Tunduma ni mji wa kipekee. Mapigo yake ni kama Kariakoo

Tunduma ni mji wa kipekee. Mapigo yake ni kama Kariakoo

Kwa biashara ya vipodozi inatakiwa mtaji kuanzia shi ngapi?
Kumbuka kwanza hiyo biashara sio Halali, utakuwa unafanya Kwa magendo mtaji unaweza kutaifishwa na wewe kufungua. Ukijua Hilo ndio uanze kujuwa mtaji unaohitajika sio tu wa kununulia mzigo wa vipodozi , Weka na budget ya kulindis huo mzigo ukiwa barabarani in case ukishikwa utoe Hela faster uachiwe
 
Huu uzi ilikuwa niuandike muda mrefu kwa mambo niliyojionea kwenye mji wa Tunduma. Kwa ambao hajawahi fika Tunduma wanaweza kudhani ni ka-mji kadogo ambacho kipokipo tu. Kwa sisi wa Arusha tulikuwa tunaamini Namanga ndo mji mkubwa zaidi wa mpakani kwa Tanzania kumbe kuna Tunduma.

Kinachonifanya niandike ni biashara kubwa iliyoko Tunduma. Ule mji wa mpakani kwa mjasiriamali mdogo ni sehemu sahihi ya kwenda kusoma ramani. Uchangamfu wake unaendana sana na Kkoo tofauti ikiwa ni ukubwa tu. Ila wafanyabiashara wa nguo Tunduma wanawezaje kuuza nguo za jumla kwa bei sawa na ya Kariakoo? Baadhi ya wafanyabiashara huuza bei chini hata kuliko Kariakoo. Kimahesabu imekaaje hii? Hata vitu vingine jamaa wako fair.

Kimsingi Tunduma ni boda kubwa zaido bongo yenye fursa nyingi sana.
Huu sio Mji wa kuishi Bali kufanya biashara na kuondoka.

Kamji la hovyo sana angalia kalivyo Pauka hapa 👇

View: https://youtube.com/watch?v=1bV5XC-yOH4&si=oCy7v6UjOmb3qtwM
 
Wakuu kumekucha tunduma hapa mishe kama zote tupeane michongo basi kwa wenyeji naona mnakaza[emoji3] ila mji unamishemishe sijawahi ona kama kariakoo vile, now naenda chunya makongolosi kupaangalia pia jioni nitarudi tunduma mjini fursa nitakazoziona huko nitawaambia wakuu.
Poa mkuu , utatupa mrejesho
 
Maeneo tulivu ni Kuanzia Majengo mapya nyuma ya Gapco petrol station nenda ma huo upande Hadi mwisho wa Mji kuelekea Sumbawanga Road, piya Nyerere secondary , Msongwa, njia panda Msongwa Hilo eneo ndio Kali Kwa Tunduma. Piya jaribu Dampo pale jirani Kwa Furaha, Momba garage, Kwa mchaga wa Viatu, Kwa Mzee Joseph Baba mkwee wa Manyanya like eneo limetulia . Piya mtaa wa Manyanya nyuma ya kabisa la Roma hapo kwenye Rasta barabarani
Mkuu AGROPRODUCT hongera kwako! Unaijua vizuri Tunduma, "boda la wajanja". Na husiti kusambaza upendo kwa wana.
 
Back
Top Bottom