Hii mishetani ndiyo maana YESU ALIISHUTI PEUPE KUWA. MSIWASHITAKI WATU KWA UONGO.. LAKINA HAYASIKII ALAFU YANATAKA KWENDA MBINGUNI. Waambie wanaowatuma kuonea watu wakumbuke kuwajengea mbingu yao ya matofari ya kuchoma.
Hawawezi kuona makosa yao wakati Viongozi wa Dini wameamua kuungana na watesi na kushangilia dhulma kwa binadamu wenzao kwa sababu tu ya mahaba ya kivyama na Kikabila.
Katiba iliyopo inababisha nchi kuwa na vitendo vya kikatili kwa kisingizio vya kulinda amani. Amani imekua ni jambo la kutumia nguvu kuwasababisha wenye uroho na ulevi wa madaraka kuendelea kubaki kwenye madaraka.
Tatizo kubwa ni MTU mmoja kuwa na madaraka makubwa ya kuteua hata watu wa kabila lake tuu au dini yake tuu au ukanda wake tuu bila kuulizwa au kuwajibishwa kikatiba.
Katiba imetoa mwanya mkubwa sana kwenye uteuzi. Ndio maana MTU kama Sabaya bado yupo Kwenye Ofisi ya umma inayogharamikiwa na asilimia kubwa sana kwa kodi ya wapinzani wa Ukanda huo. Yupo pale kuwaumiza walipa kodi kwa sababu tu ya kulinda kiti chake kinachompa chakula.
Hali ikiendelea hivi kwa vyama vya siasa kufanya Uhuni wakishirikiana na baadhi ya viongozi wa vyombo vya dola wanaolinda maslahi yao kikanda au kidini au kikabila mwishowe watapoteza mvuto kwa jamii.
Afrika bado kuba Ukabila ,Udini, ukanda na ushabiki wa kivyama mbali kabisa na Utaifa na uzalendo wa kweli. Ili kuondoa udini ,ukabila,ukanda na uvyama ni lazima watu wafanye siasa kwa Haki na usawa na pia kujenga utaifa na kuondoa huu uhunu. Ukichunguza vizuri utagundua kuwa hata ukatili na ubabe unafanywa kwa misingi hiyo hiyo ya kulinda hayo. Na wanayoyafanya wanakua na wazo hilo hilo kuwa sasa ni zamu ya dini yetu ,kabila letu ,ukanda wetu n.k watatukoma.
Waafrika tubadilike na tukatae kugawanywa na watu wachache walioahidiwa madaraka au wanaolinda madaraka yao na familia zao kwa mgongo wa zamu yetu.