Yohimbe bark
JF-Expert Member
- Sep 1, 2019
- 2,160
- 5,728
Kwangu mimi hazikusomeka kwa wakati huo ila hela ipo na nitarudi Mungu akipenda nikiwa nimejipanga vizuri.Vipi ramani zilisomeka pale Tunduma ?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwangu mimi hazikusomeka kwa wakati huo ila hela ipo na nitarudi Mungu akipenda nikiwa nimejipanga vizuri.Vipi ramani zilisomeka pale Tunduma ?
I stayed at majengo mapya for a year. Then Mpemba Near Uzunguni filling station for a year too.Unalala kokote ila Kwa maeneo ya Majengo mapya, mwaka, Kwa mwaka joka, Kwa mjeshi, kilimahewa, Nyerere, Kwa Msomali, Msongwa, dampo, Msongwa, half London ni maeneo yenye usalama mzuri
😂😂😂😂😂😂😂😂😂😄😄😄 Nimecheka Sana ulivyojibu Mkuu... Umejibu kibabe Sana na shoti endi kilia.... Nimefatilia huu uzi kuanzia mwanzo na jinsi ulivyokua mnyenyekevu kuomba konekisheni ili uende Tunduma ukapewa Kila kitu na kila mchongo mpaka kutafutiwa Loji. Ila kwenye ripoti ya matokeo Sasa.... Daaah🤣🤣🤣 Kibabe Sana mpwa
😂😂😂 kwani nimezingua mkuu?😄😄😄 Nimecheka Sana ulivyojibu Mkuu... Umejibu kibabe Sana na shoti endi kilia.... Nimefatilia huu uzi kuanzia mwanzo na jinsi ulivyokua mnyenyekevu kuomba konekisheni ili uende Tunduma ukapewa Kila kitu na kila mchongo mpaka kutafutiwa Loji. Ila kwenye ripoti ya matokeo Sasa.... Daaah🤣🤣🤣 Kibabe Sana mpwa
Aliyemtafutia wrnyeji no mimi😄😄😄 Nimecheka Sana ulivyojibu Mkuu... Umejibu kibabe Sana na shoti endi kilia.... Nimefatilia huu uzi kuanzia mwanzo na jinsi ulivyokua mnyenyekevu kuomba konekisheni ili uende Tunduma ukapewa Kila kitu na kila mchongo mpaka kutafutiwa Loji. Ila kwenye ripoti ya matokeo Sasa.... Daaah🤣🤣🤣 Kibabe Sana mpwa
Mkuu hujanipa feedback , Mimi Jamaa yake Solo , aliyekytafutia lodge pale African?😂😂😂 kwani nimezingua mkuu?
Mara ya Mwisho alikuwa Chunya , tunataka Report ya Chunya, mambo yalikwensaji?Soma posts za juu ashasema hayupo huko Tena mambo yalimshinda Ila kuna hela
Mkuu tunasibiri Report ya Chunya , yule Dada wa kuuza pochi mlifika nae Salama kwenye Biashara?😂😂😂 kwani nimezingua mkuu?
Kwanza samahani mkuu naona ulinitxt pm lakini pm yangu haifunguki mda sasa, kuhusu yule dada niliuza nae vipochi one week tulikua tunachukulia soko la mwanjelwa kwenye duka la jamaa mmoja anaitwa shafii then tunaenda kuuzia makongorosi aisee ule mziki sio poa vumbi la makongolosi plus jua ni hatari, inafika jioni umeuza vipochi viwili nikaona sio nikakimbia😂😂Mkuu tunasibiri Report ya Chunya , yule Dada wa kuuza pochi mlifika nae Salama kwenye Biashara?
Mkuu solo alinipa ushirikiano lakini sio kivile kwasababu hakukumbuka nilivyomuelezea kuhusu wewe jina lako hakulijua ila nilivyomuambia shabiki wa arsenal at least ikasaidia, alinipa ushirikiano wa kawaida wa kunipeleka lodge na kunionesha sehemu ya kula ila nilivyoanza kumdadisi issue za biashara pale tunduma kama alikua mzito hivi ndio maana nikaamua kuondoka kwenda chunya.Mkuu hujanipa feedback , Mimi Jamaa yake Solo , aliyekytafutia lodge pale African?
ChaiHuu uzi ilikuwa niuandike muda mrefu kwa mambo niliyojionea kwenye mji wa Tunduma. Kwa ambao hajawahi fika Tunduma wanaweza kudhani ni ka-mji kadogo ambacho kipokipo tu. Kwa sisi wa Arusha tulikuwa tunaamini Namanga ndo mji mkubwa zaidi wa mpakani kwa Tanzania kumbe kuna Tunduma.
Kinachonifanya niandike ni biashara kubwa iliyoko Tunduma. Ule mji wa mpakani kwa mjasiriamali mdogo ni sehemu sahihi ya kwenda kusoma ramani. Uchangamfu wake unaendana sana na Kkoo tofauti ikiwa ni ukubwa tu. Ila wafanyabiashara wa nguo Tunduma wanawezaje kuuza nguo za jumla kwa bei sawa na ya Kariakoo? Baadhi ya wafanyabiashara huuza bei chini hata kuliko Kariakoo. Kimahesabu imekaaje hii? Hata vitu vingine jamaa wako fair.
Kimsingi Tunduma ni boda kubwa zaido bongo yenye fursa nyingi sana.
Yaani ule mji ni umechangamka kwelikweli.... Watu wanapiga biashara kwelikweliZile deal za Black market upande wapili nyuma ya frame za Viatu ule upande unazalisha sana Madoni Kila mwezi kwenye deal za:-
Vipodozi.
Vitenge.
Mafuta ya Kula.
Sukari.
Sigara .
Mbegu za Mahindi / Zamsed.
Mafazeti used kutoka Zimbabwe, South Africa.
USD ;- zinatoka Congo na unazipata upande wapili, Pombe za Viroba, na Pombe za vichupa vidogo wanauza Bei ya Tshs 1000/= na Viroba vinaanzia 250-500 maeneo ya Black na Iboya.
Kuna matajiri wanspiga Hela kwenye Biashara ya kubadilisha Fedha, yeye ana Supply fedha Kwa Vijana jioni anarudishiwa na Faida , Hao wanaitwa wenye Visima , mtu ana Supply hata billioni Moja Kwa Vijana wake 30 wanaokwenda kutafuta Dolla Hadi Congo.
Kuna Wababe kwenye Biashara ya Mafuta ya Petroleum kupeleka upande wa Zambia Kuna Yule Msomali wa Petroafrica mwenye upara aliwakamata sana wa Zambia.
Kuna Yule Tajiri wa Valentine Bar ya Pale Boarder na Valentine night club Jamaa anajimbiza sana kaanzia kwenye Bar Hadi kushika soko la Viatu Hadi Kumiliki Kusoma pale Kisimani.
Yupo Dubai Tyre Jamaa anakimbiza sana kwenye biashara ya Tyre Sasa amehamia kwenye Mafuta Bei zake za Tyre ni kama Dar es salaam. Yupo yule Manyanya ameshika biashara za maduka balaa pale Boarder piya yeye ndie amehamia kwenye vituo vya Mafuta, Wapo Hawa Jamaa wa Olympic petroleum anauza Mafuta Kwa wholesale Kwa Bei ya Depot'.
Mjii wa Tunduma una Bank zaidi ya Sita, Petrol Station zaidi ya Hamsini, lodge na Bar zimetapaka Kila baada ya nyumba mbili or tatu,