Walichokiangalia Wadau ni wengi na ukubwa Wa kariakoo unachangiwa na population yote ya Tanzania wanaitwgemea Kariakoo, Ila wanaosifia Tunduma wanaangalia. Udogo wa Mji na Shughuli Zinazofanyika Tunduma utaona napo Panaukubwa kiasi Gani kwenye Shughuli za Kiuchumi. Naifahamu sana Kariakoo na ni mwenyeji mitaa na piya
Nikiangalia Shughuli Zinazofanyika Pale Tunduma kuanzia Mpemba kwenye parking ya Malori, Chapwa, Halafu uangalie kuanzia pale custom halafu upande Juu kusogo kuanzia polisi yale Maduka ya matairi na simu uingie ndani kwenye Maduka ya nguo pale sokoni, uende kwenye Maduka ya electronics , Uende Kwa Wauza Fedha mikonini, Uingie soko la Viatu Nyuma ya Dukani Kwa Manyanya. Halafu usogie Kidogo Black Market uone Elivyoshikwa na Wandali na Wanyakyusa,
Halafu uone Soko la Fedha Mkononi lilivyoshikwa na Wasafwa na Wanyakyusa, Nenda kwenye Maduka ya Nguo ni Wakinga na Wandali, Electronics na Simu ni Wakinga Maduka ya Spare na Hardware ni Wandali na Wakinga, Kwenye Matairi ni Wamalila. Ukiangalia wengi wa watu na biashara Bado Tunduma ipo vizuri Kwa ujumla ukiwacha KKOO hakuna sehemu kama Tunduma Tanzania Hii Kwa mzunguko wa Fedha. Ukienda kwenye mabanki ndio utaona huo mzunguko Kuna wateja watatu tu wanaweza hudumiwa zaidi ya masaa mawili kwenye bulk teller.