakini, tukiwa na huruma kwa wanyonge maskini wa kutupwa, tukijiandaa kwa umakini na kiutaalamu Sera na Mikakati ya kuwakomboa toka katika umaskini wa kutupwa kwa kutumia nguvu ya umma (Peoples Power) tukitumia mikakati sahihi: kwani Hakuna Kulala Mpaka Kieleweke:

Mikakati na Sera sahihi ikiwa ni kutumia misingi ya Uchumi na Miundombinu tulionayo licha ya uhalisia dhoofu tulioridhi; tukiwaenzi walioijenga na kuturidhisha kwa unyofu wao.

Roho ya Julius Nyerere ilale mahala pema Peponi. Amen!
Mkuu Nyerere hakuwahi kuwa mungu wa Tanzania Wala nchi yoyote.ni ujinga wa kiwango Cha juu kabisa kuamini kuwa Nyerere hakuwahi kufanya makosa au kuamini kuwa utetezi wa mtei au mtu mwingine yoyote yule ndo kidhibitisho kuwa Nyerere hajawahi kufanya makosa
 
Ameandika tena Tundu Lissu

Mzee Jomo Kenyatta wa Kenya, alikaa gerezani miaka tisa. Alipotoka kifungoni alienda moja kwa moja Ikulu ya Kenya kama Rais.

Fidel Castro alikaa gerezani miaka miwili gerezani, lakini aliishia kuwa Rais wa Cuba. Nelson Mandela alikaa gerezani miaka 27, naye aliishia kuwa Rais wa Afrika Kusini iliyokuwa huru.

Wapo pia akina Kwame Nkrumah, Jawaharlal Nehru, Robert Mugabe n.k.

Mifano ni mingi sana throughout human history. Anayeogopa machungu ya gereza basi hayuko tayari kwa ufalme wa kisiasa.

Hakika huu ni ujasili ulio pitiliza na inaonyesha kadhamilia kuwakomboa Watanzania.

View attachment 1486565
Lissu The Greatest
 
Wanao kimbilia huo utetezi wamefirisika kisiasa na wamekosa hoja
Mkuu Nyerere hakuwahi kuwa mungu wa Tanzania Wala nchi yoyote.ni ujinga wa kiwango Cha juu kabisa kuamini kuwa Nyerere hakuwahi kufanya makosa au kuamini kuwa utetezi wa mtei au mtu mwingine yoyote yule ndo kidhibitisho kuwa Nyerere hajawahi kufanya makosa
 
Back
Top Bottom